Mkuu Kiltime:
Yaani wewe bado unataka watu wameze maneno kuhusu huu wizi wa urais huko Kenya? Kama diplomatic missions wenyewe wanasema Kibaki kaiba urais unataka CHADEMA watumie maneno gani? Kumbe wewe bado unakubaliana na falsafa ya kuwa neutral? Hujui kuwa neutrality ni adui mkubwa wa conscience na ni silaha ya binadamu wote waoga na wazembe wa kutafakari? Halafu unadiriki kweli kukubaliana na Kibaki kwamba hili ni tatizo la ndani ya Kenya, na wewe unakubali kweli? Ina maana wewe huna kabisa kamshipa ka-pan africanism? Na kwa nini unakubaliana na Kibaki (serikali) na hutaki kuwasikiliza wengine wanaongea au nawe unaamini kwamba ni serikali pekee inayohodhi ukweli?
Nimejaribu kukutafutia article iliyopo kwenye The Economics ya leo naona nimeshindwa kui-access online; nakushauri sana popote ulipo utafuta nakala ya The Economics ya leo: soma uk 9 na 45 utaelimika sana kuhusu kilichotokea Kenya na naamini baada ya kusoma hizo article unaweza kubadilisha kidogo mtazamo wako.
Kitila Mkumbo,
Heshima mbele!
Mimi (Kilitime) nimechukizwa sana na Kibaki alichofanya na wewe Kitila the same na wengine wengi! na Huenda na Kikwete, huenda na Mbowe, huenda na Lipumba!!! okay no problem.
Tanzania kama taifa huenda haikufurahishwa pia, lakini Tanzania kama taifa haiwezi kusema Kibaki toka! ila yaweza kusema kaeni muyamalize Kibaki na Raila muyamalize!!! na hili ndilo UK/USA wameendelea kulisema, hawajasema Kibaki toka!!! NO!!!... kwa maana nyingine kama taasisi mbali mbali hii ndio inakua misimamo!!! lakini individual hakuna shaka mkuu!!!
Nawatakia maandamano mema!!! lakini kumbukeni hawa ni majirani na kumbukeni narudia tena tofauti ni kati ya Wananchi wa Kenya, Kibaki ni Mwananchi wa Kenya na Raila ni Mwananchi wa Kenya, ODM ni chama cha Kenya, na PNU ni chama cha Kenya. Hata kama source ni Uchaguzi au Ukabila au namna yoyote ile. Let them deal with it first!!!
Kabla pili pili ya shamba haijawawasha!!!
Kama ingekuwa Kenya na Ethiopia,,, well tungekuwa na nguvu zaidi ya sisi kusimama kama chama na kama Taifa kusema lolote kwa urahisi zaidi!
Zimbabwe tuko nao, sio kwa kusema Shangarai ni Mbaya au Mugabe ni Mzuri,,, ni kwa kusema Uingereza acheni/mpeni basi nafasi Mugabe afanyie kazi mambo ya Ndani ya nchi yake!!! Nadhani huo ndio msimamo wa Tanzania.
Hiyo article nitafutie niendelee kujielimisha lakini itakuwa imeandikwa na binadamu kama wewe na mimi sio malaika!!! anaweza lalia upande wowote!!!
Ndio maana nawapongeza sana viongozi wa dini kuombea amani, sio kuombe Raila au Kibaki adumu Madarakani?
Swali:
Ukishajibu Maraisi wa Maswali haya matatu utajua kwanini nimesema hivyo!!! regardless walichukua je madaraka!!! hata M7 awamu yake ya Kwanza haikuwa kachaguliwa but he was the president of republic of Uganda.
Raisi wa Jamhuri ya Kenya ni nani?______________________
Raisi wa Visiwa vya Zanzibar ni nani?___________________
Raisi wa Jamhuri ya Zimbabwe ni nani?__________________
Hawa wote walikuwa na issues lakini kuna marais wao ambao wako madarakani mpaka sasa pamoja na issues zinazoendelea sasa za miafaka na kadhalika!!!