101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,057
- 2,221
Biashara ya kununua mbegu za Wanaume imeonekana kunoga na kushika kasi katika Kaunti ya Murang’a nchini Kenya ambapo baadhi ya Wanawake wanawalipa Wanaume hadi Ksh. 300,000 (Tsh. mil 5.1) ili wafanye nao mapenzi na kuwapachika mimba.
Wanaume wanaopendelewa zaidi katika biashara hiyo ni walio na umri wa kati ya miaka 20 hadi 40 lakini wawe ambao wanasoma au wamehitimu kozi za masomo ambazo Wanawake hao wanaojimudu kimaisha (Miss Independents ) wanaziona ni za Watu werevu, aidha Wanawake wengi wamesema wanapendelea Wanaume warefu na walio na rangi ya ngozi ya wastani, yaani si weupe sana na si weusi kupindukia.
Kituo cha Televisheni cha NTV Kenya kimeripoti kuwa Mwanamke mmoja mjini humo amekiambia chombo cha habari cha Taifa Leo kwamba siku hizi Wanawake wanaojimudu kimaisha hususani kiuchumi hawataki usumbufu na stress za ndoa na badala yake wamesema “Sisi tunatafuta tu mbegu ili tuzae na kuendeleza kizazi”.
“Licha ya kwamba tunanunua mbegu lakini katika kuzaa tunafuatilia sana bahati ya kuwa na Watoto wenye sura za kupendeza kwa kuzaa na Wanaume wenye muonekano na pia ubongo mzuri wa kuwawezesha Watoto kung’ara na kufaulu masomoni kwa kuzaa na Wanaume werevu, Mtu akitaka kupata mimba anawapa kazi Watu ya kutafutiwa kidume cha mbegu”
#MillardAyo