Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Nairobi, Kenya. Ilikuwa patashika katika Kijiji cha Godmiaha, Homabay nchini Kenya baada ya mwanamume mmoja aliyeaminika kufariki dunia kuibuka nyumbani na kukuta msiba wake ukiendelea.
Kenneth Olwa, anadaiwa kuondoka nyumbani kwao karibu miaka 20 iliyopita na baadaye kutajwa amefariki dunia, aliibuka mbele ya waombolezaji waliokuwa kwenye msiba wake nyumbani kwa wazazi wake.
Kwa mujibu wa gazeti la The Daily Nation la Kenya, inaaminika Olwa alipoondoka nyumbani alikwenda katika mji wa Mbita na kuanza shughuli za uvuvi.
Baadaye alihamia katika eneo la Alum, kwenye ufukwe wa Ziwa Victoria.
Kiongozi wa kitongoji cha Ramba, Joseph Ndege, familia ya Olwa ilifahamishwa kwamba kijana wao alikuwa amefariki dunia baada ya kuugua.
Pia familia ilielezwa kuwa polisi waliuchukua mwili wa Olwa na kwenda kuuhifadhi katika mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Homa Bay.
“Wanafamilia hawakupoteza muda; papo hapo walianza kuandaa taratibu za maziko. Baadhi yao walikwenda hospitali ya Homa Bay kuthibitisha kama mwili uliopelekwa na polisi ulikuwa wa kijana wao,” alisema Ndege.
Familia pia ilikwenda kutoa tangazo la kifo kwenye redio na walitumia kiasi fulani cha fedha kununua vyakumba kwa ajili ya waombolezaji na maandalizi mengine ya msiba.
Hayo yakiendelea, Olwa alikuwa anasikiliza redio wakati anaendelea na shughuli zake za uvuvi, akasikia amefariki dunia kwa ugonjwa ambayo haijafahamika.
Baada ya kusikia hivyo, akawapigia simu baadhi ya ndugu zake na kuwataka waache mipango yote ya mazishi. Baadhi ya wanandugu walitumwa alipokuwa kuthibitisha anachokieleza,” alisema Ndege.
Hata hivyo, mipango ya mazishi iliendelea kwa kuwa baadhi ya ndugu hawakuamini ujumbe wa simu, hasa kwa kuwa Olwa aliondoka miaka 20 iliyopita na hakuwahi hawakuwahi kusikia sauti yake.
Mwili ulioaminika ni wa Olwa ulikuwa umechukuliwa tangu Ijumaa kwa ajili ya maziko Jumamosi mchana.
Lakini wakati shughuli za msiba zikiendelea nyumbani, baadhi ya ndugu walikutana na Olwa. Waliporejea wakiwa pamoja naye, walikuta hotuba mbalimbali za kumuaga marehemu zikiendelea, muda mfupi kabla ya kuzika.
Olwa aliwahakikishia ndugu na jamaa waliokusanyika kwenye msiba kuwa alikuwa bado hai na wasiogope.
Familia ililazimika kurejesha mwili waliotaka kuuzika mochwari kwa akuwa hakuna mwingine anayedai kuutambua.