Kenya kuna Power Vacuum!

Kenya kuna Power Vacuum!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Nimegundua kwamba Kenya kuna power vacuum kubwa sana, kwa maana kwa mara ya kwanza Wakenya wamekuwa obsessed sana na uchaguzi wa TanZania.

Nilifikiri ni jambo la kawaida wakati wa kampeni za Uchaguzi, lakini cha kushangaza hata baada ya Magufuli kuapishwa kuwa Raisi wetu bado wako obsessed naye na wanafwatilia kila move anayofanya na wanatamani hata wangepata Rais kama Magufuli.

Sasa hii ni ishara mbaya kwa nchi ya Kenya, inaonyesha kwamba Wananchi wa nchi hiyo wamepoteza imani na Serikali yao na hawana cha kujivunia na ndiyo maana wanaona angalau wafwatile Rais wetu anafanya nini na anaongozaje!
 
Natanguliza salamu, na nikukosoe, japo kidogo, kwa kutumia neno obsessed kwenye post yako, tulifurahishwa jinsi mlivyojitokeza na kupiga kura kwa amani na jinsi raisi Magufuli hit the road running akaonyesha tofauti kati yake na aliyekuwa rais hapo awali.

Mimi kama Mkenya, na ndugu zangu wengi hapa, huwa tunafwatilia kwa makini matukio mengi ya Tanzania, siasa ikiwa mojawapo, so tukiona jambo zuri kama raisi mpya alivyo bana mawaziri kusafiri nje na impromptu appearance ministry of Finance Ijumaa, huwa tunapost twitter na mitandao ya kijamii kuonyesha kuwa tunataka a pro active president, tunataka iwe changamoto kwake na viongozi wengine.

Hapo hakuna obsession, tumefurahishwa na matukio yaliotendeka tangia mpige kura.
 
hey pal...ryt now we have problems of our own to deal with.I don't know where you got that idea of obsession from but the truth of the matter is that we really don't give a damn about what's happening in tz
 
hey pal...ryt now we have problems of our own to deal with.I don't know where you got that idea of obsession from but the truth of the matter is that we really don't give a damn about what's happening in tz

Your fellow Kenyan just confessed.
 
Mkuu Smatta kuna wakati mwingine uko pouwa sana hii ni moja ya post yako yenye majibu maziri yasiyo na makando kando.


Natanguliza salamu, na nikukosoe, japo kidogo, kwa kutumia neno obsessed kwenye post yako, tulifurahishwa jinsi mlivyojitokeza na kupiga kura kwa amani na jinsi raisi Magufuli hit the road running akaonyesha tofauti kati yake na aliyekuwa rais hapo awali. Mimi kama Mkenya, na ndugu zangu wengi hapa, huwa tunafwatilia kwa makini matukio mengi ya Tanzania, siasa ikiwa mojawapo, so tukiona jambo zuri kama raisi mpya alivyo bana mawaziri kusafiri nje na impromptu appearance ministry of Finance Ijumaa, huwa tunapost twitter na mitandao ya kijamii kuonyesha kuwa tunataka a pro active president, tunataka iwe changamoto kwake na viongozi wengine. Hapo hakuna obsession, tumefurahishwa na matukio yaliotendeka tangia mpige kura.
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada inakaa anapenda kuishi humu jf anadhani kila mkenya anafatilia mambo ya tz.Ukiongea na wakenya humu mitaani wengi wao hata hawajui mlikuwa na uchaguzi,na wale wanaojua hawajui ata wagombeaji walikuwa akina nani.Nyie ndo mko 'obsessed' yaani ata za waziri Waiguru mnajua za makamu rais Ruto mnaongelea kama 'maexpert' maanake kawaida yenu ni udaku mchana hadi jioni.Uliza mkenya mmoja akutajie hata waziri mmoja wa serikali ya kikwete au hata waziri mkuu,hawajali ya kwenu maanake hayana mshiko na wako 'busy' na maisha yao.
 
haukumuelewa cz amesema the word obsession is misplaced which I totally agree.alafu ii ya power vacuum nayo ndo kaaribu kabisa

Obsession na power vacuum maneno mawili pekee ya kiingereza ambayo mleta mada anayajua haijalishi kama haelewi maana ya maneno hayo.Ni kimombo!
 
Mkuu Smatta kuna wakati mwingine uko pouwa sana hii ni moja ya post yako yenye majibu maziri yasiyo na makando kando.

mkuu, wakati wote huwa najaribu kuwa mstaarabu labda kama mada ni ya kikatili hapo na kunja shati na kuburuzana tu.
 
Si kweli kwamba WaKenya pekee ndio wanafuatilia matukio ya kisiasa Tanzania. Binafsi mbona ni mfuatiliaji wa karibu sana wa siasa na matukio ya nchi karibia zote za EAC. Na hapa na nazungumzia 'in daily basis' kwa kupitia magazeti yao, redio zao, na hata mitandao yao ya kijamii.
Hivyo naamini bado kuna waTanzania wengi wenye weledi wa kawaida ambao nao ni wafuatiliaji wa mambo katika nchi jirani. Na hawafanyi hivyo kwa kuwa wako 'obessed' na nchi hizo hapana, bali kufuatilia kwao kwa karibu tu kuwa dunia inakwendaje katika siku husika.

Mwisho, pengine jambo la msingi tu ambalo nimeliona ni kuwa WaTanzania wengi ni watu wavivu (au tusiokuwa na utamaduni) wa kujishughulisha kujua yanayoendelea katika nchi za majirani zetu. Tumezoea ile kasumba ya kijamaa ya kulishwa propaganda kwenye kila jambo hata pale ambao tunaweza kujifunza vitu vido vidogo wenyewe kwa kuona. WaTanzania ni wazoefu wa kufuatilia habari za vilabu vya mipira nchi za kigeni tu kama Chelesea, ManU, etc na safu nzima ya majina ya wachezaji lakini si katika mambo makini yenye kuathiri maisha yao kwa ukaribu.
 
Its only one month na Kenyans will forget even the name mugufuli, I think the reason as to why our media is following this is to see what will happen since your opposition leader said elections were not fair
 
Back
Top Bottom