Kenani Kihongosi: Hatutahangaika kujibu Propaganda wala kutukana

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi @ccmtanzania, @kenanikihongosi amesema CCM haitapoteza muda kujibu propaganda zinazoenezwa na watu wasiolitakia mema Taifa, badala yake itaendelea kuzingatia wajibu wake wa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

Akihutubia wananchi wa Iguguno katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Mkalama, leo Januari 20, 2026, Kihongosi amesema msimamo wa Chama ni kuendelea kufanya kazi kwa weledi bila kuyumbishwa na maneno ya kuchochea au ya kupotosha.

"Tumekubaliana ndani ya Chama hatutahangaika kudili na kujibu propaganda za watu wasioitakia mema nchi yetu. Kazi yetu na mkataba wetu ni kwenda kusimamia utekelezaji wa Ilani, maendeleo yaende kwa wananchi. Hamtatusikia tukitukana huko, hamtatusikia tukipayuka huko," amesema.

Amesisitiza kuwa nguvu yote ya CCM itaelekezwa katika kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na juhudi za serikali.
 
Atajibuje kitu ambacho hakipo,
Hamna propaganda isipokuwa facts, ajibu facts zilizopo!
 
CCM wao ndio wamekuwa mstari wa mbele wa kufanya Propaganda..Projection ndio silaha yao..Wanashutumu wengine juu ya mambo ambayo wao CCM ndio wanayafanya,Mabaya yao wanasogezea wengine.Wanafanya hivyo kukwepa kuwajibishwa,kupumbaza watu na kuondoa fucus kutoka kwenye maovu yao then Wanatengeneza story ya uongo ya kujifanya kuwa wao ndio defenders dhidi ya threats ambazo wao wenyewe ndio wahusika wakuu.Tubaki kwenye Mstari,wapewe facts za Propaganda zao ambao zimeuza Watanzania,Wapewe facts kutokufuata kwao sheria za Nnchi kunavyovuruga amani,propaganda zao za kutaka kutugawa Watanzania kunavyohatarisha Amani,Wao ndio tatizo kubwa sana,Wasinyooshee vidole wengine,Wachutake na wakubali kuwajibishwa.
 
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi @ccmtanzania, @kenanikihongosi amesema CCM haitapoteza muda kujibu propaganda zinazoenezwa na watu wasiolitakia mema Taifa, badala yake itaendelea kuzingatia wajibu wake wa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

Akihutubia wananchi wa Iguguno katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Mkalama, leo Januari 20, 2026, Kihongosi amesema msimamo wa Chama ni kuendelea kufanya kazi kwa weledi bila kuyumbishwa na maneno ya kuchochea au ya kupotosha.

"Tumekubaliana ndani ya Chama hatutahangaika kudili na kujibu propaganda za watu wasioitakia mema nchi yetu. Kazi yetu na mkataba wetu ni kwenda kusimamia utekelezaji wa Ilani, maendeleo yaende kwa wananchi. Hamtatusikia tukitukana huko, hamtatusikia tukipayuka huko," amesema.

Amesisitiza kuwa nguvu yote ya CCM itaelekezwa katika kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na juhudi za serikali.
Hapo kafanya nini sasa! Kakaa kimya?
 
Back
Top Bottom