Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Sanduku hilo lilipatikana karibu na makutano ya Napeililim katika barabara ya Lodwar kuelekea Kakuma, lilikuwa limefungwa lakini lilikuwa na shimo chini.
Maafisa wa Chama cha Jubilee walikuwa wa kwanza kuwasili eneo hilo baada ya kuarifiwa na wafugaji walithibitisha kuwa sanduku hilo halikuwa na karatasi za kura ndani.
Mwenyekiti wa Chama hicho katika kaunti hiyo, Bw James Kuya alisema shimo katika sanduku hilo ni kubwa, ishara kwamba karatasi za kura zilizokuwepo zilitolewa.
"Masanduku yote ya uchaguzi na vifaa vingine vinavyotumiwa ni lazima viwe mikononi mwa Serikali. Kwa nini sanduku hili liko hapa siku saba baada ya uchaguzi?", aliuliza
Alisema viongozi wa Jubilee katika kaunti hiyo walikuwa wamelalamika kuhusu jinsi Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC ilivyosimamia uchaguzi eneo hilo.