KENYA: Koffi Olomide ampiga mateke mnenguaji wa kike baada ya kutua jijini Nairobi

Duh exotic news.
 
Safi sana, udhalilishaji huu usipewe nafasi hata chembe. Kama anaweza kumpiga teke hadharani bila shaka kama hawako hadharani huwafanyia udhalilishaji wa hali ya juu. Hongera sana Polisi Kenya.

Tayari usiku huu yupo chini ya ulinzi na amepigwa muhuri mwekundu...hatoingia tena Kenya
Bravo Kenya
 
Kilichotokea ni madhara ya bosi kuwa na mahusiano na mfanyakazi wake na hatimaye kuoa mfanyakazi huyo na kumuacha akiendelea kufanya kazi ofisi hiyo hiyo na wafanyakazi wenzake wale wale.....
Chanzo cha Ugomvi kimeanzia mbali sana hata kabla hawajatua Kenya na aliyesababisha sekeseke lile litokee ni mrembo Cindy ambae Alikuwa ni mcheza shoo wa Koffi akaja akawa mpenzi wake na hatimaye mkewe.....

Baada ya Cindy kuwa mke wa Koffi hali kwenye band ilibadilika....Cindy alipandishwa cheo na kuwa kiongozi wa choreography ambaye Alikuwa na jukumu la kuongoza mazoezi ya kudance kubuni staili mbalimbali na mitindo kadha wa kadha ya kudance...Hilo halikuwapendeza waliokuwa wacheza shoo wenzake waliokuwa wanaamini nafasi aliyopewa hakustahili hata kama ni mke wa bosi kwani kulikuwa na wacheza shoo kibao wenye uwezo kumzidi na wazoefu na wako kwenye kundi kwa muda mrefu kuliko yeye,hao ndo wangepaswa kupewa nafasi hiyo...
Hali hiyo ikazua bifu kati ya Cindy na madensa hao wengine hususani wa kike...Sasaaaa Cindy hutumia madaraka yake kuwaadhibu hao mahasimu wake na huwaadhibu kwa kutowajumuisha kwenye tripu za kusafiri nje ya nchi.....

Kwenye safari ya kuja Kenya kuna madada hatari sana na wakali wa kudance waliachwa kitendo kilichowakera dancers wengine akiwemo Pamela yule aliyepigwa teke.....Pamela yeye bwana ni mropokaji hasa na hakusita kuzinguana na Cindy .......

Pale airport sasaaaaa Cindy si akamfuata Pamela na kumuambia amsaidie kubeba begi, Pamela akachomoa kisha akamuongelea shombo Cindy na si unajua wale wanawake tena,basi walirushiana maneno kiasi cha kuchapana makofi,hali iliyofanya Koffi afikishiwe taarifa......
Uamuzi wa Koffi ulikuwa mmoja tu,kumfuata Pamela kumsema na inasemekana Pamela aliambiwa baada ya kumalizika kwa tamasha lile yeye kazi basi.....Kama kawaida Pamela hakai na neno kifuani akaongea mbovu kwa Koffi....Unajua kilichofuata...
NDO LILE TEKE.....

KWAHIYO UKIANGALIA NA KUFUATILIA KWA MAKINI SANA TATIZO NI HILO KUJIHUSISHA NA MAPENZI NA MFANYAKAZI WAKO,UNAMPA CHEO ILI AWAONGOZE WALE WALE ALIOKUWA ANAFANYA NAO KAZI LINE MOJA,WENGINE WAKO JUU YAKE NA WENGINE WAKO CHINI YAKE....

NI JAMBO LA KAWAIDA KUWA KUNA WAFANYAKAZI WENZIE WALIKUWA WAKIMZIDI SANA KIUTENDAJI JE UNADHANI WATARIDHIKA????
NI KAWAIDA KUWA WATAKUWA NA KINYONGO NA MAMBO KAMA TAFRANI LAZIMA ZITATOKEA....
 
Hatimaye Kofi akamatwa na kusekwa lock up.
Famous Congolese singer Koffi Olomide
has been arrested on Friday night in
Kenya’s capital Nairobi after he was
caught on camera in the afternoon
kicking one of his dancers on arrival at
the airport.
The 59-year-old singer, who was
scheduled to hold a concert in Nairobi,
was arrested in front of television
cameras outside the premises of a
television station where he was granting
an interview.
 
Hasira ni moja ya mapungufu yetu......lakini kuacha hasira zikutawale na kukusababishia matatizo ni utashi wako.....
Lazima tujifunze namna ya kupokea mambo yenye mitazamo tofauti na sisi kwani tunaishi katika ya watu tuliokinzana katika mambo mengi tu......
Kuvumiliana kama wanajamii katika mambo mbali mbali ya kijamii ni nguzo kubwa ya umoja na amani miongoni mwetu......

Lazima tujue kuwa tunaishi na watu au kujumuika na watu wenye mitazamo na maoni tofauti na sisi....haijalishi iwe mitazamo chanya au hasi kwani hata sisi wenyewe sio watu wote hupendezwa na maoni yetu au mitazamo yetu.....na baadhi yao hutuambia ukweli tujirekebishe na wengine hutuacha tukipotea.....

Kitendo cha huyo Mwanamuziki mkongwe kufanya tukio hilo kimezusha maswali mengi yasiyo na majibu katika vichwa vya wastaarabu na waungwana.......bado nina amini yeye kama kiongozi wa kundi hilo kuna utaratibu maalumu wa kuwawajibisha wale wanaokwenda kinyume cha mstari kwani ni dhahiri kuwa kuna sheria zimewekwa kwa ajili ya kushughulikia masuala kama hayo......

Maamuzi aliyoyafanya ni moja ya maamuzi ya kipuuzi kupata kuyashuhudia....matukio kama hayo tumezoea kuyaona kwa vijana wanaotumia mihadarati lakini si kwa mtu mstaarabu kama huyo Koffi......maaana katika akili ya kawaida unawezaje kufanya alichokifanya huyo jamaa....??!!

Hii pia inaonyesha ndivyo pia yanavyotokea hata kwenye makundi mengine ya muziki na si wote wanaotendewa hayo wana jeuri ya kuwasemea maboss wao.......

Kwa sababu haya mambo yamefanyika katika nchi yenye utawala wa sheria...naamini hatua zaidi zitachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine wote wenye tabia kama hizo.....
 
Hiyo ni mbinu tu ya kujaza show hamna kitu
 
Power of Kenyan sociak Media #Justice served.

I am just thinking if this happened in TZ....would justice...
 
Swali lako ni la hovyo kabisa. Ulitaka teke limfikie ndio aitwe abuser! By the way, kitendo cha kuonyesha hasira na kusudio la kumpigia teke hilo linatosha kudhibitisha kuwa huyu jamaa hathamini wanawake. Wakenya hawanabudi kuboycort show zake
Post yako ni ya hovyo kabisa. Ulitaka niandike lile unalolifikiria wewe?. By the way, kila mtu ana mlengo wake katika hili suala. You have your point I got mine.
 
Sometimes mwanamke anaweza kukuudhi kiasi kwamba ukajikuta kofi limeshatoka tu kumshikisha adabu..... Hawa viumbe waache tu jinsi walivyo. Simtetei Koffii ila hawa viumbe ni wa ajabu sana na mwanaume usipokuwa nao makini utajikuta pabaya sana
 
Inasemekana eti ilikuwa ni katika kuwaprotect dancers wake kutoka kwa watu waliokuwa wanawazonga - kwamba teke lilikuwa limeelekezwa kwa mtu mwingine. All in all, nadhani hiyo ni kazi ya wale walinzi wake.
 
Inasemekana eti ilikuwa ni katika kuwaprotect dancers wake kutoka kwa watu waliokuwa wanawazonga - kwamba teke lilikuwa limeelekezwa kwa mtu mwingine. All in all, nadhani hiyo ni kazi ya wale walinzi wake.
Aah wapi, kama ingekuwa hivyo angewaambia Police wafanye hiyo kazi. Huyu jamaa mjinga sana, angekuwa West mara moja angerudishwa na asikanyage tena.

Ukiwa Mtu unayeheshimika unatakiwa uwe na uwezo wa kudhibiti hasira.
 
K
Usimtazame mwanamke kwa ukatili,
Mwanamke anatakiwa kuonewa huruma,
Mi nikikukuta unampiga mwanamke hata kama ndo ulikuwa unamrudishia baada ya yeye kukubonda na kitu.... ntakumaindi wewe , nitamsaidia mwanamke.
Komenti za kujipendekeza kwa wanawake kama hizi unatakiwa kuzitoa kwenye blogu ya mange kimambi na sio hapa jf
 
Post yako ni ya hovyo kabisa. Ulitaka niandike lile unalolifikiria wewe?. By the way, kila mtu ana mlengo wake katika hili suala. You have your point I got mine.


Mkuu linapokuja swala la haki hakuna mawazo au mlengo wako na wa mwingine. Kupiga wanawake ni kinyume cha haki na sheria sasa huwezi kutwambia eti ni mtazamo wako binafsi tukakielewa, hayo mawazo yako yamepitwa na wakati. Ni sawa na mtu anaeshabikia ubaguzi halafu atuambie ni mtazamo wake tu, NO!
Acheni kupiga wanawake. Hakuna kitu chochote kinachofanya mwanaume awe juu zaidi ya mwanamke kwenye jamii. Acheni mawazo ya kikoloni.
 
K

Komenti za kujipendekeza kwa wanawake kama hizi unatakiwa kuzitoa kwenye blogu ya mange kimambi na sio hapa jf


Hapa JF ndio mahali pake, watu wenye busara wapo wengi humu. Ni wapuuzi wachache tu ndio wanang'ang'ania wanamamlaka ya kuwapiga wanawake kisa tu ni wanawake. Mwanaume aliyekamilika hawezi kumpiga mwanamke hata siku moja.
 
We ulieleta taarifa hii ni mbea sana,hao maofisa waliokuja kumzia hapo hukuwaona?au una macho ya dj
Kazi ya polisi ni kumbembeleza mtuhumiwaa ..... Au kumchukulia hatua kwa kosa alilofanya?
 
Huyu Koffi sijui vwipi....ye hakuona Jay z alivyotulia wakati ule anapewa kipondo....mwanamuke hapigwi ati.
 
Hapa JF ndio mahali pake, watu wenye busara wapo wengi humu. Ni wapuuzi wachache tu ndio wanang'ang'ania wanamamlaka ya kuwapiga wanawake kisa tu ni wanawake. Mwanaume aliyekamilika hawezi kumpiga mwanamke hata siku moja.
.....yani we jamaa ni bonge la kuzi.,hujijui tu!
...eti mwanaume aliekamilika hawezi kufanya nini......?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…