Kenya is broke, finally

Kwahiyo Unakubariana na Ndugai?
 
Kenya has been running a fake economy for far too long. Its outcome is only starting to catch up with them now.

Evonomic realignment must take place sooner rather than later.
Hapa Umemaliza Kila Kitu ndugu
 
Kweli maisha yanaenda kasi sana, kutoka kuwa Taifa kubwa Afrika Mashariki lililoongoza ile movement ya kujitenga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki hadi kupelekea kuvunjika miaka ile hadi kuwa Taifa la kushindwa kulipa watumishi Mishahara๐Ÿค”

Waswahili wanasema mwenzio akinyolewa zako tia maji.

Ni wakati wa Sisi Watanzania kujipanga, kama hakutakuwa na udhibiti wa fedha za Umma na watu kupiga cha Juu kama ile tenda ya SGR badala ya 660 Bilioni hadi 1.1Trilioni nasi tutafika huko.

Wananchi tuna nafasi ya Kuamua viongozi wa Adilifu 2025 kabla mambo hayajawa magumu zaidi.

Mungu awasaidie Wakenya kipindi hiki cha Ukata wanachopitia
 
Mkuu, tofauti kati ya Kenya na Tanzania ni kwamba, Tanzania tunajaribu Sana kuishi kulingana na uwezo wetu, hatujikwezi.

Kenya ni watu wa kujikweza na kuonekana wanauchumi mzuri. Serikali ya Kenya haina vipaumbele vya nchi, wao siasa, ukabila na "prestige" ndivyo vinavyoongoza maamuzi ya kiuchumi.

Hivi nchi masikini Kama Kenya itawezaje kulipa "salaries" hadi madiwani?, yaani karibia Kila mbunge anapewa ulinzi na serikali, nchi kuwa na wabunge wa kitaifa na bunge la "senate", gharama ya kuendesha serikali ya Kenya pekee ni zaidi ya pesa zote za maendeleo Kenya.
 
Swali zuri Sana kaka. Sijui sababu zilizosababisha reli Yao kushindwa kuendelea, lakini huku Tanzania sababu kubwa ni mabadiliko ya sera za uchumi na mabadiliko ya malengo.

TAZARA lengo la kujengwa kwake ilikua ni kuzisaidia nchi za kusini mwa Afrika kutotegemea bandari za Makaburu katika kuisafirisha mizigo yao, wengi walikua wanategemea bandari za Afrika kusini, kwahiyo kabla ya 1994, TAZARA ilikua ikipata mzigo mkubwa Sana, baada ya uhuru wa Afrika kusini, nchi nyingi ziliamua kupirishia mizigo yao huko, kwahiyo TAZARA ikaanza kuyumba Sana.

Reli ya kati tuliirithi kutoka kwa wakoloni, hatukua na utaalamu wowote wa kuiendesha, Kama utakumbuka viwanda na mashirika ya serikali karibu yote yalifilisika.

Hivi Sasa serikali inajaribu Sana kushirikisha "private sector" katika kuiendesha haya mashirika ya Imma Kama ilivyo "UDART", ni matumaini yangu hata hii SGR pia itakua hivyo.
 
Mkuu happy sawa ila hata hivyo wanajitahidi sana kumbuka wao hawana rasilimali vitu kama sisi na karibu nusu ya ardhi yao ni kame balaa lakini bado wamefurukuta imagine wangekuwa sisi wangekuwa wapi
 
yule jamaa anayedili na Russia yuko wapi?

Anapenda mambo ya umbea eti Russia hii vita akifikisha mwaka anafilisika. Wao vurugu zimetokea wiki tu hawana pesa ..
๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ oya
 
Mkuu happy sawa ila hata hivyo wanajitahidi sana kumbuka wao hawana rasilimali vitu kama sisi na karibu nusu ya ardhi yao ni kame balaa lakini bado wamefurukuta imagine wangekuwa sisi wangekuwa wapi
Bado ni kama kamari kutabiri kuwa wangekua njema kutokana na ukabila. Kenya hata hivyo walivyo leo wangeachana na ukabila toka zamani wangekua mbali. Wana ukabila wa kipumbavu moja ya element kuu ya akili mbovu ya mtu mweusi licha ya kuchapwa bakora na mzungu na kuletewa shule.
 
Only if EAC was Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC
 
Meanwhile riggy G, rutto and mudavadi each drew 1B KSH for private cars
 
Yawezekana ikawa hivyo ila kama kweli jamaa hawana hela za kulipa basi Ruto ana safari ngumu.

Na mzee RAO atacheza na hii issue hadi handshake au wafungue server!.

...
Anapenda mambo ya umbea eti Russia hii vita akifikisha mwaka anafilisika. Wao vurugu zimetokea wiki tu hawana pesa.
 
Naona tatizo mahali yaani ujenge reli kwa matrilioni halafu umuite mwekezaji kwa ajili ya kuisimamia tu ale hela...kwamba tumeshindwa kweli kuisimamia miradi yetu ikaleta faida? Kama ni hivyo hao wawekezaji nao ingepaswa wahusishwe kwenye ujenzi watie mzigo na sio kuja tushapigwa tozo mpk basi wao waanze kuuza tiketi.
Hivi ni kweli hatukuwa na utaalamu wa kuisimamia miradi yetu au watu waliinywa na kulindana kwingi?
 
Yaani huyo Gachagua ndio bure kabisa badala kutafuta solution anasingizia uhuru ..nchi za kiafrika tu a safari ndefu Sana wao posho za mabilioni na wake zao wanajipa ila wafanyakazi wengine hawajalipwa ...hii ni second time nchi Iko broke wanaelekea kubaya eti hawataki kukopa wanategemea makusanyo Hadi next week
 
Mkuu happy sawa ila hata hivyo wanajitahidi sana kumbuka wao hawana rasilimali vitu kama sisi na karibu nusu ya ardhi yao ni kame balaa lakini bado wamefurukuta imagine wangekuwa sisi wangekuwa wapi
Mkuu, wao hujisifia kuwa na "hard working and educated citizens, pia wanasema nchi yao Iko na uchumi mkubwa.

Siku hizi mambo muhimu yanayoitajika Ili nchi iweze kupata maendeleo kwa haraka ni
1)Educated human resource
2)Capital
3)Technology
Kenya huwa wanajisifu kuwa navyo vyote hivi, kwanini hawaendelei wanatoa kisingizio Cha kukosa Ardhi na rasilimali?.
Israel, Taiwan, Singapore, South Korea na Sychelles, wote hawana Ardhi Wala rasilimali yoyote, mbona wanaendelea kwa Kasi?
 
Mkuu, wakati tunapata uhuru kulikua na madaktari 3 na Engineer mmoja nchi nzima, tuliirithi bandari tatu, reli mbili ya Tanga - Moshi na Central corridor, kweli tungeweza kuiendesha wenyewe?.

Kuhusu kuendesha, itakua Kama "UDART", sio lazima kuendeshwa na wageni, inaendeshwa na watanzania lakini sio serikali. Kwa kufanya hivyo tunawapa watanzania ajira na uwezo wa kuendesha uchumi wao.

Mkuu, serikali haipaswi kufanya biashara, inapaswa ijenge miundombinu Ili wananchi wafanye biashara, serikali imejenga Barbara lakini raia ndio wenye magari yanayotumia hizo Barbara, hata reli ni hivyo hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ