Kihongosi: Nafahamu.
Odemba: Yuko wapi Humphrey Polepole?
Kihongosi: Kwanza taarifa za Mheshimiwa Balozi Humphrey Polepole zinafahamika kwamba nini kilitokea, na vyombo vya usalama na ulinzi wa nchi yetu vilitoa taarifa na statement kupitia Jeshi la Polisi kwamba wanafanyia uchunguzi jambo la Humphrey Polepole. Ndio.
Odemba: Kwamba jambo gani lililompata?
Kihongosi: Hata wewe unafahamu kwamba Humphrey Polepole, kwa statement iliyotolewa na Jeshi la Polisi, kwamba alichukuliwa, alivamiwa na watu. Hiyo ndiyo statement iliyotoka, na uchunguzi wa jambo hilo unaendelea.
Odemba: Kwa kuwa huyu mtu alikuwa vile vile ni kiongozi waandamizi ndani ya chama chenu, pamoja na ndani ya serikali. Chama kimefanya jitihada gani ya kumtafuta huyu aliyekuwa kiongozi waandamizi ndani ya chama?
Kihongosi: Chama Cha Mapinduzi kwanza kilisikitishwa sana na tukio hilo, na pia ndani ya chama tulielekeza vyombo vinavyohusika na masuala ya upelelezi na uchunguzi kulichunguza jambo hili kwa haraka ili kiongozi mwenzetu ajulikane yuko wapi. Kwa hiyo sisi kama chama tuliumizwa na tukio hilo, na tuliomba mamlaka zinazohusika zifanye kazi, na mamlaka hizo zinaendelea kufanya kazi katika jambo hilo.
Odemba: Mara ya mwisho kufuatilia swala lake kama chama ni lini?
Kihongosi: Tunafuatilia mara kwa mara.
Odemba: Taarifa mnazopewa... uchunguzi umefikia wapi?
Kihongosi: Sasa taarifa za kiuchunguzi hawajawahi kusema zimefikia wapi kwa sababu ile ni mamlaka nyingine na zina utaratibu wa kufanya kazi. Kwa hiyo tunasubiri watakapokamilisha uchunguzi wao watatuletea sisi kama chama, lakini watapeleka katika familia na watu wengine ambao wanapaswa kupata taarifa.
Odemba: Naamini kwamba ipo siku atapatikana?
Kihongosi: Tunamuomba Mungu iwe hivyo, ndio.
Odemba: Nani ana wajibu wa kujua alipo?
Kihongosi: Vyombo sasa ndio vinaendelea na kazi hiyo. Siwezi kusema fulani ana wajibu wa kujua au mtu fulani. Naamini mamlaka zinazohusika kwa kuwa zinafanya kazi jambo hili, tuzipe muda, wataleta taarifa na Watanzania tutaweza kufahamu.
Odemba: Kumekuwepo na matukio ya utekaji na watu kupotea...
