ALERT!
Afisa habari wa KENGOLD katoa ufafanuzi wa kilichotokea jana kuhusu matumizi ya Brand mbili (NIKE na PUMA) huku sababu kuu ikiwa ni kutokana na kuchelewa kufika kwa jezi zao walizoagiza kutoka CHINA .
Jezi zimefika jana jijini MBEYA pia sababu saidizi ni kuwa walikuaa na pensi zao nyeusi lakini sheria hairuhusu kuvaa jezi zinazofana ndani ya mechi moja baina ya timu mbili hivyo ikapelekea kuwaomba wenyeji wao FOUNTAIN GATE FC kubadili jezi hasa upande wa pensi ili wao watumie nyeusi lakini walikataa , hali iliyowafanya wao kuingia katikati ya maduka ya Mjini BABATI kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata pensi za idadi ya pensi 20 lakini wakabahatika kupata pensi za kijani za NIKE hivyo ikawalazimu kuzitumia hivyo hivyo.
Cha kuwapa moyo wanambeya ni kuwa jezi zimeshafika MBEYA ila zinasubiri tu kutambulishwa kwa mujibu wa Afisa habari.