Kenya Ina Kipi Cha Kujivunia Toka Ipeleke Majeshi Somalia Takribani Miaka Nane Iliyopita?

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
26,021
Reaction score
79,710
Ikumbukwe kuwa tarehe 16 Oktoba 2011 ndiyo siku KDF walipovuka mipaka na kuingia nchini Somalia. Sababu kubwa ikiwa ni kundi la Al Shabaab kutishia usalama wa nchi ya Kenya.

Miezi michache kabla ya tarehe hiyo Al Shabaab walitekeleza mashambulizi kadhaa nchini Kenya yaliyoacha wengi wakiwa majeruhi na baadi wakifa.

Lengo kamili la KDF kuingia Somalia ilikua ni kuilinda Kenya dhidi ya mashambulizi ya Al Shabaab na kuwasaidia Wasomali kujenga serikali yao imara ili waweze kupambana wao wenyewe dhidi ya kikundi hicho cha kigaidi.

Ripoti kadhaa zimejaribu kueleza sababu zilizoisukuma serikali ya Kenya kuingiza majeshi nchini Somalia ili kupambana na Al Shabaab, baadhi ya hizo sababu ni:

1. KDF kutaka kuonyesha kuwa wanaweza kupambana na adui yeyote, kitu ambacho hata raisi wa Ugand bwana Y. K. Museveni alikejeli (katika mazungumzo yaliyovuja akiongea na mwanadiplomasia wa Marekani) kuwa jeshi la Kenya ni "career army" lilalojitutumua kupambana na haliwezi kupigana na Al Shabaab wanaotumia mbinu za vita vya misituni (guerrillas).

2. Jambo jingine ni kuwa hadhi ya Jeshi la Uganda wakati huo ilionekana kupanda kutokana na mission waliyokuwa nayo Somalia (chini ya AU) hivyo kupelekea KDF kuona kuwa inachafua their "self proclaimed" reputation kama the "superior military power" in East Africa. Hivyo ilikua ni lazima kuvuka border ili kulinda hiyo status na kurudisha imani ya wananchi waliokuwa wamechoshwa pia kwa skendo za rushwa katika jeshi hilo.

3. Report mbalimbali zinasema kuwa viongozi wakubwa nchini Kenya (wakati huo) walitarajia KDF kuwa integrated katika mission ya AU ya kulinda amani Somalia ambapo kwa wakati huo iliundwa na vikosi kutoka Burundi, Uganda na Djibouti. Kuunganishwa ka Kenya kwenye mission hiyo kungemaanisha kuwa gharama ambazo zingetumika zingetolewa na wahisani wa kimataifa na sio bajeti ya serikali ya Kenya.

4. The Somali Connection

Pamoja na kuwa mwanzoni raisi Mwai Kibaki alisita kukubali kupeleka jeshi nchini Somalia. Ripoti zanasema kuwa alishawishiwa na viongozi wa juu wakiwemo Minister of Internal Security (George Saitoti), Minister of Defense (Yusuf Haji), Mkuu wa Majeshi (Julius Karangi) na Chief of Intelligence (Michael Gichangi).

Yusuf Haji (Waziri wa Ulinzi), mwenye asili ya Somalia, inasemekana ndiye aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa raisi Kibaki. Ikumbukwe kuwa huyu Haji alikuwa anaunga mkono juhudi za kuundwa kwa Jubaland (independent state) ndani ya Somalia karibu na mipaka ya Kenya. Jubaland inajulikana kwa kuwa na wingi wa gas and oil deposits.

Huyu Haji ikumbukwe pia kuwa alikua na matamanio ya kuunganisha ukoo wake wa Ogadeni ambao umesambaa Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Ethiopia na Somalia.

Davidi Throup ambaye ni mchambuzi wa siasa za Kenya aliwahi kunukuliwa akisema.....

"Maslahi binafsi ya kiuchumi na kisiasa ya viongozi wa ngazi za juu na wanajeshi kutoka Kaskazini Mashariki mwa Kenya (Ogadeni Somali Community) vilichangia kwa kiasi kikubwa katika maamuzi ya kupeleka KDF Somalia."

5. Sababu nyingine ni nia ya serikali kuendelea kupata misaada kutoka mataifa ya Magharibi (USA to be precise). Baada ya balozi ya US kulipuliwa mwaka 1998 nchini Kenya, USA wali consider Kenya kama strategic ally katika kupambana na ugaidi.

Hivyo basi Kenya walihitaji kulinda reputation yao kwa kuunga mkono juhudi za USA katika kupambana na ugaidi, hakukuwa na njia zaidi ya kuingia Somalia kupambana na adui.



MATOKEO

Miaka takribani nane sasa tokea Kenya kuingia Somalia bado majeshi ya KDF yapo Somalia na bado Al Shabaab wanaendelea kuwa tishio kwa serikali ya Kenya.

Tunaweza kukumbuka matukio kadhaa ya kigaidi nchini Kenya yaliyoanza kutekelezwa na Al Shabaab wiki kadhaa tu baada ya KDF kuingia Somalia. Kati ya hayo ni mashambulizi ya Mwaura's, Machakos Bus Terminal, E. A. Pentecostal Church na mengine countless ambayo ni small scale.

Matukio notable ni kama mashambulizi ya Westgate, Garrisa na hivi karibuni DusitD2 Hotel.

Kama sababu ya KDF kuingia Somalia ilikua ni kuifanya Kenya iwe salama dhidi ya Al Shabaab ili iweze kuvutia wawekezaji basi kwa asilimia kubwa mission ime-fail. Ingawa kuna foreign investors lakini kitendo cha kuendelea kuwepo Al Shabaab ndani ya Kenya na kuendelea kufanya mashambulizi kila watakapo ni ishara kuwa KDF imeshindwa.

Wanajeshi wanauwawa kila uchwao na wengine kuchukuliwa mateka na Al Shabaab. Raia wanauwawa kila Al Shabaab watakapotaka kuua. Somalia mpaka sasa hawajaweza kuwa na stable government. Hizo zote ni dalili za kushindwa. Nashauri serikali ya Kenya iondoe KDF Somalia kwa sasa ili mfanye evaluation kuona mmekosea wapi na nini way forward.


Natoa Credit kwa: The Conversation, CSIS, Crisisgroup, Wikileaks, Daily Nation.
 
Mmarekani alimkimbia general Aidid
Na hawa wanakufa na tai shingoni
Waacheni wafe tu wabakaji hao

Sent from my SM using Tapatalk
 
Ukisikia kuwasha moto ambao unakushinda kuzima ndio hii,Kenya sio kama hawawezi kutoka Somalia,wanachohofia hapa ni kuwa wakitoka bado itaonekana wameshindwa, na Alshabab hawatawaacha kwani watajua hawa jamaa ni wachovu,kwahiyo wanaona bora waendelee kukaa Somalia ili waonekanae kuwa bado wanauweza mchezo...
 
Consequences za kuendelea kubaki Somalia ni negative zaidi ya faida. Kwanini wasitoke wakaendea kuji evaluate?

Kuna video nimeiona imenitia masikitiko sana. Nikiweza nita upload.
 
kdf wameshindwa kabisa huko somali land warudi nyuma kabisa na pia kuwa na muunganiko na wasomali katika serikali yao na katika jeshi lao "ASILI HAIWEZ KUACHA ASILI" na pia wana poor milltary intellgncy
guarill war ni ngumu sana si rahisi kama wao wanavyo dhani warudi nyuma tu then wapige ambush moja wakiwa na 100% milltary intellgncy
 
binafsi naona ni sababu za kiusalama unajua KDF walipo ni kusini mwa Somalia karibu na Kenya na hayo maeneo ndio Al shaabab wananguvu na walikimbilia huko mara baada ya kufurushwa pale Mogadishu na UPDF (Uganda) mi nafikiri wakiondoa majeshi yao bac kuna hatari kubwa sana hawa Al shabaab ku sambaa zaidi sababu tayari wapo ndani ya Kenya na wakiachwa wasambaaae zaidi nafikiri itakuwa ni hatari hata kwa baadhi ya nchi zilizopo ktk jumuiya ya afrika mashariki. Offcourse unaweza ona ni kama waliingia kwa maslahi binafsi lkn tazama matokeo yake ss iv hao magaidi wapo ndani ya Kenya kila uchao wanafanya matukio nafikiri ss iv Kenya wanahitaji msaada mkubwa sana wa ULINZI sio wamipaka yao tu bali hata ndani ya Kenya
 
Serikali ikiwa unstable ni ngumu sana kushinda vita nyie wakuja,somali siyo sehemu salama,waite mazungumzo ya amani tu al shabab,wakae mezani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Observation nzuri mkuu, ila katika issue kama hii unatakiwa urudi nyuma mpaka katika pre-incursion period. Je Al Shabaab hawakuwepo?

Na kama walikuwepo je walikuwa threat to what extent? Ndio uje sasa kwenye post-incursion era, imekuwa na faida gani au hasara gani? Je kama nchi inaumia tu ingawa inajitahidi ku thwart potential threats je ni vibaya ku fall back na kuanza upya ili kurekebisha penye palikua hapajakaa sawa?
 
Mimi nashindwa, shida ya hawa watanzania ni gani?

1. KDF haitumii pesa yao.
2. Somalia hawana border na wao.
3. Somalia ikiwa na amani ama vita, Tanzania haifaidiki kwa lolote.
4. Tanzania haina refugee wowote kutoka Somalia.
5. Somalia ikiwa na amani, wanabiashara wao bado hawataweza chapa kazi.
6. Tanzania haina exports zozote kwenda Somalia.

Wakenya hawafungui thread kila dakika kumi kusema tutoke Somalia, lakini watanzania ndio hao.
 
ati brothers hakuna u brotherhood hapa, kama nyinyi jeshi lenyu la kuvunja matofali liko imara ingieni somalia then mmalize alshabaab as ur claim

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani hujaona vyenye tuliwa thwart huko kibiti, rufiji?

Sijaleta mada hii kama sehemu yenu ile ya ku brag about military prowess. Nimejaribu kufanya critical thinking, some kind of objective analysis.
 
Unakosea sana budaa. Ladba ka hujui kuwa tupo na trade bloc between EAC members. So pakiwa hakuna stability Kenya, all members of the bloc are affected in one way or another.

Kuna EAC summit on 1st of February i hope wanaweza kuzungumzia hili swala.
 
since u tanzanians aint in somalia ,why dont u mind your business ,whether tuko.somalia au hatuko why does it concern your ass?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona tunaumia na kuwa concerned na matatizo yenu ujue tunawapenda,kenya na Tanzania ni ndugu,mi nna ndugu kibao huko hivyo siwezi kufurahia nyie mkipata majanga.ndio maana tunawashauri mtoke somalia badala yake muelekeze nguvu kwenye kulinda mipaka yenu na ku eradicate sleeper cells za hao maharamia zilizopo humohumo ndani kwenyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Okay ila lazima ujiulize pia AMISOM inawanajeshi toka Uganda kabla ya kuondoka, Kenya, Ethiopia, Djibouti, na Burundi LKN jiulize kwann KENYA ? hapo ss swali lako la pre na post Incursion liweke ktk mabano, WHY Kenya ? kwann Al shabaab hawashambulii Ethiopia, au Burundi. Hitimisho langu ni kwamba mpaka ss Kenya wanafanya vizuri kupambana na magaidi JAPO KDF wakitoka Somalia bac mi nina imani bado mashambulizi yatakuwepo tu sababu tayari magaidi wengine ni wa Kenya pia tazama dusit attack tumesikia baadhi ya magaidi ni wakenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…