Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

RESULTS ZINGINE MPYA ZIMETOKA NAKOMPAILI NIZILETE. RAILA AMESONGA MBELE TENA

UHURU KENYATTA ANAHOJIWA HAPO STUDIONI WAKIMUULIZA NI KWANINI KURA ZA KUTOKA KWA KIBAKI AU NGOME ZAKE HAZILETWI NAIROBI? ANASEMA ATI HIO NDIO WASIWASI UMETUMA YEYE KUENDA KUCHUNGUZA ECK HEDKUATA.

RESULTS ZA KWA KINA ALI BADO ZINABISHWA NA NAFUATA HIYO STORI

Asante sana K-T kwa kazi nzuri uliyofanya leo maana website zingine zote zilizidiwa nguvu lakini JF yetu ikapeta na wewe bila kuchoka umetupatia hizi habari.

Ninavyoona mimi Raila atashinda hizi kura hata kama margin ni ndogo.

Good news:

Mawaziri zaidi ya 15 wa Kibaki wamepigwa mweleka

Makamu wa Raisi amepigwa chini

ccm ya kenya AKA kanu nayo imepigwa chini

Watoto wa moi choka mbaya na wajiandae kwenda jela kwa ufisadi

Total man aliyeshiriki kumuua Ouko - Biwott naye choka mbaya

Mzee Nyachae anayevuruga wakisii wasiungane na wenzao wa Nyanza naye amepigwa chini

Musikari Kombo - naye chini


Leo ni siku nzuri ya kusherehekea na sasa hivi naelekea pub ya wakenya hapa nikasherehekee ushindi

BTW - Mtanzania usitafute kununua kitu maana Raila atashinda hata wakijaribu kuiba kura watajikuta wakiweka zake. New year nitakuwa London na nitakutafuta basi........
 
UPDATES HIZI HAPA:

SOURCE: KTN

TIME: 2.05PM

NATIONAL RESULTS: TOTAL VOTES - 14, 308, 909

1. Raila - 3, 679, 854
2. Kibaki - 3, 090, 260
3. Kalonzo - 516, 749


MIKOANI:

1. WESTERN PROVINCE: TOTAL NUMBER OF VOTES: 1, 564, 854 Mill.

a) Raila - 642, 214
b) Kibaki - 312, 564
c) Kalonzo - 6, 905


2. EASTERN PROVINCE: TOTAL NUMBER OF VOTES: 2,388, 765 Mill.

a) Raila - 48, 712
b) Kalonzo - 441, 936
c) Kibaki - 349, 147

3. NORTH EASTERN PROVINCE: TOTAL NUMBER OF VOTES: 315, 664

a) Kibaki - 64, 704
b) Raila - 58,808

4. NYANZA PROVINCE: TOTAL NUMBER OF VOTES: 2, 041, 686 Mill.

a) Raila - 1, 115, 338
b) Kibaki - 14, 750


5. CENTRAL PROVINCE: TOTAL NUMBER OF VOTES: 2,186, 315 Mill.

a) Raila - 27, 396
b) Kibaki - 1, 385,814

6. RIFT VALLEY PROVINCE: TOTAL NUMBER OF VOTES: 3, 358, 285 Mill.

a) Raila - 1, 313, 560
b) Kibaki - 543, 500
c) Kalonzo - 33, 502

7. COAST: TOTAL NUMBER OF VOTES: 1, 178, 319 Mill.

a) Raila - 243, 238
b) Kibaki - 131, 821
c) Kalonzo - 23, 283


8. NAIROBI: TOTAL NUMBER OF VOTES: 1, 275, 021 Mill.

a) Raila - 192, 843
b) Kibaki - 159, 959
c) Kalonzo - 24, 995



MUHIMU: BADO KUNA MAENEO BUNGE 51 HAZIJAINGIA.

____________________
 
K-T,
Hayo ni maeneo Bunge ni ya mikoa gani? Tukijua ni kura za maeneo gani ni rahisi kufanya prediction. Hata hivyo sina uhakika kama turn out ilikuwa 100%. Kama watu watakuwa wamejitahidi sana basi itakuwa ni around 70% ambayo ni sawa na wapiga kura milioni 10, ambayo bado naona ni kura nyingi na hasa kama maeneo Bunge yaliyobaki yako kwenye ngome ya Kibaki.
 
K-T,
Hayo ni maeneo Bunge ni ya mikoa gani? Tukijua ni kura za maeneo gani ni rahisi kufanya prediction. Hata hivyo sina uhakika kama turn out ilikuwa 100%. Kama watu watakuwa wamejitahidi sana basi itakuwa ni around 70% ambayo ni sawa na wapiga kura milioni 10, ambayo bado naona ni kura nyingi na hasa kama maeneo Bunge yaliyobaki yako kwenye ngome ya Kibaki.

MAMBO SI MAZURI SANA HUKU. TUOMBEENI MWENYEZI MUNGU USIKU WA LEO. NGUVU SA SHETANI ZINATAWALA WALIOKUWA WANAENDA KUSHINDWA NA SASA WAMEANZA MICHEZO MICHAFU.

I AM SO SO ANNOYED. NENDA ZANGU KUSIKIZA MAZUNGUMZO YA HUKO MABARABARANI NA MAJIRANI. KUNA THEORY AU STORY TATU ZINASAMBAA KAMA UPEPO MKALI KATI YA WANA ODM HUKU...

THEORY YA KWANZA YASEMA HIVI: KIFUPI UCHAGUZI UMEIBIWA! SITAKI KUFANYA MZAHA ILA PICHA IMEANZA KUJITOKEZA SASA. WAKATI HUU WOTE WAMEKUWA WAKISHIKILIA MABOX ZA KUTOKA MAENEO ZA KIBAKI/SERIKALI ILI MABOX ZA UPINZANI ZIINGIE ZOTE KISHA WAJUE NI KIASI KIPI CHA KURA BANDIA WASINDILIE NDANI. WAKATI WANANCHI WA ODM WANAFURAHIA MATOKEO ZAO ZA CHAPCHAP HAWA MAJAMAA WALIKUWA WANASHIKILIA KURA WAKIWA NA NIA MBAYA SASA IMEDHIHIRIKA AU WATU WANAANZA KUELEWA KWANINI KUFIKIA JIONI YA JANA SAA KUMI NI KURA TU ZA MAENEO BUNGE 50 NA KITU ZILIKUWA ZIMEINGA NYINGI ZIKIWA ZA OPPOSITION!

THEORY YA PILI INASEMA: UCHAGUZI ULIIBWA ASUBUHI NA WANANGOJA TU ITANGAZWE KIBAKI AMEMU OVERTAKE RAILA NA MDA SIO MREFU WAMUAPISHE NA KUKUTANA NA RIOTS ZA WANANCHI NA FORCE/POLISI ETC

THEORY YA TATU: WAKIFANYA HIVYO BASI HUKU OLE WETU.

SIWAFANYIENI MZAHA.........YOU CAN FEEL THE TENSION IN THE AIR....NA KUHARIBU ZAIDI UHURU KENYATTA NA AMOS KIMUNYA ALIYEKUWA WAZIRI WA FINANCE WAMEHOJIWA MUDA MFUPI ULIOPITA NA WANAONEKANA KANA KWAMBA WANAJUA KITU LAKINI HAWASEMI LOTE ILA NUSU NUSU TUU ETI RAIS KIBAKI ASHASHINDA HII KURA NA HAWANA WASIWASI YEYOTE! AMESHINDAJE NA ILHALI KURA HAZIMALIZIKA? WANAJUA NI NINI KINAFANYIKA AU KISHAFANYIKA KWA MABOX YALIYO HUKO CENTRAL PROVINCE NA EASTERN PROVINCE AMBAKO NI NGOME ZAO!
 
K-T Thanks kwa updates but dont giveup

Kwa kweli kazi ipo naamini utulivu utakuwepo na usikate tamaa pambana hadi mwisho.

Inawezekana wanajaribu tu kuweka hali tete ili upinzani waanzishe vurugu wapate kisingizio

Thanks for the update but Dont give up
 
K-T
Kapumzike utulize akili
that is a real Africa , Mimi nahisi kuna kitu tuna miss ama tunazipeleka akili zetu kusiko.

Maana kiongozi lazima akubarike kwa wale anaowangoza nikiwa namaana hata kama unaamini wewe mwenyewe una weza kuongoza lakini unaowaongoza wasikuamini kwanini usikae pembeni umwachie wanayemtaka na kufikiri atawaongoza vyema?? kwanini utake kuwaongoza watu kwa nguvu?? hadi ufikie kuiba kura?? na kutishia amani ya Nchi, sawa yawezekana unataka fedha lakini mbona fedha hawa ma Rais wanazo za kutosha??
Tatizo letu nini kutaka kuongoza watu kwa ma bavu??

Mie jamani nafikia hatua ya kwenda mbali zaidi na kutaka kumukalibia DR WARTOSON wa kuhoji uwezo wetu wa Akili jamani hebu nisaidieni kwa hili.
 
Kenyan-Tanzanian,

Inasikitisha! Nilibashiri toka mwanzo kuwa wangefanya ujanja huo, baada ya kuona wanaanza kutangaza tu matokeo ya maeneo ya upinzani. Huo mchezo CCM iliufanya Tz mwaka 1995, na ninaamini watu wa Kibaki wanazo hizo notes. Lakini kama wakenya mmeshagundua hilo, bado mnayo nafasi ya kuzuia lisitokee, kwa kuhakikisha mnakuwepo kulinda masanduku hayo na kuzuia masanduku ya rigging yasiingizwe. Na hapo mkilala tu, just 20 seconds, ni bao! Inabidi mpeane zamu hata za ku-blink, maana muda huo unatosha kabisa kufanya swapping ya ballot boxes. Na mkishindwa kuwakamata, mtakosa ushahidi, na Kibaki atasemekana ameshinda "kihalali". Yaani hapo ni hakuna kulala, mkifanya hivyo na bado mkashindwa, mjue kweli mmeshindwa. Mkishindwa kulinda kura na matokeo yake mkashindwa uchaguzi, bado mtakuwa mmeshindwa pia! Itawabidi tu mkubali mmeshindwa (it doesn't matter mmeshindwa uchaguzi au mmezidiwa ujanja!).

Kwa hiyo guys don't give up, it's bado too early for that.

Best of luck, nasisitiza MUWE MACHO, mkizubaa kidogo ni shaaaa! Bao la kisigino!
 
Nimeanza kuwa na hofu ya vurugu maana muda unavyozidi kwenda na hawa watu hawatoi matokeo jazba inazidi kupanda na soon or late vurugu itatokea kati ya washabiki wa pande mbili.

Pili wakati wa kutangaza mshindi kama ikitokea tofauti na matarajio ya sasa hata kama hakuna udanganyifu lakini kitendo cha kuchelewesha kutoa matokeo kitaleta vurugu.

Nadhani ni muda muafaka media mbali mbali nchini KQ zingeweka pressure kuanzia sasa ili matokeo yatangazwe mapema ili kuhakikisha hali inakuwa salama.

Naanza kuomba Mungu hayo yasitokee maana Tz wanakazana kufunga makambi yote ya wakaimbizi by June 2008. Tusingependa vurugu itokee Kenya iendelee kwa amani nawatakieni kila la kheri
 
From BBC World:
Kenyan opposition leader Raila Odinga is ahead of President Mwai Kibaki in a hard fought election, according to partial and unofficial results.
In a setback for Mr Kibaki, 16 of his ministers lost their seats.
But correspondents say the president has been closing the gap and most of the remaining votes to be counted are in his heartland.
Despite isolated incidents of violence, international observers have said that the election was mainly well organized.
By 2215 (1915 GMT), the Electoral Commission of Kenya had released results from 69 of 210 constituencies, putting Mr Odinga at 1,691,679 votes and Mr Kibaki at 1,222,725 in the presidential contest, Reuters news agency reported.
Unofficial reports said that 50% of votes had been counted and President Kibaki trailed Mr Odinga and his Orange Democratic Movement (ODM) by about one million votes.
But the BBC's Adam Mynott in Nairobi says the lead has narrowed considerably in the past few hours and there is still a mathematical possibility that President Kibaki could snatch victory.
The ECK head, Samuel Kivuito, has said there were delays in voting and counting, and the process of compiling results was going slowly.

"It is true that the ODM is ahead, but it's only fair to wait until the last ballot is counted before we know the winner of the elections," said Ngari Gituku, a spokesman for Mr Kibaki's Party of National Unity (PNU).
"We are not going to lose hope until the last soldier is shot down and we have no intention of giving up until such a time," he told AFP news agency, adding that his party had evidence of widespread rigging.
Mr Odinga's ODM has in turn accused the electoral commission of deliberately delaying the results, and now says Mr Kibaki should concede.
"Kibaki seems to be going out in a very untidy manner and really is not being respectful or grateful to the democratic process that put him in power," said ODM official Anyang Ngong.
ODM General Secretary Joseph Nyaga said the delay threatened to cause instability and unrest right across the country.
Police Commissioner Hussein Ali has urged poll losers to respect the outcome.
 
Amani iwe nanyi katika kipindi hiki kigumu. Nilidhani uchaguzi huu utaenda kwa amani lakini inaelekea dhana yangu itakuwa sivyo.

Watu wanaweka mbele maslahi yao na kung'ang'ania kuendelea kuwa madarakani bila kufikiria kwamba pale ambapo wananchi wataona uchaguzi haukuwa wa haki basi maafa makubwa yanaweza kutokea.

Kweli siasa ni mchezo mchafu sana. Uchaguzi ulifanyika tangu Dec 27, 2007 na matokeo yaliahidiwa kutolewa siku hiyo hiyo, lakini siku mbili baadaye bado matokeo hayajatangazwa rasmi. Afrika bado tuna safari ndefu sana kuelekea kwenye demokrasi au si ajabu itabaki kuwa ndoto tu, lakini kamwe hatutafika huko.
 
Hii iko kwenye Guardian, inaonekana Mzee Kibaki anasubiri miujiza ya mungu kushinda, na miujiza huwa inatokea.

Kenyan president Mwai Kibaki appeared to be heading for a humiliating election defeat last night as voters signalled their discontent with his government by evicting most of the powerful political old guard from office.
Local television stations reported that, with more than half the votes counted by midnight local time, opposition leader and former political prisoner Raila Odinga had won 3.6m votes, a 51% share, compared with 42% for Kibaki, on 2.9m votes. Odinga's Orange Democratic Movement was also heading for an overwhelming victory over Kibaki's Party of National Unity.
The election commission of Kenya trailed far behind the media in releasing results, although it also showed Odinga comfortably in the lead. Though it was still theoretically possible for Kibaki, 76, to reverse the deficit, analysts said it would take a minor miracle.
If he does not, it will be the first time a Kenyan president has lost through the ballot box, and will represent a clean break from the political dynasty that has governed the country since independence.

It is a remarkable reversal of fortunes for a man who enjoyed huge support when he was elected in 2002, ending 24 years of autocratic rule by Daniel arap Moi. Although Kibaki helped to improve the economy and civil service, his decision to remain loyal to political veterans - many with dubious records, or from his own Kikuyu ethnic group - rather than bring in new blood, has counted against him.

At least 16 of Kibaki's 32-member cabinet members were confirmed to have lost their seats, including his vice-president Moody Awori, 80, and the defence and roads ministers, both in their late 70s. "This was an unprecedented revolt from the ground against the corruption of parliament and against the old political class," said Mutahi Ngunyi, a political scientist in Nairobi. "It's a huge vote of no confidence in the government, and allows a new generation a chance at leadership."

A part of the winning coalition five years ago, Odinga left the government in 2005, angered by Kibaki's failure to honour a power-sharing agreement and his attempt to push through an unpopular constitution. Odinga has been campaigning ever since, accusing Kibaki of failing in his election pledges to end high-level corruption and to create 500,000 jobs a year. Under-40 voters in particular, many of whom remain unemployed, bought into Odinga's message that he was the man to bring about the change they had voted for in 2002.

In an attempt to close the gap, Kibaki, who had already drawn Uhuru Kenyatta, son of Kenya's first president, Jomo Kenyatta, into his party, enlisted the help of the second president, Moi.

It was a damaging misjudgment of the public mood. Even in Moi's traditional stronghold of Rift Valley province his legacy of corruption and misrule overshadowed his supposed elder statesman role, and he was booed at rallies.

Three sons of Moi who stood for parliament lost, including Gideon Moi, in the seat he took over from his father. In August he featured prominently in a leaked report commissioned by the government from the risk consultancy Kroll, which aimed to trace the assets of people suspected of looting state coffers. The other notable MP in the Kroll report, Nicholas Biwott, also lost his seat.

Others voted out included David Mwiraria and Chris Murungaru, who were forced to step down as ministers in 2006 after being accused of complicity in a huge corruption scandal known as Anglo Leasing, which involved bogus companies, some registered in the UK. They are both banned from visiting Britain.

International observers praised the organisation and conduct of the poll, although there was violence at several polling stations during counting yesterday
 
Amani iwe nanyi katika kipindi hiki kigumu. Nilidhani uchaguzi huu utaenda kwa amani lakini inaelekea dhana yangu itakuwa sivyo.

Watu wanaweka mbele maslahi yao na kung'ang'ania kuendelea kuwa madarakani bila kufikiria kwamba pale ambapo wananchi wataona uchaguzi haukuwa wa haki basi maafa makubwa yanaweza kutokea.

Kweli siasa ni mchezo mchafu sana. Uchaguzi ulifanyika tangu Dec 27, 2007 na matokeo yaliahidiwa kutolewa siku hiyo hiyo, lakini siku mbili baadaye bado matokeo hayajatangazwa rasmi. Afrika bado tuna safari ndefu sana kuelekea kwenye demokrasi au si ajabu itabaki kuwa ndoto tu, lakini kamwe hatutafika huko.

Sio Afrika tu, hata huko kwa Bush wanakodai kuna demokrasia, ule uchaguzi uliomwingiza Bush madarakani mwaka 2000 ulikuwa utata mtupu, kulichezwa zengwe jimbo la Florida ambako kaka yake Jeb Bush alikuwa gavana. Wakarudia zoezi la kuhesabu kura, matokeo ya mwisho yakaja wiki mbili baada ya muda uliotarajiwa, tena kwa uungwana tu (au sijui kitu gani kingine) wa Al Gore kukubali kwamba basi waache tu wasiendelee kuhesabu upya kura! Al Gore aliibiwa ushindi ule, na dunia nzima inalielewa hilo.

Ujumbe hapa ni kwamba ufisadi hauna mipaka ya rangi wala kabila, ukiona mwafrika fisadi si sababu ya uafrika wake, bali kwa kuwa ni fisadi. Tusijidhalilishe bure kana kwamba Afrika ni ya mafisadi watupu na wezi wa kura, la hasha, maana huko ni kutowatendea haki wale wasiokuwa na tabia hiyo.

Nawatakia heri wakenya, ni kipindi kigumu sana hiki, lakini wanapaswa pia kutumia busara na kufanya kazi kwa tahadhari kubwa kupambana na ufisadi wa wizi wa kura na/au matokeo yanayoweza kusababishwa na wizi kama huo.
 
Sio Afrika tu, hata huko kwa Bush wanakodai kuna demokrasia, ule uchaguzi uliomwingiza Bush madarakani mwaka 2000 ulikuwa utata mtupu, kulichezwa zengwe jimbo la Florida ambako kaka yake Jeb Bush alikuwa gavana. Wakarudia zoezi la kuhesabu kura, matokeo ya mwisho yakaja wiki mbili baada ya muda uliotarajiwa, tena kwa uungwana tu (au sijui kitu gani kingine) wa Al Gore kukubali kwamba basi waache tu wasiendelee kuhesabu upya kura! Al Gore aliibiwa ushindi ule, na dunia nzima inalielewa hilo.

Ujumbe hapa ni kwamba ufisadi hauna mipaka ya rangi wala kabila, ukiona mwafrika fisadi si sababu ya uafrika wake, bali kwa kuwa ni fisadi. Tusijidhalilishe bure kana kwamba Afrika ni ya mafisadi watupu na wezi wa kura, la hasha, maana huko ni kutowatendea haki wale wasiokuwa na tabia hiyo.

Nawatakia heri wakenya, ni kipindi kigumu sana hiki, lakini wanapaswa pia kutumia busara na kufanya kazi kwa tahadhari kubwa kupambana na ufisadi wa wizi wa kura na/au matokeo yanayoweza kusababishwa na wizi kama huo.

Najua hilo la kuhusiana na uchaguzi wa US mwaka 2000. Hata uchaguzi wa 2004 kulikuwa na namna na huo ujao wa mwaka kesho ujanja unaweza tena kufanyika kama mashine za kupigia kura zikitumika tena. Tofauti na wenzetu kwetu huwa kunakuwa na maafa katika hizi chaguzi za vyama vingi na maafa haya yanaweza kuziingiza nchi zetu katika vita vya muda mrefu.
 
Wengi wavuka mpaka Namanga kutokea Kenya

2007-12-28 08:29:10
Na Novatus Makunga, PST Arusha

Idadi ya watu wanaoingia nchini kupitia mpaka wa Namanga wakitokea nchini Kenya, imeongezeka katika siku tisa zilizopita hali ambayo inahusishwa na uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Hata hivyo, ongezeko hilo linaonekana kuwa ni dogo kutokana na idadi ya watu wanaovuka mpaka kupitia Namanga kutojumuisha watalii ambao wengi wao hivi sasa wamesitisha safari zao kutokana na kuhofia vurugu zinazoweza kutokea kutokana na uchaguzi mkuu wa Kenya.

Afisa uhamiaji mkoani Arusha, Bw. Justin Kabigumira aliiambia PST kwamba kumekuwepo na ongezeko dogo mpakani Namanga, kwa kawaida huwepo wastani wa kuingiza watu 800 kwa siku wakitokea nchini Kenya.

``Kwa siku hizo tisa, kumekuwepo na jumla ya watu waliongia nchini wakitokea Kenya wapatao 7,519 ikiwa ni sawa na wastani wa watu 836 kwa siku ambao ni ziada ya watu 36, lakini ukiondoa idadi ya watalii wanaopitia Kenya ambayo wamepungua sana,`` alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Kabigumira,kati ya tarehe 17 na 26 ya mwezi huu, jumla ya watu 3,046 wenye pasi za kusafiria za Kenya waliingia nchini, wakati Waasia walioingia nchini wakipitia Kenya walikuwa 133 na Wapakistani 8, huku Watanzania waliorejea nchini wakitokea Kenya walikuwa 4,332.

Hata hivyo, mmoja kati ya madereva wa mabasi yanayotoa huduma kati ya Nairobi na Arusha Bw. Charles Okenywa wa kampuni ya Riverside Shuttle, alisema idadi kubwa ya wanaoingia nchini kupitia Namanga inaonekana ni ndogo kutokana na kutokuwepo kwa watalii wapya wanaoingia kupitia Kenya.

Bw.Okenywa alisema kuwa hifadhi za taifa za ukanda wa kaskazini kwa kawaida hupokea watalii wengi wanaopitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wa nchini Kenya kutokana na kuwa na safari nyingi za ndege za kimataifa kuliko ilivyo kwa uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Alisema hivi sasa watalii waliopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini ni wale walioingia kuanzia tarehe 17 ya mwezi huu, wengi wao wakiwa na programu za kupanda Mlima Kilimanjaro na kutembelea mbuga za wanyama za ukanda wa kaskazini ambazo ni pamoja na bonde la Ngorongoro, Ziwa Manyara,Tarangire, Serengeti na Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Aidha uchaguzi huo ambao ulifanyika nchini humo jana, pia umeathiri biashara ya usafirishaji kati ya Arusha na Nairobi ambapo kampuni nyingi kuanzia juzi zimesitisha safari kutokana na kukosa abiria wanaoingia nchini Kenya.

Meneja wa kampuni ya Bobby Shuttle, Bw. Juma Mliyangi alisema kampuni yake imeshindwa kufanya safari kati ya Arusha na Nairobi kutokana na kukosa abiria wa kutosha na kuoanisha hali hiyo na uchaguzi unaendelea nchini humo.

Hali nchini Kenya inategemea kuwa shwari baada ya kutangazwa kwa matokeo na kuapishwa kwa mgombea atakayeibuka na ushindi.
SOURCE: Nipashe
 
Hongera sana wa-Kenya kwa kuamua kufanya mabadiliko ya kweli, tunausubiri kwa hamu ushindi wa Raila Odinga!

Viva ODM!
Aluta Continua!
 
Tofauti ya kura laki tano kati ya odinga na Kibaki ni ndogo sana(Source TvT asubuhi).

Lakini pia kumungoa Rais wa nchi siyo kazi ndogo. Kazi iliyofanyika kwa wabunge ni kubwa sana.

Nina imani tayari mizizi imekatwa bado tu shina kung'oka.

Mwisho shina litangoka
 
Mpaka sasa nikama nguvu sawa, wote wanakaribu kura 3m. Nahuko ni stronghold ya raila, maeneo ya kibaki kura hazijatangazwa! Lakini nikweli Raila atawasaidia wakenya?
 
K-T,
Ninakuona msee, je, kuna mpya zaidi? Hebu tupashe zilizo kwenye ground toka hapo Nai!
 
Source: Internal ODM tallying!

Nachukua fursa hii kuwaeleza kuwa Agwambo Raila Amolo Jaramogi Oginga Odinga ameshinda kiti cha Urais wa Kenya.

Nimetoka kuongea na Prof. Anyang Nyong'o sasa hivi. Yupo katika upbeat mood na tayari Kamati ndogo ya kuunda baraza lipya la Mawaziri imeteuliwa. Kalonzo ameshampigia simu Raila ya kuconcede defeat. Wanasubiri simu ya Kibaki ili watangaze matokeo.

ODM haiwezi kutoa matokeo yake kwa sasa kwa public kwani inaweza kuleta chaos maana wananchi wataingia barabarani. Wanasubiri Tume iamue. Wao tayari wamepokea matokeo ya nchi nzima na wameyahakiki usiku mzima wa jana na wameshinda.

Haya, ngoja mimi sasa nijisomee makabrasha yangu ya madini maana toka jana nilikua nafuatilia hili tu.
 
Back
Top Bottom