PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Very brainy inputs...Mapato yanakusanywa ila wanatumia zaidi ya 60% kulipa madeni ya nje na ndani. Kiuchumi ni bora ukose kulipa mishahara kuliko madeni kama bonds yafikie maturity alafu uingie mitini. Hapo unakuwa defaulted na unafeli vibaya mno na sarafu yako inashuka thamani haraka sana. Pia ni bora usilipe mishahara kuliko nchi ikose huduma za kijamii na kukosa kuagiza bidhaa muhimu. Nchi zetu za kimaskini hizi unakuta waajiriwa wa serikali ni kama 15% ya wananchi, na sio wote hawajalipwa. Sijui idadi ila utakuta wasiolipwa hawafiki 10% ya raia, sasa huwezi kufanya ukichaa kuacha hospitali hazina dawa eti ulipe mishahara yote. Hapo unatafuta priorities kama hela haitoshi.
Kenya tangu wapate uhuru hawakuwahi kosa kulipa mshahara, na watalipa mishahara hii kwa makusanyo ya kodi yanayofuata. Ila wanatakiwa wapunguze matumizi, Kenya ina matumizi makubwa sana ya serikali. Na wapambane na ufisadi.
Tatizo lingine ni miradi isiyozalisha na mikopo mikubwa mikubwa inayofuatana. Haya mambo ya kukopa kwa pamoja ujenge SGR, barabara, ndege na vitu visivyozalisha direct itatufikisha uko. Mfano trilioni za SGR tutazilipa kwa hela hii hii tunayomkamua muuza mkaa. Wakati nchi zenye akili zinakopa zijenge viwanda zizalishe bidhaa faida ndio ilipe mkopo na riba yake. Au basi tukope hela tuanzishe miradi mikubwa ya kilimo. Kwani trilioni ngapi zinahitajika kufunga mifumo ya umwagiliaji watu wakalima mwaka mzima, tena hii inagusa almost kila Mtanzania na faida yake inaanza kurudi mwaka uleule mfumo umeanza.
Tunatumia trilioni 14 kujenga SGR ambayo inabeba watu zaidi kuliko mizigo. Hii sio India au China ya watu zaidi ya bilioni moja. Tumenunua ndege kwa hela nyingi ambavyo Air Tanzania haitokaa ipate faida. Baada ya hapo tubangaize na makusanyo ya PAYE na VAT kulipa mikopo.