Kelvin John (Mbape) alimkosea nini coach Adel Amrouch?

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Coach wa Taifa stars hajamujuisha mshambuliaji hatari wa Tanzania anayecheza KRC Genk ya Belgium

Coach huyo alipoulizwa ameapa hatomuita tena kuchezea team ya Taifa kwa utovu wa nidhamu aliounesha

Mimi najiuliza utovu wa nidhamu gani huo ambao hausameheki

Kelvin John ni kijana mdogo bila shaka kukosea kupo kwa vijana na coach inatakiwa aweze kumuongoza na kulinda carrier yake

Namsihi coach amuite ni kijana mwenye kipaji kikubwa mno tunamhitaji kama taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makocha wanapaswa kuingiliwa maana muda mwingine wanakuwa na mihemko ambapo inapelekea kuligharimu taifa. Mfano kocha wa Ivory coast kumwacha Wilfried Zaha kama sio mihemko nini. Hakuna anaemzidi zaha kwenye kikosi cha Ivory coast ila kocha kamwacha. Ni kama huyu nae anamwacha Kelvin John sababu ni ipi hasa ?
 
Kabisa hata bila mashabiki na baadhi ya Viongozi Wa nchi kupiga kelele Kule Morocco Zyechi asingeitwa timu ya Taifa sababu ya bifu za kijinga
 
Tupe takwimu zake, ili tumlinganishe na walioitwa.
 
Mnatetea watovu wa nidhamu si ndio?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kelvin John anamzidi nani?
 
Kocha yupo sahihi kumuacha mchezaji kwasababu yoyote ikiwemo utovu wa nidhamu. Kocha Daniel Passarella aliwahi kumuacha Fernando Redondo kwenye kikosi cha Argentina cha WC 1998 kwa kugoma tu kunyoa nywele!😄

Pia, Romario aliwahi kuachwa na Kocha Scolari WC 2002 licha ya Rais wa Brazil wakati huo Cardoso kumuombea aitwe tena kupitiwa vyombo vya habari. Wote hao walikuwa katika kiwango cha juu cha uchezaji. Hii bembelezambeleza ya wachezaji wa Kibongo ndio maana hawafiki mbali!
 
Kipaji bila nidhamu ni sawa na gari bila dereva au ndoa bila mizagamuano. Kocha yuko sahihi kijana bado mdogo anapaswa kuonywa na amepewa nafasi kuomba radhi kwa hiyo uamuzi ni wake aidha aendelee kuushikilia utovu wa nidhamu yake au aombe radhi mambo yaishe.

Tusimuingilie kocha kwa story sijui za Ziyech na watu gani wengine huko kwa sababu hayo ni mambo tofauti na hata kiviwango tunatofautiana. Tumuache kocha afanye maamuzi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…