Kenya: Magoha aishauri Serikali kufunga tovuti za Ngono kuokoa Vijana

Kenya: Magoha aishauri Serikali kufunga tovuti za Ngono kuokoa Vijana

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Katibu wa Baraza la Mawaziri upande wa Elimu anaye maliza muda wake George Magoha ameishauri Serikali kuzifungia tovuti zote zinazo jihusisha na maudhui ya ngono nchini Kenya ili kuwanusuru vijana hasa wanafunzi dhidi ya athari hasi za tovuti hizo.

Amebainisha kuwa pamoja na kuwa dunia inafurahia uhuru wa mambo mengi, ikiwemo matumizi ya internet katika kufanikisha mambo mbalimbali, tovuti za ngono zinapaswa kufutwa, na ingefaa zaidi kama zingekuwa zimeondolewa haraka iwezekanavyo.

Amesisitiza kuwa hajali kama ataitwa dikteta kwa kutoa hoja hii na ameiomba Serikali mpya kulinda uhai wa taifa la Kesho nchini humo kwa kufanya jambo hilo haraka.

“Nilipo zungumza jambo hili kwa mara ya kwanza niliitwa dikteta. Binafsi sijali, linapokuja swala la maudhui ya ponografia ni bora waendelee kuniita hivyo”

Magoha au maarufu zaidi kama “mtu asiyependa mambo ya kipuuzi” amenukuliwa akisema kuwa kuingilia uhuru huo unaolenga kulinda maslahi ya watoto siyo udikteta, bali ni uwajibikaji wenye tija.

K24 TV
 
Hii nchi waliona tatizo kubwa ni izo web wakatubania.
 
Back
Top Bottom