Kenya haipaswi kuwa “eneo la kuzuia virusi vya Ebola” kwa Marekani

Kenya haipaswi kuwa “eneo la kuzuia virusi vya Ebola” kwa Marekani

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG41N1148114019.jpg

Mwezi Juni kwa kawaida huwa ni msimu wa baridi na wa kupendeza katika maeneo ya uwanda wa juu wa Afrika Mashariki. Lakini wakazi wa Nanyuki katikati mwa Kenya siku hizi wana hasira kubwa. Wamekusanyika katika malango ya Kituo cha Anga cha Laikipia, wakifanya maandamano ili kupinga kuanzishwa kwa kituo cha karantini kwaajili ya raia wa Marekani ambao wanahisiwa kuambukizwa virusi vya Ebola.

Tangu mwezi uliopita, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imekuwa ikibaliwa na mlipuko wa Ebola. Kwa mujibu wa takwimu, nchi hiyo imethibitisha wagonjwa 343 wa Ebola, huku watu wengine takriban 1,000 wakihisiwa kuambukizwa. Dalili za kuenea kwa virusi hivyo tayari zimeibuka. Uganda imeripoti watu tisa waliothibitishwa kuambukizwa. Kenya bado haijarekodi mgonjwa hata mmoja aliyethibitishwa kuambukizwa, na inafanya kila iwezalo kuzuia virusi hivyo kuingia nchini.

Serikali ya Marekani imefafanua sababu ya kufanya hivyo: ili kulinda usalama wake wa ndani, imeamua kuwaweka karantini raia wake walioambukizwa Ebola nje ya nchi. Shirikisho la Madaktari wa Kenya limelaani likisema kuwa, ikiwa kitu fulani ni hatari sana kwa Marekani, basi kitu hicho hicho ni hatari zaidi kwa Kenya.

Kitendo hiki cha Marekani kimekumbana na upinzani mkali kutoka kwa jamii ya Kenya. Watu wa Kenya wanaona hili si kana kwamba ni jambo la kidiplomasia, bali ni kama kitendo cha “kuwaweka mamilioni ya Wakenya katika uwezekano wa kuwa na janga”. Mwanasheria mmoja wa Kenya aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba mtu yeyote anayethubutu kuwaleta Wamarekani wenye virusi vya Ebola nchini Kenya, atakuwa msaliti. Siku mbili kabla ya watu wa Nanyuki kufanya maandamano, Mahakama Kuu ya Kenya ilitoa amri ya kusimamisha ujenzi wa kituo hicho cha karantini, na kupiga marufuku kuingia kwa wagonjwa wowote wa kigeni, wakati wa kushughulikia kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanasheria cha Kenya pamoja na shirika moja la usimamizi wa katiba, ambao wamedai kwamba kutokana na miundombinu dhaifu na rasilimali chache za mfumo wa afya wa Kenya, wagonjwa wa kigeni wa Ebola hawapaswi kuruhusiwa kuingia kwenye nchi hiyo.

Ili kukabiliana na malalamiko makubwa ya watu wa Kenya, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ametangaza kutenga dola milioni 13.5 ili kuunga mkono juhudi za Kenya katika kuzuia na kudhibiti Ebola. Hata hivyo, watu wa Kenya wanaona kuwa, fedha hizo hazipaswi kuchukuliwa kama msaada wa kweli, bali ni malipo ya aibu yanayokusudiwa kununua ukimya wa watu. Inajaribu kuficha ukweli ulio wazi: Marekani inatumia uwezo wake wa kiuchumi ili kuifanya Kenya kuwa eneo lake la kuzuia virusi.
 
Wakenya tunajua ni Wazungu weusi sioni kosa la Marekani kwenda Kenya kwa Wazungu wenzao!!!!

Kenya ni mshirika wa Wazungu wenzao!!!
Kwenye rahaaa na shida!!!
 
Afadhari Wakenya walishtuka mapema,huku Tanganyika kingefanya kazi hata mwaka mmoja ndo tungegundua kwamba kilijengwa!!!

Mahakama zetu yaani ndo zisingethubutu kabisa kukemea na kusimamisha ujenzi wake
 
Back
Top Bottom