MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,500
Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limeanzisha safari za ndege za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JFK jijini New York .
Rais Uhuru Kenyatta Jumapili usiku aliongoza hatua hiyo ya kihistoria kwa sekta ya safari za ndege nchini Kenya alipozindua safari ya ndege ya kwanza, KQ Boeing 787-8 Dreamliner.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 234. Tiketi za kawaida zinauzwa Sh89,000
Ndege hiyo itachukua muda wa masaa 15, hii ikiwa imepunguza muda wa zamani wa safari hiyo kwa masaa saba.
Ndege hiyo iliondoka JKIA saa tano kasorobo usiku na inatarajiwa kuwasili uwanja wa JFK saa kumi na dakika 25
Image captionSafari ya kwenda Marekani itapunguzwa kwa saa saba
Miongoni mwa abiria waliosafiri kwa ndege hiyo katika safari yake ya kwanza ya moja kwa moja kutoka Nairobi hadi jijini New York ni Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni balozi Monica Juma na balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec.
Rais Kenyatta alimkabidhi Balozi Juma bendera ya Kenya huku afisa mmoja wa Ubalozi wa Marekani akimkabidhi balozi Godec bendera ya Marekani.
Abiria wengine katika ndege hiyo ni Katibu wa Wizara ya Uchukuzi Esther Koimett na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Kenya Airways Sebastian Mikosz.