Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi juu ya mishahara na stahiki nyingine za waratibu wa Press Clubs ambazo zilitakiwa kulipwa hadi kufikia Desemba 31, 2025.
Mishahara hiyo ya miezi minne ikiwa imeambatana stahiki zao za kusitishiwa mikataba na michango ya NSSF. Niliona maandiko kadhaa mtandaoni juu ya madai hayo ambayo kimsingi ni ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu.
Kwakuwa waratibu waliondolewa kazini ilibidi ni tafute aliyekuwa mratibu wetu na kumuuliza juu ya hayo malalamiko na ikiwa yana ukweli wowote haswa kuhusu pesa inayodaiwa kutolewa na SIDA ambao ndiyo wafadhilii wakuu wa UTPC. Baada ya kuzungumza nae akanitumia nakala ya barua kutoka kwa balozi wa Sweden nchini Tanzania akisisitiza kuwa wao wameshawapa pesa UTPC kwaiyo hawajui kwanini wao waratibu hawajalipwa.
Ukiisoma barua ya Balozi utastaajabu sana. Kenneth Simbaya, sekretariet yake pamoja na Bodi ya wakurugenzi ikiingozwa na;
1. Frank Leonard (Mwenyekiti Iringa PC)
2. Cloud Gwandu (Mkt Arusha PC)
3. Liliaan Lucas (Katibu Morogoro PC)
4. Salma Abdul - Uyui FM Tabora (Katibu Tabora PC)
5. Musa Musa - Uhuru (M/kit Dodoma PC)
6. Abdallah Mfaume - ZBC (M/Kiti Zanzibar PC)
7. Paulina David - RFA (Mweka hazina Mwanza PC)
Ninyi ndio mlikuwa viongozi wa hao waratibu huko mikoani lakini mmetanguliza maslahi yenu binafsi mmeshindwa kutenda haki huku mkijua mnachofanya ni kinyume cha sheria na haki za binadamu. Mnaleta ushkaji kwenye kuongoza taasisi hii sio sawa.
Nimetonywa kuwa Victor Maleko amekuwa akiwapigia baadhi ya waratibu kuwadanganya kuwa wasilalamike kwenye group lao kuhusu mishahara eti kuna nafasi nyingi za kazi UTPC watawapa hizo nafasi ikiwa hawataongea.
Sasa cha kujiuliza kwanini itumike nguvu kubwa kuwanyamazisha waratibu ikiwa mnachosema ni kweli kwamba hamjapewa pesa na SIDA? Na mnataka kusema mfadhili ni muongo?
Waratibu mnatakiwa mshikamane msiwape mwanya hawa wanyonyaji wenu wadhulumu jasho lenu. Mtakuwa wajinga. Hivyo vitisho ambavyo mnapewa kuwa hamtapewa nyaraka za NSSF kwa ajili ya mafao yenu ni UPUUZI. Hiyo ni haki yenu na ni sheria ndo inayomtaka Simbaya afanye hivyo. MSIKUBALI.
Kwenye hizi Klabu zetu hali ni mbaya sana. Tangu Kenneth aingie mambo hayajawahi kueleweka hatimaye PC nyingi zimekufa. Liko wazi kabisa hilo. Huku kwetu tulikuwa na kikao tunapambana na wadau ili tuendelee kusimama kwasababu tangu Simbaya aingie huduma nyingi zilikatwa. Walivyopewa pesa April 2023
1. Kodi ya nyumba ilikatwa tukapangiwa kiasi cha kulipa ikiwa unakaa kwenye ofisi ya zaidi ya kiasi walichoweka unatakiwa kuhama. Pia kuna baadhi ya klabu hazikupewa kodi na wanadaiwa zaidi ya Million 6.
2. Gharama za maji, umeme na king'amuzi tukanyimwa kabisa.
3. Gharama ya internet kabla yake ilikua laki moja kwa mwezi ikapunguzwa na kuwa 50,000/-mwaka jana ikapunguzwa tena na kuwa 40,000/-
3. Media Day- miaka ya nyuma hadi 2022 fedha za media day kwa kila Klabu ilikuwa Tsh. 3,000,000 lakini kuanzia Simbaya aingie kila Klabu ilikuwa inapewa Tsh. 1,000,000 tu na wakati mwingine tusipewe.
Mwaka jana mwezi May 2025 baada ya SIDA kuwapa fedha za Januari - Agosti 2025 SEK 2,300,000/ ambazo ni zaidi ya
Tsh. Milioni 630, kwenye zoom meeting Kenneth Simbaya akasema kwakuwa fedha zilizoingia ni KIDOGO hivyo gharama zote zilizokuwa zinatoka UTPC kuja kwenye Klabu zetu zitakatwa kwa 20% (na tulikatwa kweli). Cha ajabu alitaka kukata hadi mishahara ya waratibu 20% watoto wa watu wakapambana hadi huko SIDA wakalipwa pesa yao yote. Na ndio maana Victor na wenzie wanatumia nguvu kubwa kuwavuruga waratibu kwasababu anajua NGUVU yao.
Hata hili la sasa hivi waratibu wamepambana hadi kwa balozi wa Sweden wakapewa ushahidi wa fedha zote zilizowekwa UTPC kwa mwaka wote 2025. Ikiwemo fedha zilizowekwa Desemba 2025 SEK 500,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh. Milioni 130.
Fedha hizi ndizo zilikuwa zilipe mishahara ya waratibu na stahiki zao zote. Kwa utashi wa Simbaya akaona walipane wao mishahara, kodi ya ofisi HQ, posho za wajumbe wa bodi (hawa wanakula pesa nyingi bila kazi yoyote nitarudi siku nyingine kwa ajili yao nikikamilisha data zao).
Malalamiko ya waratibu yakawa mengi baada ya kujulishwa na ubalozi kuwa walishatoa pesa UTPC tangu Desemba 2025 na hiyo likuwa Machi 2026. INAUMIZA SANA.
Nawasihi viongozi wenzangu wa Klabu zote nchini tuhakikishe kwanza UTPC analipa mishahara ya waratibu kwakuwa wamefanya kazi na sisi ni mashahidi na tusipokuwa makini Simbaya anaweza kutuangushia mzigo wa kuwalipa waratibu. Pili kwa muda usiozidi miaka mitatu Kenneth Simbaya ameua taasisi yetu tuliyokuwa nayo tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000. Hakuna tena Ofisi pale. Bodi inajua na Sekretariet inajua.
Viongozi wa Bodi mmekubali kutumika na kuingia kwenye kashfa ya matumizi mabaya ya fedha kwasababu ya vipande vidogo mnavyopata huko. Kwa ulafi wenu mmeua UTPC mmeua na Klabu. AIBU YENU MILELE.
Kenneth Simbaya umeonyesha wazi kuwa huwezi kuongoza popote. Ilipofika UTPC ukaifanya kama ni yako. Ukafukuza waliokuwepo ukaajiri wengine kinyume cha utaratibu. Uliwahi kutangaza nafasi ya kazi aliyochukua ANDREW MARAWITI aliyekuwa MISA-TAN? si umemuajiri kwa urafiki wenu tu? Ukamchukua mhasibu aliyekuwa anafanya kazi kwenye taasisi yako Sumbawanga ukamleta hapo UTPC kwa madai kuwa muhasibu aliyepo hawezi kazi. Inawezekana ni kweli ulifuata sheria ya kumuajiri?ulitangaza nafasi akafanya na interview?
Usione watu wapo kimya ukafikiri hatujui yanayoendelea. Tunaumia sana kuharibiwa kwa taasisi yetu iliyotukuza kitaaluma tangu wengine sisi tukiwa tunaanza uandishi wa habari.
MWISHO hizo fedha unazosema utatulipa kwenye mkutano wa kubadilisha katiba ya UTPC walipe watoto wa watu jasho lao. Malizana nao kisheria hatufurahii taasisi yetu kupelekwa CMA kwa vitu ambavyo vinaweza kumalizwa bila makelele.
STEPHEN CHIMALO ni aibu kwako kukaa kimya juu mambo haya SIMAMA watoto wa watu wapate HAKI yao.
VICTOR MALEKO wewe bado mdogo sana. Unavyowaambia waratibu sio wastaarabu eti wanadai pesa kwa fujo ingekuwa wewe ungeweza kunyamaza? Au unasema kwakuwa unajiona UMESIMAMA? Tunajua wewe na mkeo mnafanya kazi hapo UTPC angefanyiwa kama hao waratibu ungembwambia akae kimya? Basi kuwa makini sana USIANGUKE punguza ujuaji una safari ndefu. Simbaya anakutumia kwa manufaa yake na hao kina Marawiti.
Kwa VIONGOZI WA Press Club solidarity forever. TUSIKUBALI KUUA Press Clubs ZETU kwasababu ya mtu mmoja. Hili sakata la waratibu limetupa vitu vingi ambavyo tulikua hatuvijui.
✌️✌️✌️