insi mauaji ya kutisha ya polisi nane yalivyofanyikaYaani leo nimeenda namanga upande wa Kenya ni misomali tupu kuzidi ata wamasai..!
By Waandishi Wetu, Mwananchi; mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
MATUKIO
Mei, 2016: Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na lile la Mei mwaka jana ambapo Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Saidi Mbwana aliuawa kwa kupigwa risasi.
Oktoba 2016: Kadhalika, Oktoba mwaka jana aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Ally Milandu aliuawa baada ya kuvamiwa na watu wanne, waliompiga risasi mbili.
Novemba, 2016: Novemba mwaka jana, wenyeviti wawili wa vitongoji wa kijiji hicho waliuawa kwa kupigwa risasi.
Januari 2017: Januari mwaka huu, katika kijiji cha Nyambunda, kitongoji cha Mkwandara, watu wasiofahamika walimuua mfanyabiashara, Oswald Mrope kwa kumpiga risasi mbele ya familia yake.
Februari 2017: Tukio jingine ni lile la Februari 3, mwaka huu ambapo majambazi walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga, ambaye alifanikiwa kuwatoroka.
Hata hivyo majambazi hayo yalipomkosa, yalirejea na kumwaga mafuta, kisha kuichoma moto nyumba yake.
Februari 24: Februari 24 mwaka huu, majambazi hayo yalimuua ofisa upelelezi, wilaya hiyo, Peter Kubezya na maofisa maliasili wawili.
Machi 2017: Machi mwaka huu, polisi iliwaua kwa kuwapiga risasi watu watatu waliovalia kike wakati walipojaribu kukwepa vizuizi vitatu vya barabarani wakiwa na pikipiki mbili. Waliuawa katika daraja la Mkapa.