KERO Kelele za mitambo ya kiwanda cha Kerai Construction Ltd- Mbezi Jogoo (Dar) zinatutesa wakazi wa karibu

KERO Kelele za mitambo ya kiwanda cha Kerai Construction Ltd- Mbezi Jogoo (Dar) zinatutesa wakazi wa karibu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Mbezi Juu, Mtaa wa Jogoo, Jijini Dar es Salaam tunaathiriwa na kelele zinazotokana na kiwanda cha zege cha Kerai Construction Ltd, ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa bidhaa za ujenzi.

Kiwanda hicho, ambacho kipo karibu na maeneo ya makazi, kimekuwa kero kubwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani, ikiwemo Mbezi Ndumbwi, ambako, takribani mita 300 kutoka kiwandani, kuna Shule ya Msingi. Aidha, wakazi wa maeneo ya Jogoo na Africana pia wanaathiriwa na kelele hizo.
photo_2026-07-08_08-33-00.jpg
photo_2026-07-08_08-33-03.jpg
Mitambo ya kiwanda hicho hutoa mingurumo mizito wakati shughuli za uzalishaji zinapoendelea. Wananchi tumekuwa tukilalamikia hali hii kwa muda mrefu kupitia nyakati mbalimbali, lakini majibu tunayopata ni kwamba kiwanda hicho kipo eneo hilo kwa mujibu wa sheria na kwamba wakazi wengi waliokaribu walikikuta tayari kikiendelea na shughuli zake.

Huenda ni kweli kwamba baadhi ya wakazi walikikuta kiwanda hicho kikiwa tayari eneo hilo lakini hakukuwepo kelele za aina hiyo. Hata hivyo, hoja hiyo haihalalishi kuendelea kwa shughuli zinazowaathiri wananchi ambao nao wanaishi katika maeneo hayo kihalali na wanamiliki hati za ardhi.
photo_2026-07-08_08-33-05.jpg
Kero kubwa kwetu ni kelele za mitambo hiyo, ambazo hudumu kwa muda mrefu kuanzia asubuhi hadi jioni na wakati mwingine zinaweza kwenda mpaka majira ya saa mbili usiku.

Hali hii husababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi na kuathiri utulivu wa maisha yetu. Kwa sababu hiyo, naomba kutoa wito kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Tanzania (NEMC) kufuatilia na kutatua kero hii. Inaonekana Serikali ya Mtaa wa Jogoo imeshindwa kupata suluhu ya tatizo hili, licha ya wananchi kulifikisha mezani kwao kwa muda mrefu.

Iwapo kiwanda hicho hakiwezi kufanya maboresho ya mitambo yake ili kupunguza kelele zinazosababishwa na shughuli za uzalishaji, basi ni vyema shughuli hizo zikahamishiwa katika eneo lingine ambalo hazitasababisha usumbufu kwa wananchi wanaoishi karibu.
 
Back
Top Bottom