Kenya imetoa mwanya kwa Congo River Alliance's kufanya mipango ya mapinduzi Congo na RSF kuigawa Sudan

Kenya imetoa mwanya kwa Congo River Alliance's kufanya mipango ya mapinduzi Congo na RSF kuigawa Sudan

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,042
Reaction score
3,674
Kenya katika EAC inaelekea kuwa kitovu cha mipango hasi dhidi ya serikali kadhaa za ukanda huu.

Kabla ya vita kupamba moto DRC, viongozi wa makundi mbalimbali ikiwemo M23 walikutana Kenya na kuunda umoja wao yaani Congo River Alliance's baada ya hapo vita ikazuka ya nguvu sana DRC, mipango hii ilifanyika Nairobi na bila shaka Rais Ruto alitoa baraka na hii ni moja wapo ya sababu za Congo kulitaka jeshi la Kenya liondoke DRC.

Katika hali ya kushangaza huku vita vikichukua sura mpya na mbaya zaidi Sudan, Kenya imewakaribisha waasi wa Rapid support forces Nairobi ili kujadili na kukubaliana jinsi ya kuunda serikali yao nchini Sudan 🇸🇩, yaani wawe na nchi yao wajitenge.

Ikumbukwe paia kiongozi wa upinzani Bw. Besigye wa Uganda alikamatwa akiwa Kenya na kukabidhiwa kwa serikali ya Uganda.

Kenya inatakiwa kujitafakari upya juu ya displomasia yake, ni kama vile mipango mingi ya mabeberu kuhusu afrika kwa sasa inafanyikia Nairobi.

Ni kama Sudan sasa inagawanyika na hali hii pia uhenda ikatokea Congo mashariki iwapo AU, UN au jumuiya za kikanda zitashindwa kabisa kuchukua hatua madhubuti na za haraka.
 
Usibabaishwe sana na hiii mipaka ya Wakoloni tunatakiwa tuunganishe Afrika ili hii mipaka ife kifo cha asili.
 
Kenya ni mwanachama asiye rasmi wa umoja wa kujihami wa nchi za magharib/NATO kama alivyoiteua rais Biden miezi michache iliyopita.

Hivyo mjue Kenya ni sufuria la kupika matatizo afrika mashariki na kati wakishirikiana na mwanaintelijensia kagame
 
Propaganda
 
Mwanzoni nilidhani ni propaganda, ila baada ya uchunguzi wa kina ni kweli kabisa ulivyosema.
 
1000283178.jpg
1000283177.jpg
 
Back
Top Bottom