OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Nimeangalia mechi zote za Mapinduzi Cup alizocheza Simba Sc. Kuna kitu nimekiona miguuni kwa baadhi ya wanandinga wa Simba Sc.
Nimemuona Kazi akipiga kazi nzuri akiimarisha ulinzi eneo hatari la Simba. Jana dogo sambamba na Kenedy Juma wamepiga soka zuri kwa kujiamini.
Kuhusu Israel Mwenda nimemcheki game mbili za mwisho group stage kwa kweli amebadilika sana. Ni mchezaji wa kufuatiliwa kwa karibu ili arekebishwe makosa machache anayofanya azidi kujiamini
Kuhusu kipa Hussein Abel, mpaka leo bado nashangaa Ally Salum anawezaje kumuweka bench? Sisemi Ally mbovu bali huyu jamaa Abel anamzidi Ally Salum baadhi ya vitu. Fuatilia hata mechi zake msimu uliopita, nafikiri ndio kipa mwenye saves nyingi kuliko.
Jiulize nini kilitokea majeruhi Manula akadakishwa mechi ya Yanga, huku mwamba Hussein Abel akikosekana hata kwenye bench.
Mashabiki tuna wajibu wa kuwatia moyo, kuwaambia mapungufu yao kwa staha ili wazidi kujiamini.