Kenya imetupora ushawishi wetu katika anga za Diplomasia

Kenya imetupora ushawishi wetu katika anga za Diplomasia

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana,

Tanzania ya Mwl. ilikuwa juu sana katika siasa za kimataifa. Tanzania ilikuwa kinara katika siasa za ukombozi Kusini mwa Afrika. Mwl. alikuwa Mwenyekiti wa nchi zilizo mstari wa mbele kupigania uhuru wa nchi za Kiafrika hasa Kusini mwa bara la Afrika.

Tanzania ya Mzee Ruksa ilifuta nyayo za Mwl Nyerere ingawa taratibu tulianza kupoteza heshima yetu katika siasa za kimataifa. Tanzania ya Mzee Mkapa na Kikwete ilijaribu kurejea katika nafasi yake ingawa si kwa kiwango cha juu.

Tanzania ya Mzee Magufuli iliacha kabisa masuala yote ya mahusiano ya diplomasia. Mahusiano yetu na majirani zetu yalikuwa hovyo sana.

Kifupi Mzee Magufuli siasa zake zilituacha hoi bin taabani lilipokuja suala mahusiano mazuri na majirani, wafadhili. Tanzania ya Mama inajitahidi kurejea katika nafasi yake ya uongozi hasa wafadhili na majirani.

Vurugu zilizojitokeza huko Msumbiji tuliona nchi ya Rwanda ikipeleka wanajeshi kusaidia kurejesha amani. Ikumbukwe Rwanda si mwanachama wa SADC.

Vurugu zilinazoendelea huko Congo DRC nchi ya Kenya imechukua uongozi kwa kutuma wanajeshi na Rais Mstaafu wa Kenya ni msuluhishi Mkuu.

Tanzania ipo kando ikisubiri Rwanda watuzalishie wakimbizi na kuharibu usalama eneo lote la mikoa ya mipakani.
 
Hizo gharama utalipia wewe sio?..

Mtu huyuhuyu utakuta analalamikia huduma duni zitolewazo nchini kisa ufinyu wa bajeti but anataka jeshi liende DRC..kwa interest gani kwa nchi yetu?..kama ipo ni sawa..ila kama ni kuonyesha tu kuwa TZ bado ni kinara wa kutunza amani hilo ni big No.
 
Nimefurahishwa na Baraza la mawaziri Kenya, kuutoa mshahara wao wa November kwenda kupunguzia mzigo wa njaa wananchi waliokumbwa na ukame.

Nikatafakari,hivii hii nchi yetu, serikali haiwezi kuamua kutonunua magari mapya kwa kipindi hata cha miaka 3,na pesa zielekezwe kutengeneza irrigation system kwenye maeneo ya kimkakati ili kuwapa fursa vijana wakapige kazi na kuongeza mnyororo wa thamani kwa kuuza mazao na matunda nje ya nchi?

Maana sioni kazi ya mabwana/mabibi shamba nchini,zaidi ya porojo na kujaa maofisini.
 
Kenya wanatuita 'a sleeping giant' washatuona maboya nchi kubwa kama hii yenye rasilimali lukuki unashindwa vipi kuwa na economical and diplomatic dominance katika eneo la EA hadi unaacha nchi kama rwanda na uganda wana undermine regional stability jambo ambalo linaathiri maslahi ya nchi kiuchumi kwa kiasi kikubwa!

Hivi Tanzania hawana maslahi na DRC hadi wakae pembeni waangalie ikivurugwa? Haishangazi baada ya kuiteka Uganda waliachia tu kizembe bila kuitumia kuimarisha uchumi wake uliokuwa umetetereka baada ya vita.​
 
Viongozi wetu siku hizi hawajali, awamu ya Magufuli iliharibu mahusiano yetu kimataifa, Samia akaja na msemo wake wa kufungua nchi, ameanza kuifungua nchi lakini ajabu kabla haijafunguka vizuri, naona nae ni kama ameanza kuifunga tena.

Kwa ile kauli yake kwamba hataki wapinzani kwenye serikali yake afanye nao kazi, hata kama wakimshtaki kwenye sheria za kimataifa yeye atawabana kwa sheria za ndani, anasahau mikataba ya kimataifa tuliingia wenyewe kama nchi kwa mapenzi yetu.

Huyu anaturudisha kule kwa Magufuli tulipotoka, ndio maana Lema akasema utawala wa Samia ni mbaya zaidi ya wa Magufuli, atakuwa ameshaona dalili vile mtawala alivyoanza kulewa madaraka, mtawala wa aina hii anaweza kufanya chochote ili kulinda nafasi yake hasa kuelekea 2025.
 
Kenya walikataa kufuata sera mbovu za Ujamaa ndiyo maana wanaendelea kidiplomasia, kiuchumi, na kidemokrasia.
 
Heshima sana,

Tanzania ya Mwl. ilikuwa juu sana katika siasa za kimataifa. Tanzania ilikuwa kinara katika siasa za ukombozi Kusini mwa Afrika. Mwl. alikuwa Mwenyekiti wa nchi zilizo mstari wa mbele kupigania uhuru wa nchi za Kiafrika hasa Kusini mwa bara la Afrika.

Tanzania ya Mzee Ruksa ilifuta nyayo za Mwl Nyerere ingawa taratibu tulianza kupoteza heshima yetu katika siasa za kimataifa. Tanzania ya Mzee Mkapa na Kikwete ilijaribu kurejea katika nafasi yake ingawa si kwa kiwango cha juu.

Tanzania ya Mzee Magufuli iliacha kabisa masuala yote ya mahusiano ya diplomasia. Mahusiano yetu na majirani zetu yalikuwa hovyo sana.

Kifupi Mzee Magufuli siasa zake zilituacha hoi bin taabani lilipokuja suala mahusiano mazuri na majirani, wafadhili. Tanzania ya Mama inajitahidi kurejea katika nafasi yake ya uongozi hasa wafadhili na majirani.

Vurugu zilizojitokeza huko Msumbiji tuliona nchi ya Rwanda ikipeleka wanajeshi kusaidia kurejesha amani. Ikumbukwe Rwanda si mwanachama wa SADC.

Vurugu zilinazoendelea huko Congo DRC nchi ya Kenya imechukua uongozi kwa kutuma wanajeshi na Rais Mstaafu wa Kenya ni msuluhishi Mkuu.

Tanzania ipo kando ikisubiri Rwanda watuzalishie wakimbizi na kuharibu usalama eneo lote la mikoa ya mipakani.
Mama ameurudisha Tena
 
Back
Top Bottom