Ikumbukwe kuwa tarehe 16 Oktoba 2011 ndiyo siku KDF walipovuka mipaka na kuingia nchini Somalia. Sababu kubwa ikiwa ni kundi la Al Shabaab kutishia usalama wa nchi ya Kenya.
Miezi michache kabla ya tarehe hiyo Al Shabaab walitekeleza mashambulizi kadhaa nchini Kenya yaliyoacha wengi wakiwa majeruhi na baadi wakifa.
Lengo kamili la KDF kuingia Somalia ilikua ni kuilinda Kenya dhidi ya mashambulizi ya Al Shabaab na kuwasaidia Wasomali kujenga serikali yao imara ili waweze kupambana wao wenyewe dhidi ya kikundi hicho cha kigaidi.
Ripoti kadhaa zimejaribu kueleza sababu zilizoisukuma serikali ya Kenya kuingiza majeshi nchini Somalia ili kupambana na Al Shabaab, baadhi ya hizo sababu ni:
1. KDF kutaka kuonyesha kuwa wanaweza kupambana na adui yeyote, kitu ambacho hata raisi wa Ugand bwana Y. K. Museveni alikejeli (katika mazungumzo yaliyovuja akiongea na mwanadiplomasia wa Marekani) kuwa jeshi la Kenya ni "career army" lilalojitutumua kupambana na haliwezi kupigana na Al Shabaab wanaotumia mbinu za vita vya misituni (guerrillas).
2. Jambo jingine ni kuwa hadhi ya Jeshi la Uganda wakati huo ilionekana kupanda kutokana na mission waliyokuwa nayo Somalia (chini ya AU) hivyo kupelekea KDF kuona kuwa inachafua their "self proclaimed" reputation kama the "superior military power" in East Africa. Hivyo ilikua ni lazima kuvuka border ili kulinda hiyo status na kurudisha imani ya wananchi waliokuwa wamechoshwa pia kwa skendo za rushwa katika jeshi hilo.
3. Report mbalimbali zinasema kuwa viongozi wakubwa nchini Kenya (wakati huo) walitarajia KDF kuwa integrated katika mission ya AU ya kulinda amani Somalia ambapo kwa wakati huo iliundwa na vikosi kutoka Burundi, Uganda na Djibouti. Kuunganishwa ka Kenya kwenye mission hiyo kungemaanisha kuwa gharama ambazo zingetumika zingetolewa na wahisani wa kimataifa na sio bajeti ya serikali ya Kenya.
4. The Somali Connection
Pamoja na kuwa mwanzoni raisi Mwai Kibaki alisita kukubali kupeleka jeshi nchini Somalia. Ripoti zanasema kuwa alishawishiwa na viongozi wa juu wakiwemo Minister of Internal Security (George Saitoti), Minister of Defense (Yusuf Haji), Mkuu wa Majeshi (Julius Karangi) na Chief of Intelligence (Michael Gichangi).
Yusuf Haji (Waziri wa Ulinzi), mwenye asili ya Somalia, inasemekana ndiye aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa raisi Kibaki. Ikumbukwe kuwa huyu Haji alikuwa anaunga mkono juhudi za kuundwa kwa Jubaland (independent state) ndani ya Somalia karibu na mipaka ya Kenya. Jubaland inajulikana kwa kuwa na wingi wa gas and oil deposits.
Huyu Haji ikumbukwe pia kuwa alikua na matamanio ya kuunganisha ukoo wake wa Ogadeni ambao umesambaa Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Ethiopia na Somalia.
Davidi Throup ambaye ni mchambuzi wa siasa za Kenya aliwahi kunukuliwa akisema.....
"Maslahi binafsi ya kiuchumi na kisiasa ya viongozi wa ngazi za juu na wanajeshi kutoka Kaskazini Mashariki mwa Kenya (Ogadeni Somali Community) vilichangia kwa kiasi kikubwa katika maamuzi ya kupeleka KDF Somalia."
5. Sababu nyingine ni nia ya serikali kuendelea kupata misaada kutoka mataifa ya Magharibi (USA to be precise). Baada ya balozi ya US kulipuliwa mwaka 1998 nchini Kenya, USA wali consider Kenya kama strategic ally katika kupambana na ugaidi.
Hivyo basi Kenya walihitaji kulinda reputation yao kwa kuunga mkono juhudi za USA katika kupambana na ugaidi, hakukuwa na njia zaidi ya kuingia Somalia kupambana na adui.
MATOKEO
Miaka takribani nane sasa tokea Kenya kuingia Somalia bado majeshi ya KDF yapo Somalia na bado Al Shabaab wanaendelea kuwa tishio kwa serikali ya Kenya.
Tunaweza kukumbuka matukio kadhaa ya kigaidi nchini Kenya yaliyoanza kutekelezwa na Al Shabaab wiki kadhaa tu baada ya KDF kuingia Somalia. Kati ya hayo ni mashambulizi ya Mwaura's, Machakos Bus Terminal, E. A. Pentecostal Church na mengine countless ambayo ni small scale.
Matukio notable ni kama mashambulizi ya Westgate, Garrisa na hivi karibuni DusitD2 Hotel.
Kama sababu ya KDF kuingia Somalia ilikua ni kuifanya Kenya iwe salama dhidi ya Al Shabaab ili iweze kuvutia wawekezaji basi kwa asilimia kubwa mission ime-fail. Ingawa kuna foreign investors lakini kitendo cha kuendelea kuwepo Al Shabaab ndani ya Kenya na kuendelea kufanya mashambulizi kila watakapo ni ishara kuwa KDF imeshindwa.
Wanajeshi wanauwawa kila uchwao na wengine kuchukuliwa mateka na Al Shabaab. Raia wanauwawa kila Al Shabaab watakapotaka kuua. Somalia mpaka sasa hawajaweza kuwa na stable government. Hizo zote ni dalili za kushindwa. Nashauri serikali ya Kenya iondoe KDF Somalia kwa sasa ili mfanye evaluation kuona mmekosea wapi na nini way forward.
Natoa Credit kwa: The Conversation, CSIS, Crisisgroup, Wikileaks, Daily Nation.