Kenya: Mchungaji Ng’ang’a azua gumzo kwa kuuza Mikate na Maandazi kwa bei ya juu, isiyo ya kawaida Kanisani

Kenya: Mchungaji Ng’ang’a azua gumzo kwa kuuza Mikate na Maandazi kwa bei ya juu, isiyo ya kawaida Kanisani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mchungaji James Ng’ang’a, mwanzilishi wa Neno Evangelism Centre, ameendelea kuzua mjadala kwa hatua yake ya hivi karibuni ambayo imewashangaza wengi.

Katika ibada ya hivi karibuni, mhubiri huyo wa injili aliamua kuuza mikate na mandazi kwa waumini wake kwa bei ya juu isiyo ya kawaida.

Mkate mmoja uliuzwa kwa KSh 200 (TZS 3838.96), huku mandazi yakiuzwa kwa KSh 100 (TZS 1919.48) kila moja. Kwa mtindo wake wa kawaida wa kuvutia, Mchungaji Ng’ang’a alitangaza bidhaa hizo kwa shauku kubwa.

"Mliskia kuna mikate leo eeh? Mkate moja ni 200 na maandazi ni 100. Kama unataka, leta KSh 200 nauza, customer customer, na hakuna change." alitangaza kwa msisitizo.
 
Naamini kabisa kwamba hiyo mikate na maandazi yaliisha
 
Naamini kabisa kwamba hiyo mikate na maandazi yaliisha
Mikate ya fundraising hiyo imebarikiwa, waumini wanainunua bila kulazimishwa.

Haki ya kuabudu watu wanavyotaka ni haki ya msingi ya kikatiba na kibinadamu.

Kuna watu wanatoa pesa kanisani bila hata kupewa mkate.

Muacheni Mchungaji atimize haki yake ya kikatiba na kibinadamu kufanya ibada anavyotaka.

Niko hapa kutetea haki za kikatiba na kibinadamu za kila mtu kuabudu anavyotaka ilimradi hajalazimisha mtu kumfuata.
 
Back
Top Bottom