GE2025 Kenani Kihongosi: Vyama vingine vinaruhusiwa kuja kusikiliza sera za CCM Agosti 28, 2025

GE2025 Kenani Kihongosi: Vyama vingine vinaruhusiwa kuja kusikiliza sera za CCM Agosti 28, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakuu,

Tayari Katibu mpya wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Kenani Kihongosi ameanza kufanya kazi

-----------
Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatarajiwa kuanza kampeni za kuwania nafasi ya Urais ,Ubunge na Udiwani siku ya kesho huku chama hicho kikisisitiza kitafanya kampeni za kisataarabu zitakazo zingatia utu wa Mtanzania

Akizungumza Jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea na kukagua maandalizi ya eneo la Tanganyika Packers Kawe ambapo uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Kenani Kihongosi amesema kampeni hizo zitazinduliwa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan

Aidha Kihongosi ameongeza kuwa katika uzinduzi wa kampeni hizo vyama vingine vya siasa vinaruhusiwa kwenda kusikiliza sera za CCM ambazo zitajikita katika hoja zaidi


 
Back
Top Bottom