Swali zuri Sana kaka. Sijui sababu zilizosababisha reli Yao kushindwa kuendelea, lakini huku Tanzania sababu kubwa ni mabadiliko ya sera za uchumi na mabadiliko ya malengo.
TAZARA lengo la kujengwa kwake ilikua ni kuzisaidia nchi za kusini mwa Afrika kutotegemea bandari za Makaburu katika kuisafirisha mizigo yao, wengi walikua wanategemea bandari za Afrika kusini, kwahiyo kabla ya 1994, TAZARA ilikua ikipata mzigo mkubwa Sana, baada ya uhuru wa Afrika kusini, nchi nyingi ziliamua kupirishia mizigo yao huko, kwahiyo TAZARA ikaanza kuyumba Sana.
Reli ya kati tuliirithi kutoka kwa wakoloni, hatukua na utaalamu wowote wa kuiendesha, Kama utakumbuka viwanda na mashirika ya serikali karibu yote yalifilisika.
Hivi Sasa serikali inajaribu Sana kushirikisha "private sector" katika kuiendesha haya mashirika ya Imma Kama ilivyo "UDART", ni matumaini yangu hata hii SGR pia itakua hivyo.