Inavyoonekana ni kuwa kura ambazo zimethibitishwa (6.5 mil) ni 46% ya kura zilizopigwa. Ingawa Raila anaongoza kwa very clear margin, si rahisi kupredict mshindi bado kwa kutumia taarifa hizi pekee kwani kura zilizobaki ni nyingi zaidi. Labda walioko huko Kenya au wengine wenye taarifa watujulishe, hizo kura ambazo bado kuthibitishwa ni za watu wa maeneo gani, na odds zikoje za support ya Kibaki na Odinga huko. Tutajie bado eneo A, B, C, D, na ni stronghold ya Kibaki au Odinga , itasaidia kutafsiri hii trend vizuri.
Hili jambo la mchuano mkali tulijifunza kidogo Tz mwaka 1995. Tume ilianza kutoa matokeo zile sehemu zilizokuwa na nguvu zaidi ya upinzani wakati huo, Kilimanjaro, Pemba, Mara, Kigoma, Arusha, na Iringa, basi tukajua CCM ndio basi tena "tumeshawatema". Kumbe bwana! Walipoona hata Dar nayo pia wanaipoteza, wakavuruga matokeo na kutangaza marudio ya uchaguzi Dar. Kisha wakaanza kutoa matokeo ya sehemu nyingine, ikawa "goli juu ya goli", wakakomba viti vyote vilivyobaki (isipokuwa kimoja tu cha Dar)! Na huo ndio uchaguzi pekee ambako vyama vya upinzani kweli viliitingisha CCM bara, baada ya hapo wakawageuza kuwa kejeli!
Pongezi za pekee kwa mshkaji wangu "Ridikyulasi", ila kwa namna fulani amemuweka pabaya mwenzie wa Tz, "Masanja Mkandamizaji", kwani sasa wataanza "kumwangalia kwa makini"!
Tupeni basi odds za maeneo yaliobaki, nani mwenye nafasi ya ushindi au support kubwa?