Kelele za mashabiki zinazosikika wakati wa mechi EPL

kikiboxer

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2017
Posts
3,668
Reaction score
9,809
Wakuu salam.
Wale wafuatiliaji wa mpira wa mabeberu hapa nazungumzia ligi mbali mbali za ulaya hasa ligi pendwa Epl wanafahamu kwamba kipindi hiki cha covid19 mashabiki wamezuiwa kujumuika viwanjani kushangilia team zao.

Sasa basi kwa sisi tunaoangalia kwenye Tv kuna kelele za mashabiki bado tunazipata kama vile wapo uwanjani.
Yani unakuta goli likifungwa wanashangilia zaidi au kosa kosa zile unasikia aaah.!
Wakati mwingine mchezaji akifanya foul mbaya wanam-booooh! Same kwa mchezaji akiwa anatoka unasikia makofi.

Swali langu ni je hawa mabeberu wameweka zile sauti automatic kwamba zinasense mpira unavochezwa au kuna mtu/watu wanacontrol hizi sauti.
Yote kwa yote mabeberu wamecheza sana kutuwekea hii kitu.
 
Ukiangalia mpira mashabiki huwaoni
 

Hizo sauti zinaingiziwa studio!
Zinachukuliwa sauti za mechi ambazo zilishachezwa, then zinachanganywa changanywa kutokana na matukio yanayoendelea uwanjani!
Wazalishaji wa FIFA 20, na EA sport kwa kiasi kikubwa ndio wanaohusika kufanya hayo!
Lakini pia utambue wachezaji wakiwa uwanjani hizo sauti hawazisikii, ni wale watazamaji wanaofuatilia kwa tv ndio huwa wanaziksikia pekee! Pia zipo channels ambazo zina option ya kuondoa hizo sauti fake za hao mashabiki!
Vile vile kama unafuatilia laliga utaona wanapandikiza mashabiki feki (virtual fans) ili kuleta mzuka zaidi, huku epl wakifunika uwanja kwa kutumia covers ambazo zina rangi/nembo za home team ama wadhamini!
 
Hii inaitwa Artificial Intelligence Technology ambapo tabia za kibinadam zinafanywa na computer na kutoonyesha tofauti.

Mambo mengi tuu yashafanywa hasa kwa kutumia Robots
 
Wazalishaji wa FIFA 20 ni EA electronics

Sent from my SM-M105F using JamiiForums mobile app
 
Ni sauti za mashabiki wa ukweli wale ambao wapo majumbani au Cinema halls. Sauti zinaingizwa katika system kupitia videos calls mf skype..may be
 
Mkuu hii inaweza kuwa kweli ila kumbe wachezaji wao hawazisikii?
 
Sauti za mashabiki Wa yanga mbovu zile😂😂😂
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…