Kenya: KEMSA yashutumiwa kufanya ununuzi wa vifaa kinga dhidi ya Corona kwa mara mbili ya bei halisi

Kenya: KEMSA yashutumiwa kufanya ununuzi wa vifaa kinga dhidi ya Corona kwa mara mbili ya bei halisi

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
logo.jpg


Kenya Medical Supply (KEMSA) ambayo inahusika na ununuzi wa dawa na vifaa tiba kwa vituo vyote vya Afya vilivyopo Kenya imeingia katika kashfa nyingine kutokana na ununuzi wa vifaa vya dharura dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Taarifa zinasema vifaa hivyo vilinunuliwa kwa gharama ya juu sana kulinganisha na bei halisi iliyopo sokoni kama iliyoainishwa kwenye jedwali hapo chini.

KIFAA
IDADI
BEI YASOKO (Ksh)
BEI ILIYONUNULIWA (Ksh)
N95 Masks
5000​
700​
1300​
KN95 Masks
1,836,400​
450​
700​
Disposable surgical masks
(Haijawekwa wazi)​
90​
50​
PPE
(Haijawekwa wazi)​
4500​
9000​


Hata hivyo mkurugenzi wa KEMSA Jonnah Manjari Mwangi alisema kuwa wamenunua kwa bei ya juu zaidi ili kuhakikisha wanapita vifaa vyenye ubora zaidi, kauli hiyo inakuja baada ya wahudumu wa afya kuishutumu serikali kuwapatia vifaa visivyo na ubora wa kuridhisha. Mpaka tarehe 17/07/2020 jumla ya wahudumu 429 katika vituo vya afya wamethibitika kupata maambukizi ya virusi vya corona, ambapo wahudumu wanne (4) (Madaktari 2, Nesi 2) wameshapoteza uhai kwa ugonjwa wa Covid-19.

Source: Revealed: Kemsa procures PPEs at double market price
 
Hiyo nchi imekua Kama danguro..kila mtu anaingia na kutoka. Ndiyo maana corona haiishi..kumbe inawapa watu ulaji
 
Back
Top Bottom