Kenya exports to Tanzania hit ten-year low

Sijakataa kuongelea sababu, na ndio kiini cha hoja hii. Na kwenye masuala kama haya sababu lazima zitakuwa ni nyingi, katu haiwezi kuwa moja.

Nilichosema kuwa siwezi kufanya ni kuleta data za tz, wewe unaweza kuzileta lakini mimi uzi wangu haulengi huko.
 
Yeah wapo ila ni ya Kenyata Family iko kule ili mtu akimkataa Kenya basi analetewa bidhaa ile ile toka Uganda
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Such a clever guy!
 
Swali la msingi hapa la kujiuliza, ni je supply ya bidhaa nchini imepungua na hivyo kupelekea demand kuwa kubwa then bei zimependa? Kama sivyo, basi kuna kitu kimelikidhi hilo soko.

Ni hali ya kawaida tu, lazima ingetokea tu hata iweje. Simiyu haitumii tena maziwa toka nje, Meatu imereplace, chaki nknk
 
Nchi ya viwonder si mtuletee data za exports kuelekea KENYA.
 
Hivi hii ban iliwekwa na Tanzania tuu, au Kenya na wao waliweka ban kwenye bidhaa za Tanzania ? Na nani hasa alianza na huu mchezo wa ban kama sio Kenya? tokea tour van, unga wa ngano mpaka cooking gas. List ni ndefu.
 
Hivi hii ban iliwekwa na Tanzania tuu, au Kenya na wao waliweka ban kwenye bidhaa za Tanzania ? Na nani hasa alianza na huu mchezo wa ban kama sio Kenya? tokea tour van, unga wa ngano mpaka cooking gas. List ni ndefu.
Tanzania ndo ilianza ban tokea enzi za ujamaa policies, hivi we haujui tour van za Kenya zilibaniwa kuingia Tz tangu 1980's??? Kenya imekua ikiruhusu tour van za Tz kuingia kenya miaka hio yote bila kuwakazia, eti list ni ndefu hebu toa hio list tuione...

Enda kwa EAC upewe list official na uangalie ni nchi gani ndani ya EAC inazuilia zaidi biashara na exports za wenzake
 
Labda hujuwi na ndio maana mnachangaya mambo, ban ya tour van za Kenya ni kuingia kwenye mbuga za wanyama za Tanzania tuu sio kuingia nchini Tanzania. Hivyo ni vitu viwili tofauti na kama ban ingekuwepo, mabasi ya abiria ya Kenya yasingeigia Tanzania yakiwa na abiria, wengine humo ni watalii. Nyinyi mli ban van za Tanzania kuingia JKIA swali ambalo mnashidwa kulijibu mpaka leo hii, Is an airport a tourist attraction??

Usidanganye watu eti Tanzania ndio ina ban vitu vya Kenya. Mpaka 2010, Kenya ilikuwa inaingiza bidhaa nyingi Tanzania na Uganda kuliko inavyo nunuwa kutoka nchi hizo, Tanzania na Uganda walipo amza to build their own capacity, Kenya ikakimbikia ku ban bidhaa za Tanzania na Uganda. Kuanzia Kuku wa Uganda mpaka, tyres za Tanzania eti ziko below standard. Mimi nilishasema humu JF, Wakenya mna weka ban mpaka mtakuja kuji-ban wenyewe, haya sasa, ushahidi huo hapo, sales are taking nosedive.
 
Wacha kuchezea maneno wewe...Kuna umuhimu ghani wa kuruhusu tour van ya kenya kuingia Tz kama hautairuhusu kuingia mbugani? Hata mimi naeza kujibu kama ulivyonijibu, ban ya tour van za Tz si ban ya kuingia Kenya bali ni ban ya kuingia jkia tu!
Mlituban kuingia mbugani na sisi tukaban pale mtaumia manake tulijua tour van za tz haziwezi kutishia Kenya tukiendelea kuziruhusu kuingia mbuga za kenya.

Inajulikana EAC nzima kua Tz ndo inaongoza kwa non tariff barriers kwa majirani wake.
BTW, exports za Kenya to Uganda ni $600m, to south sudan ni $300m, hata mkiban kila kitu Kenya bado itapata market mpya ya kuuza bidhaa zake
 
Haha, unaona eh, unafanya makosa yale yale viongozi wenu wamukuwa wanafanya. Ban ya mbuga za wanyama iko nchi zote mbili tena walikubaliana kufanya hivyo kulinda local jobs. Lakini wewe pamoja na viongozi wenu mnashidwa kueleza kama uwanja wa ndege ni kivutio cha watali au la. Hili swali jepesi sana lakini majibu yanakuwa magumu kutoka.
 
Hebu mwanzo nieleze kwanini mliban maziwa ya kenya bidhaa Ambayo haihusiani na gesi hafifu ya tz
 
Hebu mwanzo nieleze kwanini mliban maziwa ya kenya bidhaa Ambayo haihusiani na gesi hafifu ya tz
Hivi mnajuwa kazi ngapi mliuwa kwa Ku ban gas ya kutoka Tanzania? Halafu mnataka sisi tuwachekee tu na kuwaacha mnazalisha kazi Kenya. Hapa ni jino kwa jino
 
Hilo ndilo tatizo la viongozi wa Kenya la kutowaambia ukweli wananchi wao badala yake wanawafanya always kujiona wao wana haki muda wote na kwamba nchi zingine zinawaonea"crying baby syndrome", hata kuhusu EPA walijenga mazingira ya kuonyesha kwamba Tanzania inataka kuhujumu uchumi wa Kenya, eti Tanzania isifanye vile inavyoona ni sawa kwasababu tu Kenya ita athirika.

Sasa katika hili, kama kweli Kenya ndiyo iliyokua na haki, kwanini baada ya Tanzania kulipiza kwa kupunguza safari za KQ waliamua kuruhusu?, je Kenya imekua very weak kwa Tanzania kiasi cha kushindwa kupigania haki yake badala yake ina surrender kwa pressure ya Tanzania.

Kumbuka hadi leo Kenya imekataa kutekeleza makubaliano ya usafiri wa anga katika ya Kenya na Tanzania kwa zaidi ya miaka 35 sasa, ila hilo viongozi wa Kenya hawalisemi na wala wakenya wengi hawalijui, hii ni kwasababu Kenya inafaidika zaidi, wala husikii Tanzania ikilalamika kwamba Kenya inazuia biashara kwa upande wake.
 
Viongozi wao wana waachia magazeti yao ndio yaamdike ili kujivuwa lawama. Na magazeti yao ni ya kidaku kupidukia kwa kupidua-pidua ukweli in favour ya Kenya. Wanachi wao wakisoma kwenye magazeti hata hawaweki mbili na mbili kujuwa ukweli ni upi. Matokeo yake ndio haya, kila kitu Magufuli mbaya. Ilikuwaga Kikwete sasa ni Magufuli
 
Hivi mnajuwa kazi ngapi mliuwa kwa Ku ban gas ya kutoka Tanzania? Halafu mnataka sisi tuwachekee tu na kuwaacha mnazalisha kazi Kenya. Hapa ni jino kwa jino
Hauajajibu swali!
Anyway, hivi unajua watoto wangapi wamekosa elimu mlipo ban walimu wa Kenya ?

Hivi unajua ni kazi ngapi mliua na wakulima wangapi mliwapotezea biashara mlipo ban maziwa ya kenya... Hivi uko aware kua nusu ya hayo maziwa (processed milk) tunayowauzia huko Tz hua yametoka kwa wakulima wa tz wanaouzia kampuni za Kenya Raw milk ambapo Kenya hua inanunua kwa bei ya juu kuliko vile kampuni za Tz hununua?
 
Sijasikia hata mkulima mmoja wa Tanzania aliyelalamika kuhusu ban. Nyinyi mnadhani choices has NO consequences. Walimu wengi wa kenya walifukuzwa kwa kujifanya wajanja wa kutokufata utaratibu wala kulipa kodi. Wenye vibali wapo na hawana shida. Tatizo wakenya mlitegemea solo la EAC ni la kenya tuu. Sasa hivi mna panic, mna rusha MAWE YA BAN bila muelekeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…