Iconoclastes
JF-Expert Member
- May 26, 2014
- 4,091
- 2,511
Niliuliza bei ya mahitaji ya kila siku mf chakula katika migahawa ya kawaida, vinywaji baridi na pombe za kawaida kama bia,petrol umeshajibu ni sawa na. huku tu,bei za nyumba zakupanga katika mitaa ya kawaida lakini sio mitaa yahovyo
Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
Ah, hilo tu? Samahani kwanza kuchelewa kukujibu.
Sidhani kama kuna tofauti kubwa sana kati ya bei ya vyakula (staple) Kenya na Tanzania.
Jijini Nairobi
1)vyakula kwenye migawa ya kawaida, tuchukue mifano ya vyakula vinavyotumika huku Kenya sana kama ugali, mchele, chapati, nyama, samaki au maharage...
Tuseme kwa mfano:
Ugali/wali/chapati kwa nyama na sukumawiki ni 120.00
Ugali/ wali/ chapati kwa maharage/ndengu ama peas - 80.00
au hata 100.00
Chips mkavu ni 50- 80.00
Kuku nusu ni 150.00
2)Vinyuaji baridi kama soda (1ltr) ni sh. 99.
Minute maid au Del Monte Juice 1ltr pkt is 180.00.
3)Vileo Kenya bei ni ghali mno, juu ya serikali kuweka kodi ya juu kukabiliana na tabia ya ulevi.
Vodka, mf. Smirnoff 1ltr ni 1300.00
Beer ya Tusker ni 170.00 kwa chupa. Guiness ni 200.00
4)Nyumba za apartments..itategemea na mtaa pamoja na size ya nyumba, ikiwa ni one, two ama three n.k (sisi huku hupima ukubwa wa apt in terms of the no. of bedrooms, not in sq.ft).
One bedroom apt may range from 10.000 (Umoja estate) to 25.000 (Langata).
Erm...hilo halijumuishi malipo ya maji, stima, takataka/usafi na ulinzi.
Rent hulipwa kila mwezi, sio mara moja kwa mwaka kama huko Tanzania.