Kenya: Askari Polisi washtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu

Kenya: Askari Polisi washtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Maafisa 12 wa polisi Nchini Kenya wanakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa madai ya kuhusika katika makosa yaliyofanywa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2017, ikiwa ni pamoja na mauaji ya mtoto wa miezi sita.

Mwendesha Mashtaka Mkuu anasema uchunguzi unaonyesha kuwa maafisa wa ngazi za juu ndio wanaohusika na ukatili unaofanywa katika ngome ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika Mji wa Kisumu, Magharibi mwa Kenya.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji anasema mashambulizi hayo hayakuwa ya ghafla bali yalipangwa na kuratibiwa na maafisa hao.

Hakutaja utambulisho wa washukiwa hao, lakini ametoa mwanya wa kuwafungulia mashtaka kwa makosa mbalimbali yaliyofanywa chini ya mamlaka yao - ikiwa ni pamoja na mauaji, mateso na ubakaji.



============

Kenya police to be charged with crimes against humanity

Twelve police officers in Kenya face charges of crimes against humanity for their alleged role in offences committed during the 2017 election period, including the murder of a six-month-old baby.

The country’s chief prosecutor says investigations show that high-ranking officers bear greatest responsibility for atrocities committed in the stronghold of opposition leader Raila Odinga’s hometown of Kisumu, in western Kenya.

Director of Public Prosecutions Noordin Haji says the attacks were not spontaneous but were planned and coordinated by those officers.

He did not reveal the identity of the suspects, but has given the nod to charge the officers for various crimes committed under their authority - including murder, torture, and rape.


Source: BBC
 
Kazi imeanza, visasi na malipo yanafatia
Si hivyo, Kisumu ni ngome ya Raila, maovu haya yalifanyiwa wakaazi wa Kisumu, Kama ingekua Raila ndo Rais basi tungesema kweli kwamba Raila analipiza kisasi kwa mapolisi waliodhulumu wafwasi wa Raila... Lakini ni Ruto ndo Rais, ruto hakupata kura ata asilimia 3 kutoka Kisumu....

Inaonekana kiongozi wa mashtaka alikua ameketia hii kesi kwa muda mrefu lakini alikua anajua akijaribu kuipeleka kotini chini ya serekali ya Uhuru Kenyatta basi angejipata taabani, amengojea hadi Uhuru na watu wake wametoka serekalini ndo sasa amepata uhuru wa kupeleka kesi mahakamani bila vikwazo vya watu wenye ushawishi mkuu.
 
Back
Top Bottom