Usihamishe mada hadi Somaliland. Tunaongea kuhusu Somalia. Kwa hivyo wewe ulitaka Kenya tuache Al Shabab wazidi kutawala Somalia. Waendelee kukata mikono za watu. Kupiga watu mawe na kukata watu shingo kama kuku kwa makosa madogo madogo huko Somalia.
Mbaya zaidi ulikuwa unataka Shabab waendelee kuja Kenya kuteka nyara watalii na kuwapeleka Somalia? Yaani tulistahili kuendelea kucheka na Al Shabab kwa sababu kama tungeingia Somalia kuwakimbiza basi Eliakeem angesema kuwa sisi ni Aggresor. Hata kama Al Shabab sio serikali bali terror group bado tunaambiwa kwamba tumeattack nchi huru. Kwamba ingekuwa bora kama Kenya ingeendelea kucheka cheka na Al Shabab badala ya kuingia Somalia na kuwaangamiza.
Kwa mawazo mgando kama huo basi inaonekana hata nyinyi mlienda Congo kama aggresors. Mlienda huko kuattack serikali ya nchi huru bali hamkuenda kuattack rebel group iliyokuwa inanyanyasa watu (M23).