Kenya: Mahakama ya Juu kutoa Uamuzi leo, Uhuru Kenyatta au Raila Odinga

Kenya: Mahakama ya Juu kutoa Uamuzi leo, Uhuru Kenyatta au Raila Odinga

Status
Not open for further replies.

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Leo Mahakama ya juu kabisa nchini Kenya inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya uchaguzi wa urais.

Kesi hii imekuwa ikisikilizwa tangu mwanzoni mwa wiki na jopo la majaji 7.

Kesi hii ilifunguliwa na wanasiasa wa Muungano wa Upinzani NASA, wakidai kuwa ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta ulitokana na hila zilizofanywa kupitia mfumo wa Computer wa Tume huru ya uchaguzi IEBC na wanataka matokeo hayo yafutwe na uchaguzi kuitishwa upya ndani ya siku 60.

Kwa upande wa pili tume ya uchaguzi IEBC na mawakili wa chama cha Jubilee wanasisitiza hakuna ushahidi wa kuyafutilia mbali matokeo ya uchaguzi yaliyompa Rais Uhuru Kenyatta ushindi.

======== ======== =========

Update;

==>Ulinzi mkali nje ya Mahakama ya Juu Nairobi, huku kukutarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais muda mfupi kuanzia sasa
4eb50f63e5fc8b9c46d21371b6850087.jpg
f0b6371d6687acc10cf7b8759a3bc840.jpg
fd16037538b2e5e061e84fc9a1f613c7.jpg


==>Odinga awasili mahakamani akiambatana viongozi wenzako wa NASA
 
NASA wakichomoka hapo kwa kukubaliwa madai yao, nitakubali Kenya kwa demokrasia wako mbele
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom