The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Ndani ya kipindi kifupi tunasikia taarifa ya wizi wizi wizi wa mali za umma kila kona, kila mahala na mbaya zaidi na watu wakubwa kabisa.
Juzi hapa tulisikia mkurugenzi huko Gairo wa halmashauri ameiba Nondo na Simenti na akazirudisha baada ya kuombwa na waziri Mkuu.
Leo hii kelele za wizi wa Tanzanite zinasikika kila kona, serikali ina mgodi/shimo lake la Tanzanite kule Mirerani watu wanachukua Tanzanite ya Serikali kama ya kwao. Rais aliliongelea hilo mwezi sa 4 akasema wizi huo ukomeshwe lakini sasa ndio unashika kasi.
Leo unasikia ubadhilifu mkubwa wa pesa za umma chuo kikuu Udom, wizi uliopindukia tena kutoka kwa watu wa ngazi za juu kabisa.
Hujakaa sawa unasimia ubadhirifu wa pesa za umma TBC wa kiwango cha kufa mtu, ni wizi uliopindukia kutoka kwa watu wa juu kabisa pale TBC. Ndio maana TBC ukiangalia taarifa ya habari inabidi ukae jirani na tv maana ubovu wa picha unashindwa kuelewa vizuri picha ni ya mtu ama mbuzi, kumbe hela za video camera za hd zimeibiwa.
Leo unasimia mgao wa umeme kila kona, na hili joto watu wanalala bila kuoga, sasa hivi Dar karibu 60% ya watu wananuka vikwapa, hakuna maji na hakuna umeme, ni hatari.
Tanzania tutafika kweli?