real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
KENYA: Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira, imepanga kufungia matumizi ya chupa za plastiki mwaka huu.
Sababu za kufungia ni kutokana na madhara ya chupa hizo katika mazingira kama ilivyo mifuko ya plastiki ambayo ilifungiwa mwaka jana
Mwenyekiti wa bodi hiyo amewapa washikadau hadi tarehe 30 Aprili kukubaliana na maelekezo yatakayoweka mkondo wa kuanza kwa marufuku hiyo
Kenya ilipiga matumizi ya mifuko ya plastiki mwaka jana na imesema itafungia masoko ambayo bado mifuko hiyo inaendelea kutumika
Moja ya wadau waliotoa dukuduku lao ni kampuni ya Coca cola imeomba kuahirishwa utekelezaji wa marufuku hiyo na kusema wapo katika mpango wa kuazisha kiwanda kitakachokuwa kinachakata chupa hizo kwa ajili ya kutumika tena