Wakaguongo
Member
- Sep 23, 2026
- 95
- 38
Kipruto, bingwa wa London Marathon mwaka 2022, alifanya hatua yake ya ushindi katika sehemu ya mwisho ya mbio, akimwacha bingwa mtetezi Jacob Kiplimo wa Uganda. Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Kipruto katika Chicago Marathon baada ya kumaliza wa tatu mwaka 2024 na wa pili mwaka 2025.
Aidha kina dada wameiweka Kenya kwenye jukwaa la mbio hizo baada ya Sharon Lokedi kumaliza wa pili kwa muda wa saa 2:14:07, akiweka rekodi mpya ya maisha yake huku Brigid Kosgei akimaliza wa tatu kwa saa 2:14:55.
Hata hivyo, ushindi wa wanawake ulienda kwa Methiopia Hawi Feysa, ambaye alitetea ubingwa wake kwa muda wa saa 2:13:33. Kwa mujibu wa World Athletics, ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya marathon ambapo wanawake watatu walimaliza ndani ya saa 2:15.
Matokeo hayo yanaendeleza historia ya Kenya katika mashindano makubwa ya marathon duniani, huku wanariadha wa Kenya wakiendelea kushindana katika kiwango cha juu kabisa.
Unadhani ni kitu gani kinaifanya Kenya iendelee kutoa wanariadha wanaoshindana na kushinda katika marathon za kiwango cha dunia?