mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Hivi hebu tujadili, je kenya iwarudishe wakimbizi zaidi ya laki tano kwao Somalia? Sehemu kubwa ya wakimbizi hao ni waislam ambao alshabab wanadai wanawalipizia kisasi, kisa ni kuwa wanadai majeshi ya kenya yanaua waislam huko Somalia. Kinachonishangaza ni kuwa hao wanaotetewa na alshabab, walikimbilia kenya wakiwakimbia alshabab! Kama kenya ikiwafukuza halafu wakaenda kuuliwa na alshabab je kenya ilaumiwe? Je katika mazingira hayo wanaoshabikia alshabab kwa kisingizio cha dini watasemaje?