Kenya borrowed on average Sh129.5 billion per month in the last three months of the 2018/2019 fiscal year
www.businessdailyafrica.com
Deni la Kenya linazidi kuongezeka kwa kasi, hali hii inajitokeza wakati ambapo baadhi ya wakenya wanajisifu kukusanya pesa Mara mbili ya Tanzania. Jambo linaloshangaza ni kwamba, pamoja na majigambo ya kukusanya pesa nyingi, lakini GoK haina uwezo hata kulipa Madeni yake ya nyuma, hulazimika kukopa ili kulipa Madeni ya nyuma.
Pamoja na Kenya kukusanya pesa nyingi, na kukopa pesa nyingi kuliko nchi yoyote hapa EAC, lakini ni nchi ya mwisho katika kuwekeza katika miradi ya maendeleo, jambo hili limeifanya WB kuwa na wasiwasi juu ya uwezo wa Kenya kulipa Madeni yake kutokana na ukweli kwamba, pesa inayokopwa hutumika kulipia mishaara, kulipa Madeni na kugharimia shughuli za serikali ambazo ni kubwa kupita uwezo wa nchi.
Katika hali hii ni wazi kuwa "Future" ya Kenya kama nchi na maisha ya wakenya yapo mashakani, hasa ukizingatia kwamba sasa hivi Kenya inanunua zaidi kuliko inachokiuza katika nchi za Africa ambazo zilisaidia Sana kupunguza "Negative balance of trade " na nchi za Nje ya Afrika.