Kenya imeondoa VAT kwenye Magari ya Utalii

Tanzania ndio inanunua body za mabasi Kenya...Master Fabrication Ni kampuni kubwa ambapo Basi nyingi za Tanzania zinatengenezwa huko

Kenya walianza kutengeneza body za magari ya safari kabla ya Tanzania.
Hapa tunaongelea magari ya kubeba watalii, ambo kuna kampuni iko Arusha wao ndio wenye kibali cha Ku modify Toyota land cruiser Africa mashariki yote. Na hizo gari zinauzwa Kenya na south Africa.

HAL | Re-defining Safari Vehicle Conversion

Ukija kwenye mabasi ya abiria siku hizi makampuni mengi ya Tanzania yananunua mabasi kamili toka South Africa chini ya mwamvuli wa SADC.
 
Sasa ukisema hivi, mbona Tanzania ndio nchi inayopata watalii wengi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki?
 
We are officially a failed state economically
 
Sasa ukisema hivi, mbona Tanzania ndio nchi inayopata watalii wengi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki?
Umekielewa nilichoandika hapo na sababu inayofanya utalii uelekee pabaya lakini?..hao watalii wengi ni hao ambao wanapita na Kenya au?.

Hata kama tunaongoza kwa idadi ya watalii kusipokua na mipango efficient hiyo idadi itashuka ipasavyo
 
Asalam
Kama mambo ni hayo naona hii taasisi ya tourism itazidi kudidimia.
Mwaka jana nilienda mitaa ya soni, lushoto. Basi kule kuna hoteli nzuri na hali ya hewa saafi sana. Sasa nilikuwa na broda mmoja wa mambo ya tour. Sasa kwenye matembezi yetu kuna mtu mmoja kwa mbali akatusalimia huku akitutizama saana. Mm kwa kweli sikufurahiwa na ile tabia lakini tukampotezea sasa mbeleni nikamuuliza yule broda yule mtu ni nani? Jibu ni yule ndugu ni mtu wa uhamiaji na akanielezea mausumbufu yao kwa watalii. Akaendelea kueleza ya kwamba huwa wanaenda hoteli zile zinazofikia watu wa nnje kama wazungu na wengineo usiku na kuanza kuwagongea vyumbani mwao na kuanza kuwauliza visa na vyeti vya utambulisho na kadhalika.
Kwakweli kama mambo yataendelea hivi bila uvumbuzi tz itakosa sana soko la watalii na ni vibaya nchi iliyobahati na vivutio vingi kukosa wateja.
 
Umekielewa nilichoandika hapo na sababu inayofanya utalii uelekee pabaya lakini?..hao watalii wengi ni hao ambao wanapita na Kenya au?.

Hata kama tunaongoza kwa idadi ya watalii kusipokua na mipango efficient hiyo idadi itashuka ipasavyo
Nadhani unasema haya huku ukidhani utali wetu unaporomoka, hakuna vielelzo vyoyote vinaonyesha tunashuka kiutalii. Kwanza kabisa watalii wanaokuja Tanzania kipitia Kenya wamepinguwa sasa, kutokana na watalii wengi wanapenda kuja moja kwa moja Tanzania. Ugaidi pia unawaogopesha kutua Kenya, nchi kama Marekani bado wana tamko la kuwatadharisha watu wao wawe makini wakiwa Kenya. Hoteli zinaongezeka Tanzania, vivutio vya kusini vinaanza kuimarishwa na kutagazwa. Sasa sujuwi wapi unafikiri Tanzania inakosea. Zanzibar peke yake, inapata watalii wengi kuliko Kenya yote.
 
Hivyo vielelezo vingine unavyovitaka utavitafuta on your own time. Nimezungumzia effect ya kuweka VAT kwenye viingilio vya National parks. Mimi ni mdau wa utalii (Usiniulize kivipi). Tangu ongezeko la VAT June last year tumeona bookings na income vikishuka compared to last year (2015) ambao pamoja na vuguvugu la uchaguzi watalii bado walikua wakiingia.

Kuna watakaosema tunaogopa changes but ili change iwe na tija kwa wote it has to be orchestrated.

Ps. Endelea kuamini katika matangazo ya southern circuit as if yameanza this time. Northern Circuit pamoja na ubora wake still matangazo yamekua finyu na ambayo hayawi financed properly.

Something has to be done.
 
Kampuni kama KVM zina convert all range of vehicles hata za ambulance, including safri land cruiser, ni rahisi sana kupata Kibali as long as unaonyesha uwezo wakufanya professional job ambayo haitashusha hadhi kampuni iliotengeneza gari lenyewe.....
Pitia hapa uone mapicha Conversions

Eti "Ukija kwenye mabasi ya abiria siku hizi makampuni mengi ya Tanzania yananunua mabasi kamili toka South Africa chini ya mwamvuli wa SADC"

Nai alisema hivyo? wapi proof??? Yani uko radhi utaje hadi SA ilimradi usikubali mengine yanatoka hapa Kenya ambapo body building ikimalizika inasafirishwa hadi Tz, UG, Rwanda kwa Urahisi manake ni karibu, Ukiona bus ambayo hapo nyuma imeandikwa body build by MCI ujue iko Kenya..
Hata sijaongelea akina KVM na ile nyengine iko mombasa nimesahau jina yake ambao hao ndo babu kubwa hapa Kenya ikija kwa industry ya magari
 
Usishangae watalii kuja Tz. Luna mengi ya Kuja kutalii. Eg. Kuona hao wa Tz wanaopata msaada toka Ethiopia .wenye wasomi wa kiwango cha juu KBS cha kukariri.
 
Wow, hata wewe umekuwa brainwashed, hii hoja ya VAT wapinzani walishikilia bango lakini wakaibwaga kama jadi yao. Hivi wewe unasema unafanya kazi on tourism industry si ungejuwa hata takwimu moja au mbili. Usitudanganye mkuu, mwaka 2015 Tanzania tulipata watalii 2million. VAT has shown little sign of number declining. Kwanza ndio kwanza watalii wameongezeka, huku wewe unasema wamepunguwa ....proof wapi!!!! Kilimajanro imeongezeka sana, deep dive watalii wameongezeka, watalii wanaokuja kufanya utafiti mafia wameongezeka, (hawa wanaokuja na meli zao za utafiti wanakaa hapo miezi mitatu, sita, wengine hadi mwaka) usikubali ya kuambiwa fanya utafiti. Unataka kusema mtali anaetoka South Africa na gari yake, anakuja kuingia mbugani na gari yake amesha panga kutumia $5,000- 7,000 atashidwa kulipa VAT 18%? Au hata mtalii aliyrtoka marekani au ulaya. Wanaotunyonya na kupiga kelele ni makampuni ya utali ambayo yanatupa mahesabu ya uwongo wakati wao wanalipwa hela yao nje.

Tanzania: Tourist Arrivals Increased By 10 Per Cent in 2016
 
Umeanza kuleta mambo ya "wapinzani walishikilia bango"..usiniweke kwenye siasa mana sijadili politics. Ukienda na politics kwenye maswala ya aina hii utaprove failure. Usinihusishe kabisa na siasa..kama wapinzani walisema hivyo thats upto them.

Unaweza kunipa official source ya wapi umetoa takwimu za idadi ya watalii kufika 2 Million? Au ni data za kutengenezea nyumbani kwako?.

Sasa turudi nyuma..Tanzania tulibreak the 1 Million marker ya idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vyetu mwaka 2012 kama sijakosea, na tukaendelea na trend hiyo mpaka 2015 ambapo idadi ilishuka mpaka roughly 960, 000 na hii kulingana na akili yangu (ambayo according to you nimekua brain washed) kushuka huko kulisababishwa na unpredictable political situation ya mwaka huo kitu amabacho hata wewe utakubaliana na mimi.

Sasa ikaingia 2016 mambo yakaonekana yako shwari people started planning about their vacations na kufanya booking. Suddenly kufika May serikali ikatangaza badiliko kubwa kwenye sekta. Wale waliokua wamepanga tayari safari zao wakawa hawana la kufanya zaidi ya kuendelea na mipango.

Takwimu zikatoka last year kwamba kumekua na ongezeko la 10% ambalo in reality ni kurejea tu kwa idadi ya awali ( Ili uelewe zaidi chukua 10% ya idadi ya 2015 kisha jumlisha mwenyewe). Sasa kwakua wewe umeamua kutokubaliana na swala hilo wait takwimu za 2017 utafikia conclusion ambayo utaona inafaa.
 
Sijaona basi huku kwentu na maneno MCI (and I'm not trying to be funny). Ukija kwetu na ukaenda kwenye makampuni ya mabasi Dar express, Kilimajanro express etc ukiwailiza watakwbia most of there fleet inatoka SA. Hata expansion loans wantowa huko huko.

In regard to tour van, kuna kampuni ziko Arusha ambao wanatengeneza specific style ya hizo tour van (utaona kwenye link below). Ni Tanzania tuu ndio walipewa kibali na Toyota to build those van in that style (enclosed van). Za Kenya ziko wazi covered with canvas hawawezi Ku copy ya Tanzania kwasababu imewekwa copyright. Na tunauza hizo van Kenya south Africa, sometimes mpaka Europe.

Safari Vehicles - Bobby Tours Tanzania Safaris, Tanzania Safaris, safari tanzania, mount Kilimanjaro climb

http://allafrica.com/stories/201503030050.html

HAL | Re-defining Safari Vehicle Conversion
 
Soma kabla huja jibu, wapi nilikuambia wewe ni mpinzani? Nilichosema, hoja kama hiyo ilibebwa na wapinzani lakini wakaibwaga kwakuwa takwimu hazikuqa upande wao. Mkuu unafanya kweli kwenye tourism industry au unababaisha. Any that is your problem, Lakini hata kugoogle kidogo tuu imeshidwa. Hebu fanya hata kazi ndogo ya kadakua mtadaoni (Tanzania 2million tourist). Magufuli aliliongelea hili swala wakati mfalme wa Morocco alivyo kuja, na hilo nalo hukulisikia?
 
Nilichikuambia ni usinihusishe na SIASA mambo ya wapinzani walisema usiyalete hapa ongelea ninachokiandika. Nilikuelekeza mwanzoni kwamba swala la mimi kua mdau wa utalii usiliulize sana.

Hivi tunaongelea expectations hapa au reality? hizo za 2 M ni expectations za 2017 sio real data za 2017. Nilizokuwekea hapo juu na ninachokiandika ni reality. Na usitegemee hata kidogo unless uwe unaota mchana kwamba kutakua na 100% increase ya watalii kwenye nchi ambayo last year ilikua na ongezeko la 10% only..narudia tena maybe IN YOUR DREAMS!.
 
Majibu ya mtazania aliyekata tamaa na maisha. Pole, the number has already pass expectation, and you of the all people should know unless umetydanganta kazi unayo fanya. Lakini unashindwa hata kutushawishi kama utali umeshuka. I have given you the links before, umezipuuza. Makampuni ya ndege Ethiopian, KLM wanabadiki ndege za kuja tz na kuleta kubwa na safari zinaongezeka unafukiri wanabeba nini huko, kuku?
 
The number has already passed expectations?, You must be out of your mind. Halafu Soma ile comment uliyoquote part of it kabla ya kunieleza mambo ya kunipa links.

Au ngoja nikuwekee hapa ujisomee tena

Umeanza kuleta mambo ya "wapinzani walishikilia bango"..usiniweke kwenye siasa mana sijadili politics. Ukienda na politics kwenye maswala ya aina hii utaprove failure. Usinihusishe kabisa na siasa..kama wapinzani walisema hivyo thats upto them.

Unaweza kunipa official source ya wapi umetoa takwimu za idadi ya watalii kufika 2 Million? Au ni data za kutengenezea nyumbani kwako?.

Sasa turudi nyuma..Tanzania tulibreak the 1 Million marker ya idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vyetu mwaka 2012 kama sijakosea, na tukaendelea na trend hiyo mpaka 2015 ambapo idadi ilishuka mpaka roughly 960, 000 na hii kulingana na akili yangu (ambayo according to you nimekua brain washed) kushuka huko kulisababishwa na unpredictable political situation ya mwaka huo kitu amabacho hata wewe utakubaliana na mimi.

Sasa ikaingia 2016 mambo yakaonekana yako shwari people started planning about their vacations na kufanya booking. Suddenly kufika May serikali ikatangaza badiliko kubwa kwenye sekta. Wale waliokua wamepanga tayari safari zao wakawa hawana la kufanya zaidi ya kuendelea na mipango.

Takwimu zikatoka last year kwamba kumekua na ongezeko la 10% ambalo in reality ni kurejea tu kwa idadi ya awali ( Ili uelewe zaidi chukua 10% ya idadi ya 2015 kisha jumlisha mwenyewe). Sasa kwakua wewe umeamua kutokubaliana na swala hilo wait takwimu za 2017 utafikia conclusion ambayo utaona inafaa.
 
The number has already passed expectations?, You must be out of your mind. Halafu Soma ile comment uliyoquote part of it kabla ya kunieleza mambo ya kunipa links.
Kinacho kupigisha kelele hata sijuwi ni nini, ni kwamba tourism industry tz imekufa au. You've baseless claim ambazo unashundwa hata kuzisukuma. Bajeti inakuja June, itakubidi uje ututhibitishie haya unayoyasema kama utali wetu imekufa kwaajili ya VAT (Mimi nitakutafuta hapa jf). Halafu unasema unafanya kwenye park.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…