Kemebos Sec.School aliyefeli sana ana Division One ya 7

Mkuu usipende kutumia AI kwenye vitu local ambavyo havina majibu ya moja kwa moja. AI iulize mfano term, phenomenon au process. Sio kama wabongo wanaipa task ya kupanga menu kwa kutumia buku kwa siku sasa AI ikae ijue leo matembele soko la Mabibo yamepanda bei.

Fact kubwa ni Kemebos kuchuja wanafunzi, ile top wanasajiliwa NECTA kama Kemebos. Wale wanaobaki wanasajiliwa NECTA kama Kaizirege. Hii AI hailijui na ndio la msingi sana. Hayo mengine yote shule kubwa zinayafanya pia.
 
Hiyo shule nimeisikia sana sifa zake, inabidi serikali na watu binafsi watumie ujasusi kujua mbinu gani wanatumia then wazitumie hizo mbinu kujiimarisha kama wanaweza, matokeo yao sio kawaida
Mwalimu wa serikali nyumbani kweke kapangisha bonanza la mchina wanafunzi kutwa kucha wapo pale wanacheza unategemea nini?
 
Kiukweli mimi huwa nayakubali sana matokeo ya shule za kitaifa za serikali. Zimejaa uhalisia. Huwa tokeo lolote likitoka lazima nicheki kwanza Ilboru, Mzumbe, Kibaha, Msalato, Tabora boys & girls, Kilakala, Tech schools (Tanga, Ifunda, Moshi na Iyunga), Arusha sec, Karatu, Arusha day, na Old Moshi.

Nikimaliza hao natazama shule za maeneo ya nyumbani. Oljoro, Mwandet, Kimaseki, Kaloleni, St Joseph Ngarenaro, Oldadai, Naura, Winning Spirit, Makumira na Kikatiti.

Mwisho namalizia na Feza schools, St Francis, Marian, Kemebos, Ahmes, Canossa, Precious Blood, Tengeru boys nk
 
Hizi LLM AI zina data za maana kuhusu Tanzania kuliko serikali yenyewe inavyojijua, research utaelewa
 
Hiyo ni kwa baadhi ya shule tu
Lakini shule ambazo wanafunzi wake ni vipanga na wanafaulu kulingana na uwezo wao zipo nyingi tu
Sio kila shule inatumia janja janja
 
Sasa kama washangaa Kemebos, ukiwaona St. Francis utafanya nini. Angalia GPA hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…