Kenya asks UN to end Uhuru, Ruto ICC trial

Kenya asks UN to end Uhuru, Ruto ICC trial

Narudia tena,though my Bw Kabaridi, anajaribu kukwepa ukweli,lakini ukweli utabaki pale pale.

naomba niulize.Hivi UN wana-mandate ya kuingilia kesi za icc na kuzifuta? Huyu balozi alikuwa anafanya haya bila baraka za ikulu?

Hawa jamaa wanajaribu kujikosha kwenye swala ambalo wanajua haliwezekani,mimi naona kama vile wanazidi kujichanganya..swala zima la muendesha mashtaka kumuongezea Uhuru mashtaka ya wafuasi wake kutumia silaha ni well culculated. Hapo jamaa hachomoki...mbaya zaidi wanajaribu kuonyesha kwamba hawana imani na ICC...majaji hawako tayari kuwa embarased na kupoteza kazi zao kirahisi

Hivyo,pia swala la Kagame na kuingilia haya maswala yanazidi kumuharibia Uhuruto.

Kitu kingine siku ya kuapishwa kwa Uhuru, Museveni aliishutumu ICC vibaya sana,bila kujua kwamba alikuwa anawaponza Uhuruto...wao na wakenya wengine walimchukulia kama shujaa lakini ukiangalia impact yake deeply inaonyesha kwamba alikuwa anawashtua ICC kukaza uzi na kudig deep na kuwachimbua Uhuruto,ndio maana mashtaka yameongezeka upande wa uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Ukweli ni upi? ukweli ni gani? Crucial Man ni lini ICC wameweza kuthibitisha haya kortini? mashaidi wagani wametokea hadharani kuthibitisha haya? hata hivyo maafa yanazidi kuendelea tana river na hata bungoma licha ya kuwa kenya ni signatories wa ICC, ikiwa ni kweli wanataka kufanya uchunguzi na kujali watu kuuwawa wangetafuta kujua sababu ya mauaji haya. wajaluo wana chuki na wakikuyu lakini lazima utaratibu zote zifatiliwe na ICC ndio mtu aitwe mhalifu.

kinacholeta michafuko afrika mashariki na kuhusika kwa ICC ni mataifa kama DRC na Somalia. Somalia imerejea hali yake na DRC mradi hali ya kawaida itarejeshwa ICC. ikiwa TZ na vikosi vingine vya Afrika kusini watajiondoa hapo haitapata mwanya wa kuingilia Africa. Je, kuhusika kwa TZ na Africa kusini inaweza kuwa inasimamia matamanio ya ICC DRC????? jibu tutajua hivi karibinu. nimetaja TZ hapa sababu wewe ni mtanzania na unahamu sana na ICC na Kenya....

ocampo mwenyewe ndio wanazidi kujichanganya na kutafuta kujikomboa kutoka kwa mtego wamejinasa wenyewe kisa na maana, hawa watuhumiwa uhuru na ruto wamekubali kufanya kazi na ICC ukweli ujulikane. hili limekuwa pigo sana kwao. taswira pia ya majaji wa hague kukosoana wenyewe-kwa-wenyewe na wengine kujihuzulu, (umoja hakuna) ina maana hivi karibuni tutasikia kukawa na deferrals nyingi. ama kweli kuzama kwa meli si kwa mpigo....

ICC sio mahakama huru na utaratibu wao huendeshwa kama vibaraka wa uingereza, maana hutenda mambo kulingana na mabosi wao wa marekani na mataifa mengine yanavyosema.. sioni jambo geni maana hata kidiplomasia umoja wa mataifa una usemi mkubwa kuliko ICC..
 
Back
Top Bottom