Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Kukataliwa kwa 'agreement' hiyo, pamoja na mambo mengine anayoyafanya Kibaki na wenzie ni dalili tosha kuwa wamedhamiria liwalo na liwe; hawawezi kuondoka madarakani.
 
Labda kuna kitu sijaelewa kuhusu suala la Kibaki, mpaka sasa dunia nzima ukiondoa Uganda hawamtambui Kibaki.

Lakini ukiangalia habari zote za magazeti, Redio, television wanasema Rais wa Kenya Mwai Kibaki.

Je wanahabari wameamua kumtambua Kibaki kivyao vyao?
 
Labda kuna kitu sijaelewa kuhusu suala la Kibaki, mpaka sasa dunia nzima ukiondoa Uganda hawamtambui Kibaki.

Lakini ukiangalia habari zote za magazeti, Redio, television wanasema Rais wa Kenya Mwai Kibaki.

Je wanahabari wameamua kumtambua Kibaki kivyao vyao?

Nimesikia kwenye taarifa ya habari ya saa moja redio tanzania kuwa Morocco, Swaziland na Kuwait wamemtumia salam za pongezi kibaki.
 
297826201.jpg

Wanadai ni picha ya wakikuyu wakikimbia machafuko huko Rift Valley

297826199.jpg
 
The struggle continues,no matter what there is still a need to fight.Watu wa East Africa na wapenda Demokrasia inatosimamia haki,maadili ana uaminifu hatupaswi kukubali mambo yaishe kiholela.Raila hakugombea uwaziri mkuu bali urais,kwa maoni yangu kama mtu ninayyeamini ameibiwa kurana wapumbavu wasiojua hata kujiandaa na wanaume waoga sana na kwa mapenzi yangu na demokrasia ninashauri twende mbele ya sheria,movement ziendelee kwa sana,na wana ODM wawe wamoja.Itatuumiza sana kuona Raila amekubali kitu kisicho cha hadhi yake au amekubali kushindwa kirahisi.International community ichukue hatua haraka sana si kuja kupoteza muda kumshauri Raila akubali serikali ya jambazi zee.Keep the pirit high,we want changes with Raila not Kibaki.
 
..tujiandae kupokea ofisi kadhaa za UN nchini.

..politics na economics za east africa zinajipanga upya!inabidi tuwe tayari kwa kazi zaidi.

Na bandari zetu zinazoshindwa kufanya kazi? Tanzania sio wepesi wa kuchangamkia opportunity.

Hivi tumeshindwa kuwa na bandari zenye ufanisi pamoja na kwamba tuna bahari toka Tanga mpaka Mtwara?
 
Kenya election protests to resume

Kenya's main opposition party will resume mass protests after last month's disputed elections, its spokesman says.
The announcement follows the failure of efforts to mediate in the crisis by Ghana's President John Kufuor, who is the African Union chairman.

He has left Kenya, unable to persuade opposition leader Raila Odinga to meet President Mwai Kibaki.

Violent protests over alleged election fraud have left some 600 people dead across the country.

A spokesman for the opposition Orange Democratic Movement (ODM), Salim Lone, said further details would be announced later.

The ODM called off a planned rally on Tuesday, saying it would give international mediation efforts a chance to succeed.

Top US Africa official Jendayi Frazer and four former African presidents have been in Kenya trying to end the crisis in what has been seen as a relative beacon of stability in East Africa.
 
Is it GENOCIDE yet?
Like many opportunists, am waiting to write a book on Kenya massacres...am thinking of the title 'Kenyan Massacres: Lessons Hard learned' or 'The Great Lakes Blood Still Haunting; who's Next?' perhaps Tz is next, who knows... you can suggest other titles...
 
Kuna sehemu nimesoma kwamba kumpata speaker mpaka two third ya wabunge wakubali. Kama ni kweli, speaker atapatikana kweli?

Naomba mnaojua juu ya hili tuelemisheni. Maana sasa ni kuangalia options mbalimbali za kumwondoa Kibaki.
 
ninaweza kuwa kidogo na mada ila tu ni kutaka kujua.

hivi JK alituma majeshi kwenye mpaka ili kuzuia wakimbizi wasiingie tanzania? ninadhani hapana na ninaona kafanya vema.

pili sisi tuliokuwa tunapigwa vita na wakenya, raisi wetu kakubali kuitanbua serikali ya kupumbavu ya mwaikibaki? ninadhani hapana.

sasa wakenya wajue kuwa sisi hatuwachukii na tunawapenda tofauti na dhana iliyokuwa imejengeka hapo awali. your friend in need is your friend in deed.

tusingekuwa watu wa kutafakari na misimamo, tungelegalize serikali hii kwa haraka tofauti na maoni yenu.

M7 ameonekana mtu asiye na msimamo na hapo inabidi wakati mwingine mchuje upuuzi unaowezatokea siku katika kuandaa fideration mtakapoamua ninyi kufuatana na M7 na kusema kile kinachosemwa tanzania ni waoga. hata sasa atakuwa anasema JK ni mwoga.
 
Kuna sehemu nimesoma kwamba kumpata speaker mpaka two third ya wabunge wakubali. Kama ni kweli, speaker atapatikana kweli?

Naomba mnaojua juu ya hili tuelemisheni. Maana sasa ni kuangalia options mbalimbali za kumwondoa Kibaki.

Kuna mchangiaji mmoja alisema kwamba, sheria inataka 2/3, kama asipopatikana ndani ya round mbili za mwanzo then round ya tatu wanatumia simple majority. Sina hakika sana juu ya hilo, maana nilisoma kwenye thread hii.

Lakini swali ni kwamba, je, ODM wana number ya simple majority?

Bunge lina viti 122, hapa kuna seat moja haijapata mtu. So the number will be 121. Je, ODM na NARC wana viti 111?
 
Kuna mchangiaji mmoja alisema kwamba, sheria inataka 2/3, kama asipopatikana ndani ya round mbili za mwanzo then round ya tatu wanatumia simple majority. Sina hakika sana juu ya hilo, maana nilisoma kwenye thread hii.

Lakini swali ni kwamba, je, ODM wana number ya simple majority?

Bunge lina viti 122, hapa kuna seat moja haijapata mtu. So the number will be 121. Je, ODM na NARC wana viti 111?

Nafikiri kwa sasa wabunge ni 207 maama majimbo matatu yaliahirishwa kwenye ubunge. Kwenye urais ndio jimbo moja lilifutwa.

Kama hao 12 hawatateuliwa mapema basi ODM wana viti 102. Wana kosa viti viwili, naona wanaweza kuvipata kama watacheza karata zao vizuri.

Kwa ilipofikia wawe tayari kuachia nafasi ya umakamu speaker na kuvipa vyama vidogo ili kuwa na idadi kubwa ya wabunge bungeni na kuweza kukabiliana na Kibaki. Pia inabidi watumie uwingi wao kuweza kuvishawishi
vyama vidogo kwa kuvipa nafasi kwenye kamati mbalimbali na boards.

Naona tutakuwa na safari ndefu kweli hapa.
 
Kuna mchangiaji mmoja alisema kwamba, sheria inataka 2/3, kama asipopatikana ndani ya round mbili za mwanzo then round ya tatu wanatumia simple majority. Sina hakika sana juu ya hilo, maana nilisoma kwenye thread hii.

Lakini swali ni kwamba, je, ODM wana number ya simple majority?

Bunge lina viti 122, hapa kuna seat moja haijapata mtu. So the number will be 121. Je, ODM na NARC wana viti 111?

Yeah ni kweli,

Ni kweli kuwa Uchaguzi wa spika unafanyika kwa round tatu (kama ni lazima) ambapo round mbili za kwanza lazima spika apate 2/3 ya kura na ikishindikana basi round tatu wanatumia simple majority.

So far mambo hayaonekani mazuri kwa ODM. Ingawa watateua wabunge sita (hii imethibitishwa) bado watakuwa wamefikisha wabunge 108 au zaidi sana wanaweza kupata wabunge 110. Ukichukulia kuwa kutakuwa na wabunge 122 ( ukitoa 3 unabaki na 119) bado jamaa wanaweza kukosa hata hiyo simple majority kama vyama vingine vyote vitamuunga Kibaki.

Kumbuka kuwa vyama kama Safina, Ford Kenya, New Ford Kenya, Narc Kenya, Ford People (if any), bado vina alliance kwa Kibaki. Kwa sasa tegemeo la ODM ni wabunge binafsi (kama yule aliyemshinda Nyachae - Kisii) na wengineo wachache. Kama watano miongoni mwao wakimuunga mkono ODM basi mambo yatakuwa mazuri but so far ni kazi kweli labda kama K-T ana inside information ambazo sina.

Inaumiza lakini huko ndiko tunakoelekea. Kwa sasa kuna uwezekano mkubwa aliyekuwa spika akarudi tena katika hili bunge.
 
Chama kikuu cha upinzani nchini Kenya- ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kimesema kitaendelea kuitisha maandamano ya umma kama hatua ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita.
Bwana Odinga aewaambia Polisi nchini kenya kwamba atafanya mkutano wa hadhara jumaatano wiki ijayo katika uwanja wa Uhuru Park mjini Nairobi.

Hatua hiyo inafuatia kushindwa kwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika rais John Kuffor wa Ghana katika kuwapatanisha Rais Kibaki na Bwana Odinga, ambaye anadai kwamba kulikuwa na wizi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, na kwamba yeye ndiye aliyeibuka mshindi.

Ghasia nchini Kenya zilianza punde baada ya matokoe ya uchaguzi mkuu wa urais kutangazwa , ambapo rais Kibaki alitangazwa mshindi.

Kumekuwa na utata kuhusu matokeo hayo, na Raila Odinga Odinga anasisitiza kwamba yeye ndiye aliyeshinda kwenye uchaguzi huo .

Zaidi ya watu mia sita wameshakufa kutokana machafuko na ghasia za kikabila zilizochochewa kisiasa punde baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa .

Maelfu ya watu wamelazimika kuyaacha makaazi yao maeneo mbali mbali ya nchi kutokana na ghasia.

Serikali ya Kenya imelaani hatua hiyo ya chama cha ODM ya kuitisha maandamano tena .

Waziri wa serikali za wilaya Uhuru Kenyatta ameambia waandishi wa habari kwamba mazungumzo hayawezi kufanyika barabarani.

Amesema viongozi wa ODM wanapaswa kukumbuka kwamba mazungumzo yanawezekana tu watu wakiketi pamoja, na sio kwa kuharibu mali na kuuwa watu.

Kabla ya kuondoka nchini kenya, rais Kuffor alisema katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Koffi Annan ataongoza ujumbe wa watu mashuhuri barani Afrika kwenda kuwapatanisha serikali na upinzani , ili kumaliza mgogoro wa kisiasa uliopo.

Bwana Annan anatazamiwa kwenda Kenya wiki ijayo.
 
mhenwa tabia yetu hurefer kwenye source juu ya habari tunazoziandika

ungesema ni bbc swahili ungekuwa muungwana sana

samahani kama nitakuwa nimekukosea
 
Kati mkuu wa zamani bwana Kofi Annan kuongoza juhudi za upatanisho

Upinzani nchini Kenya umeapa kufanya tena maandamano makubwa kufuatia kushindwa kwa juhudi za kuumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anaziunga mkono juhudi za katibu mkuu wa umoja huo aliyestaafu, bwana Kofi Annan, kujaribu kuutanzua mgogoro wa kisiasa nchini Kenya uliosababishwa na matokeo ya uchaguzi. Marekani na Uingereza nazo pia zimekukaribisha kuteuliwa kwa bwana Kofi Annan kuongoza juhudi za upatanisho.

Msemaji wa chama kikuu cha upinzani nchini Kenya Orange Democratic Movement, ODM, Salim Lone, amesema imedhirika wazi kwamba serikali haina haja ya kuutanzua mgogoro wla kisiasa nchini Kenya. Kwa hiyo maandamano ambayo yalikuwa yamesitishwa yataanza tena kote nchini. Tangazo hilo linafuatia kuteuliwa kwa Kofi Annan kuendeleza juhudi za upatanisho nchini humo.

Marie Okabe, msemaji wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kiongozi huyo alizungumza kwa simu na bwana Kofi Annan na kumwambia anamuunga mkono kwa dhati katika kazi yake mpya ya kuzipatisha pande zinazohasimiana nchini Kenya.

Akijibu maswali kuhusu jukumu la Umoja wa Mataifa wakati wa uchaguzi nchini Kenya, msemaji wa katibu mkuu wa umoja huo, Michele Montas, amesema umoja huo haukuwa na waangalizi wake katika uchaguzi huo wala wakati wa kuhesabiwa kwa kura. Kwa hiyo umoja wa Mataifa hauwezi kujiingiza sana katika swala ambalo haukuhusika na hauna ukweli kamili.

Rais wa Ghana John Kufuor aliyendoka jana mjini Nairobi kurejea Accra, baada ya juhudi za Umoja wa Afrika kutaka kuutanzua mzozo wa kisiasa nchini Kenya kukwama, amesema rais Mwai Kibaki wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, walikubaliana jana kushirikiana na jopo litakaloongozwa na bwana Kofi Annan kuumaliza mzozo ambao umesababisha vifo vya mamia ya watu.

O-ton Kufuor

´Jambo la kutia moyo ni kwamba pande zote mbili zimekubaliana kwamba machafuko yakomeshwe na zinapinga machafuko. Na pia zimekubaliana kuwepo na mazungumzo yatakayoongozwa na jopo la Waafrika mashuhuri.´

Akizungumzia kuhusu swala la demokrasia nchini Kenya rai John Kufuor amesema

´Kila mtu anazungumzia demokraisia. Demokrasia inataka hata kama hamjakubaliana, mkubaliane kwamba hamjakubaliana. Lakini sio kufyatuliana risasi, kuua na kuharibu mali.´

Katibu mkuu wa chama cha ODM, profesa Anyang Nyong´o anamlaumu rais Kibaki kwa kuzikwamisha juhudi za rais Kufuor kuumaliza mzozo wa kisiasa nchini Kenya.

O-ton Anyang

´Chama cha ODM hakina wasiwasi kuhusu wakati. Ni Kibaki ndiye anayeishiwa na muda. Chama cha ODM hakisababishi hali ya wasiwasi miongoni mwa Wakenya, ni Kibaki ndiye anayefanya hivyo. Kuna mtu mmoja katika ikulu ambaye hataki nchi hii isonge mbele kwa sababu anataka madaraka.´

Marekani pia imekukaribisha kuteuliwa kwa bwana Kofi Annan kuendeleza juhudi za upatanisho nchini Kenya. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani Tom Casey, amesema Marekani inapongeza juhudi za Umoja wa Afrika kusaidia kujaribu kutafuta suluhisho la tofauti za kisiasa kati ya vyama na watu binafsi nchini Kenya. Aidha bwana Casey amesema uteuzi wa bwana Annan ni sehemu ya juhudi za pamoja zinazofanywa na jumuiya ya kimataifa kujaribu tena kutafuta suluhisho la kisiasa.

Mjumbe maalumu wa Marekani, Jendayi Frazer, ambaye bado yumo mjini Nairobi, anatarajiwa kurejea nyumbani hivi karibuni. Hata hivyo Tom Casey amesema kurejea kwake hakupaswi kuonekana kana kwamba Marekani haina nia ya kusaidia kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa kisiasa nchini Kenya.

Kiongozi huyo amesema Marekani itaendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika na makundi mengine kuhakikisha makubaliano yanafikiwa kati ya vyama vya kisiasa. Marekani imetoa dola milioni tano kusaidia Wakenya walioathirika na waliolazimika kuyahama makazi yao kufuatia machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi. Fedha hizo zitatolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kimataifa kusadia katika maswala ya afya pamoja na chakula, maji, usafi na mahema.

Uingereza nayo pia inaunga mkono uteuzi wa bwana Kofi Annan kusaidia kuzipatanisha pande zinazozozana nchini Kenya. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, David Miliband, amesisitiza haja ya kuchunguza madai ya wizi wa kura na kuwatolea mwito viongozi wa Kenya washiriki kikamilifu katika mchakato wa mariadhiano bila masharti na wakubaliane vipi watakavyogawa madaraka serikalini.
 
David Miliband, amesisitiza haja ya kuchunguza madai ya wizi wa kura na kuwatolea mwito viongozi wa Kenya washiriki kikamilifu katika mchakato wa mariadhiano bila masharti na wakubaliane vipi watakavyogawa madaraka serikalini.

Huyu naye anajibu swali ambalo hajaulizwa. Kabla ya mambo ya kugawana madaraka cha kwanza kabisa ni kujua ni nani alikuwa mshindi wa kweli wa kti cha urais.
 
Nasikia kesho maandamano ya kumpinga Kibaki ni Ruksa tanzania, Ususani pale Bongo. Je Lunyungu una taharifa hii?

Je haya maandamano yanaweza kumunyima usingizi Kibaki ambaye hata wakenya wenye uwezo wa kuandamana mpaka mlangoni mwake ameona hawana maana?
 
Back
Top Bottom