Kemebos Sec.School aliyefeli sana ana Division One ya 7

Serikali tunailaumu kwa namna inavyoendesha siasa za kionevu lakini kwenye Elimu hapana inahudumia watu wengi mno mpaka vijijini wasio na exposure yoyote ya dunia.
Serikali iache fee control na iwape flexibility kwenye curriculum zao for private schools, na taxes ziko juu sana, control and heavy handed ina discourage private education na kuifanya more expensive, waondoe pua zao watu wafanye kazi
 
Sasa wewe kiande kweli unadhani huyo mwanafunzi wa Buza. Kinachomfelisha ni Ubuza uliopo ndani yake au mazingira uanayomzunguka?
 

Halafu mmiliki wake unaambiwa ni darasa la 7 alikuwa Fundi Gereji na Dereva wa Malori, aliamua kuanzisha Shule kwa sababu yeye hakusoma, baba yake alikosa ada ya kumsomesha mara baada ya kumaliza darasa la 7.
Interview yake ipo Milardi Ayo - YouTube
 
KAWAIDA kabisa...sisi wengine hayo yote tumeyafanya kwenye shule za KAWAIDA kabisa..

Tena tumesoma kwa kibatarii...tulipo shindwa kuelewa tulikaririii... Imagine Kila kitabu na Kila SOMO tulihifadhii KICHWANI kama JUZUHU 😁
 
Hivi watoto wanaotoka hizi shule huwa wanafanyia kazi wapi wakimaliza shule,nawaza tu,unakutana na mtoto aliyetoka shule kama hizi kwenye interview,huyu lazima yeye atapita tu,na anayetoa ajira huyu hawezi kumuacha,kwahiyo siye wengine wa st.kayumba inabidi tuendelee tu kutafuta vizimba vya kufanyia biashara...
 
Hatutaki watoto ama elimu ya kukariri ndugu check Finland Amsterdam elimu yao ilivyo nzuri .
Unadhani hata watt wangepata alama mia moja wote kwa Kila somo unadhani hapo wangesaidia nini ama wangejiletea faida Gani kwao na kwa Taifa Zima , we need to train our kids to think and Innovate na sio kukariri aka claiming capacity Kama za waziri mmoja ivi wa Malawi, we need to change our education system na sio kumpima mtoto wa kukariri , what then if they scored all 100% marks in their final exams
 
Jidanganye
 
"....aka claiming capacity...."
Mimi mtu wa bima sijaelewa hapo.
 
"....aka claiming capacity...."
Mimi mtu wa bima sijaelewa hapo.
Mtu anakariri kuwa Tanzania ina km ngapi za lami za vumbi ama tuna samaki kiasi gani Sasa baadaye akiulizwa hayo maswali anajibu tunamtukuza kuwa ana akili ama uwezo mkubwa sana wakati hawezi buni chochote yaani analishwa na baadaye anatapika tunasema kuwa ana uwezo mkubwa wakati akatapika alicholishwa so hana impact yoyote. Waafrika huwa wanawazidi adi wazungu kukariri na kufaulu mitihani Ila waafrika hawafundishwi ubunifu ama namna ya kuwaza ili hata waweze kujitengenezea tissue stiki za mdomoni ama pini hata wembe tunashindwa kuwaza namna ya kuzitengeneza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…