John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Francis Atwoli
Katibu wa Muungano wa Wafanyakazi (COTU), Francis Atwoli ameikosoa Serikali ya Kenya kwa kutokuwa na nguvu katika suala la Wakenya kufanyishwa kazi katika Nchi za Mashariki ya Kati.
Atwoli amewajia juu Waziri wa Kazi na Waziri wa Masuala ya Kigeni kwa kushindwa kushughulikiwa tatizo la vifo vingi vya Wakenya hasa wasichana ambao wanasafiri kwenda Uarabuni kutafuta maisha.
Akizungumza na wadau wa COTU Jijini Nairobi, Atwoli ameikosoa Serikali ya Kenya kwa kupuuzia haki za raia wao nje ya nchi hiyo licha ya matukio ya kupoteza wapenda wao mara kadhaa katika hali isiyoeleweka.
“Nafikiri Serikali haipo makini na kinachoendelea katika dunia ya Kiarabu, Qatar, Bahrain na nyinginezo, nawasisitiza muache kupeleka wasichana wenu huko.
“Kila siku asubuhi Qatar Airlines na nyingine zinashusha miili ya Wakenya kwenye Uwanja wa Ndege wa JKIA. Hatuwezi kuona hili ni tatizo na tukabuni sheria ya kuwalinda vijana wadogo?”
Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na malalamiko mengi ya Wakenya kudhalilishwa na kukutana na mazingira magumu ya kazi katika Nchi za Saudi Arabia, Qatar na Bahrain.
Source: Citizen Digital