Shigganza
Senior Member
- May 24, 2018
- 160
- 412
Mahakama kuu Nchini Kenya imepiga marufuku mapenzi ya jinsi moja, hii inafuatia mahakama kuridhia Sheria inayozuia mapenzi hayo kuendelea kutumika kinyume na matarajio ya wapenzi wa jinsi moja na wanaharakati ambao walipeleka shauri mahakamani kuomba Sheria hiyo ifutwe.
Katika uamuzi wa mahakama pamoja na mambo mengine majaji wameamua Sheria inayopingwa, maarufu kanuni ya 162 hailengi makundi yoyote maalaum ya watu badala yake inaeleza kwamba ni Makosa kwa yeyote kushiriki katika uhusiano wa aina hiyo, mahakama ilieleza kutambua haki za binadamu hata hivyo Sheria imeweka MIPAKA au UKOMO wa baadhi ya haki za binadamu. Kwa mujibu wa Sheria Nchini Kenya mtu anayepatikana kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Kufuatia uamuzi huo wa Kenya ni matarajio ya wengi wapenda hasa. WAPENDA usawa kuona mataifa ya Magharibi na Marekani kutoonesha DOUBLE STANDARD kwa kuchukua hatua ikiwemo kutoa matamko ya kulaani uamuzi wa mahakama, kutishia au kuinyima misaada Nchi ya Kenya kama yalivofanya kwa Tanzania baada ya Serikali ya awamu ya tano ilipoamua kulinda maadili ya kitanzania
Baadhi ya wanaharakati Nchini akiwemo Fatuma Karume, Maria Sarungi ni wakati wa kuwa na kutafakari kubwa kuhusu misamamo yao hasa kwenye baadhi ya 'haki za binadamu' , kwani kwa mataifa mengi ya Afrika masuala ya mapenzi ya jinsi moja HAYAKUBALIKI na hayapaswi kupewa baraka na Sheria, Kanuni na Katiba za Nchi kwa KUTAMKA KUYATAMBUA.
Tunapata funzo jingine ni muhimu wananchi bila kujali itikadi zetu za kisiasa kuunga mkono pale Serikali inapofanya au kusimamia jambo lenye maslahi kwa Nchi, wakati mataifa ya Nje yanatoa matamko na kutishia kuidhibu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madai ya kupinga mapenzi ya jinsi moja, wafuasi wa vyama vya Upinzani na wakosoaji wa Serikali ya awamu ya Nne ghafla waligeuka kuwa wadau wa mapenzi ya jinsi moja wakiyaunga mkono mataifa ya nje kuibana Serikali ikiwezekana hata kuinyima misaada ilimradi tu wafanikishe maslahi yao ya Kisiasa.