Wanaogopa maana wote karibu watavaa viatu alivovaa Kibaka. M7 anamwandaa mtoto wake huku JK akijua yatayomkuta 2010. Sioni kama kuna wa kuongelea hili suala public licha ya ukwelikwamba wao ndio majirani na ndugu wa karibu zaidi kuliko observer/kiongozi yeyote duniani.4. Hivi JK au M7 they can not intervene and do something? What is the role of EAC ktk hali kama hii? Mimi nadhani by sasa M7 na JK wangekuwa wamekutana- na kuona kitu cha kusaidia as a way foward! Inasikitisha Brown PM UK ndo amewapikigia simu Raila na Kibaki- akishawishi wakutane na waongee!
JK yeye yuko Mapumziko- Hotel ya Kitalii Sopper Lodge- anakula maisha- kweli Tanzania tunaye raisi msanii!
KT,
Hivi mpaka sasa idadi kamili ya viti vya ubunge ikoje? Nimesikia ODM wana
viti 100 na ukijumlisha vyama vingine inaonyesha kuna viti vingine bado hawajatangaza.
Mh. Mtanzania,
Hebu check kwenye post yangu ya tarekhes 30-31 Des. Niliattach jedwali lenye maeneo, wabunge na vyama vyao.
Vita vimeondoka mijini kwajili ya uzito wa polisi na kuelekea mashinani huko kwenye vijiji na jamii moja, kama amevyosema mwanahabari wa Nation M. Gaitho, hivi sasa ina face ethnic cleansing just because mtu wa jamii hio amenyakua mamlaka kinyume ya sheria za uchaguzi za nchi yake. Watu wanawachinja si mchezo. Idadi ya serikali ni 180, media wasema 270 ukiniuliza mimi ntakuambia weka hesabu zote hizo pamoja. Jamii hio inahamishwa na makabila mengine ya Kenya ikiambiwa irudi kwa mkoa waliotoka yaan Central ili watawaliwe na rais wao huyo asiyekubalika kwa mikoa 6.
Ripoti zingine zinasambaa kwamba mamia ya watu waliokimbilia huko maeneo ya Eldoret kanisani walifuatwa huko usiku na kuteketezwa moto wakiwa wanasinzia. Kila ncha ya nchi nje ya Nairobi na Central innocent lives za jamii hio zinatolewa kama kafara ya makosa ya kundi isiozidi watu 6 hapo ikulu.
Na kila kuchao ndivyo hii crisis inaendelea kutokota na kuget out of handi. Hebu mtafakari na tujadili haya waheshimiwa:
The count will continue to rise until Raila concedes. No other way.
1. Kibaki akijiuzulu sasa vile tunataka kunauwezekano wa loophole kwenye katiba. Hatuna makamu wa rais au spika wa bunge ambao angeweza chukua mamlaka kwa mda. Hii inamwachia mamlaka mkuu wa majeshi Gen. Kianga au Jaji Mkuu Gicheru.
2. Kwajili jeshi linarekognaisi Commander in Chief (Rais) aliyechaguliwa, basi kujiuzulu kwa Kibaki kutamaanisha lazima Kenya iingie kwa kura tena na kikatiba hii ni baada ya 90days. Basi mauaji na ghasia au utawala wa majeshi utachukua siku 90 ili kupatikane Rais mwengine na jeshi limkabidhi mamlaka.
3. Raila kikatiba itakua vigumu kuchukua mamlaka pindi Kibaki anpojiuzulu kwajili ECK ilimtangaza kashindwa. Na kikatiba dizisheni ya ECK is final and can only be challenged kortini.
4. Kwajili Jaji Mkuu anasemekana kuwa karibu sana na Kibaki ambaye ndiye alimuapointi awe CJ, Upinzani haina imani na yeye na ndio hata jamii ya kimataifa haitaki Raila aende kotini jili hata pata haki. Sasa itakuaje?
5. Independent Kamiti ichunguze madai dhidi ya PNU na Kibaki yanayotokana na wizi wa kura ni fikra zuli. Ila pia lina utata. Kamiti hii ikisema sasa ihesabu tena kura, hatujui kama kwa hizi siku chache PNU au serikali wamezikoroga maboxi kusahihisha marekodi.
Nafungua mjadala na naomba maoni yenu ya dhati: Itakuaje?
1. Kibaki na Raila nadhani ni marafiki- wakutane waongee the way foward na mustakabali wa Kenya!
2. Kama sii woga- wa Kibaki if Katiba Mpya anguikubali - Raila angeweza kuwa Waziri Mkuu- may be haya ya leo yasingetokea!
3. Naskia foreign observers (Commonwealth, AU) wanapendekeza Independent Commitee to view the tallying of votes! Observaers wa EAC wako wapi????? Where is EAC?
4. Hivi JK au M7 they can not intervene and do something? What is the role of EAC ktk hali kama hii? Mimi nadhani by sasa M7 na JK wangekuwa wamekutana- na kuona kitu cha kusaidia as a way foward! Inasikitisha Brown PM UK ndo amewapikigia simu Raila na Kibaki- akishawishi wakutane na waongee!
JK yeye yuko Mapumziko- Hotel ya Kitalii Sopper Lodge- anakula maisha- kweli Tanzania tunaye raisi msanii!
Asante K-T,
Kwa kuanzia tu ingawa nitakuja baadaye kwenye hili. Pressure iwe kumtoa Kibaki kwanza, the rest will come. Kuna watu wanasema kuwa jeshi lina wakikuyu wengi lakini experience yangu ya kusafiri kati Namanga na Busia inaonyesha kuwa check points nyingi zilikuwa na polisi ambao ni wakalenjin.
Hivi composition ya polisi na jeshi ikoje?
K-T, option 2 sounds better ili kuondoa 'doubts' ingine kama hiyo ya kuweka nchi chini ya CJ ambaye tayari watu hawana imani naye. Kama alivyosema Mwafrika, presure sasa iwe kumwondoa Kibaka hapo kwa state house, then within hizo siku 90 ambazo nchi itakuwa chini ya Jeshi basi iundwe EC ambayo all Kenyans watakuwa na imani nayo. Pia ktk hizo 90 days mtaweza kusettle issue nyingine kama kufikiria njia nzuri ya kutangaza matokeo toka mashinani.2. Kwajili jeshi linarekognaisi Commander in Chief (Rais) aliyechaguliwa, basi kujiuzulu kwa Kibaki kutamaanisha lazima Kenya iingie kwa kura tena na kikatiba hii ni baada ya 90days. Basi mauaji na ghasia au utawala wa majeshi utachukua siku 90 ili kupatikane Rais mwengine na jeshi limkabidhi mamlaka.
1. Kibaki na Raila nadhani ni marafiki- wakutane waongee the way foward na mustakabali wa Kenya!
2. Kama sii woga- wa Kibaki if Katiba Mpya anguikubali - Raila angeweza kuwa Waziri Mkuu- may be haya ya leo yasingetokea!
3. Naskia foreign observers (Commonwealth, AU) wanapendekeza Independent Commitee to view the tallying of votes! Observaers wa EAC wako wapi????? Where is EAC?
4. Hivi JK au M7 they can not intervene and do something? What is the role of EAC ktk hali kama hii? Mimi nadhani by sasa M7 na JK wangekuwa wamekutana- na kuona kitu cha kusaidia as a way foward! Inasikitisha Brown PM UK ndo amewapikigia simu Raila na Kibaki- akishawishi wakutane na waongee!
JK yeye yuko Mapumziko- Hotel ya Kitalii Sopper Lodge- anakula maisha- kweli Tanzania tunaye raisi msanii!
Nimesikia NPR muda mfupi uliopita kuwa Mzee Kibaki yuko under both internal and external pressure kutatua mgogoro huo. Sijui atautaua vipi wakati ni yeye aliyeuleta kwa makusudi ili ajichukulie madaraka kwa nguvu.
Anatimiza kile alichoapa kufanya ... uhalifu! Lakini nina uhakika hayo machafuko yatamfanya awe unpopular hata kwa wakikuyu wenzake ambao watapoteza ndugu kwenye hayo mapigano. Niliongea na mmasai mmoja akaniambia kwamba kinachoendelea huko ni vita kati ya makabila mengine vs wakikuyu. Ndiyo maana wakikuyu ambao wako nje ya Nairobi na Central wako kwenye risk ya kumalizwa kwa kuuawa kinyama. Kama watu wanachomwa kanisani, sioni tofauti na mauaji ya Rwanda!
...it's true Mwafrika, Mashada kumebadilika sana, heshima imeanza kurudi miongoni mwa members wa ile forum. Before kuna watu walionekana kama aliens, sure, as if not normal human being.kama ulikuwa unafuatilia ile forum inayomilikiwa na wakikuyu ya mashada (nimesema hili kwa sababu ile forum inadelete sana anti kibaki post na hata members wanaojitambulisha kama ODM wanakuwa banned every now and then) imebadilika sana tone.
Siku mbili za kwanza wakikuyu walikuwa wanatoa kashfa sana zidi ya wenzao lakini kadri muda unavyokwenda wengi wameanza kuacha maana wamegundua kuwa kabila lao ambalo limeenea kenya nzima linaweza kupunguzwa in half kama wakiendelea upuuzi huu - onyo kwa watu wasiopenda kusoma matusi usiende mashada kwa sababu kule hakuna ustaarabu wa JF na watu wanatukanana live.
The Kenyans living in London are invited for a peaceful demonstration outside the Kenyan Embassy in London on the 3rd of January from 11am. This is to show solidarity with our brothers and sisters in Kenya. For all those who feel the need to give back leadership to the people, come to London.
Come on come all
Kwa wale tulio karibu turekebishe ratiba zetu twende kuwaunga mkono wenzetu. Let us embrace peace across EAC kwa vitendo, lisiwe la kuwahaachia Wakenya then kesho tujinafiki kusaidia wakimbizi.There are parallel peaceful rallies in Washington and New York on the same day.Leadership should go back to the people.
Mhe KT,
i) Nafikiri jambo la kwanza ni kujaribu kuepuka kulifanya hili jambo kuwa ni vita kati ya Wakikuyu na makabila mengine. Hii itaharibu dhana nzima ya uporaji wa urais kulikofanywa na akina Kibaki. Naamini kuna wakikuyu wengi ambao hawajapendezwa na kilichotokea. Kama mwelekeo utaendelea kuwa wa kikabila tutawapoteza katika line yetu ya mapambano wapambaji wenzetu kama akina Nyaga ambao ni wakikuyu.
ii) Option ya maana sana kwa sasa ni international community na viongozi wa kiafrika (AU) kumsuta Kibaki na kumshinikiza kukaa pembeni wakati hii mess ikiwa sorted out. Pamoja na kwamba hamna imani na Jaji Mkuu wa sasa, kama ndivyo katiba inavyosema itabidi ashike mamlaka kwa muda kama Kibaki ata-bow to pressure maana sio sawa kuwa na vacuumu kwenye uongozi na sidhani kama ni mwafaka sana kuwaachia wanajeshi. Wasiwasi wangu ni kwamba wanajeshi wakishika usukani sasa haitakuwa rahisi kuachia pindi watakapoonja tamu ya state house na huko mbele watajigeuza kuwa civilian leaders na kugombea uongozi na tutatengeneza M7 mwingine.
iii) Vipi ile option ya kutumia bunge: to move a vote of no confidence as soon as the bunge sits in its first session?
iv) in the event that all diplomatic means are exhausted to futility, the Ukraine style becomes inevitable. The problem is that this style is likely to be diluted if the struggle will continue to take the shape of tribal fighting as it seems to be suggestive from the recent events!