Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Wakaazi wa kijiji cha Mutiribu, kaunti ya Meru walipigia simu Huduma ya Wanyama Pori KWS kuja kumnasa ‘simba’ aliyekuwa amejificha kichakani karibu na makazi yao
Ila maafisa hao walipofika mahali hapo waligundua kuwa ‘simba’ huyo alikuwa ni mfuko wa Supermarket ya Carrefour.
=========
Wakaazi wa kijiji cha Kinyana, taarifa ya ndogo ya Nkunjumu , Kiangua yapata kilomita 30 kutoka mji wa Meru nchini Kenya walipigwa na butwaa baada ya kumpata ‘simba’ aliyejificha karibu na maakazi yao.
Chifu wa eneo hilo Cyrus Mbijiwe alimwambia mwandishi wa BBC Peter Mwai kwamba mmiliki wa nyumba aliyeonekana simba huyo aliyejificha alikuwa amewasili na mfuko uliokuwa umebeba maparachichi baada ya kuhudhuria mafunzo katika kaunti ya Murang'a iliopo umbali wa kilomita 140.
Alipowasili nyumbani, aliamua kuweka mbegu za maparachichi hayo katikati ya nyumba yake na maua - mahali ambapo zingekauka.
Siku ya Jumatano wiki hii , mfanyakazi wa shambani ambaye alikuwa anatoka kuvuna nyasi za mifugo, aligundua kile alichodai kilikuwa simba na hivyobasi kupiga kamsa.
Wakaazi walikongamana katika eneo hilo ili kujionea kile kilichokuwa kikifanyika kwa umbali huku kila mtu akithibitisha alikuwa simba kwasababu hakuna aliyeweza kujongea eneo hilo.
''Niliwasili nikaona kitu kama simba ijapokuwa nilikuwa na wasiwasi'', alisema.
Maafisa wa shirika la wanyamapori waliwasili katika eneo hilo.
Mmiliki wa nyumba hiyo aliyekuwa mbali alipigiwa simu na wakati alipowasili alitakiwa kufungua mlango wa nyumba yake .
Mfuko wa plastiki ulikuwa chini ya dirisha la nyumba na ulipofunguliwa, ndio wakati walipogundua kwamba kile walichodhania kuwa simba hakikuwa na mwili. Ulikuwa mfuko wa plastiki!.
Haijulikani ni kwanini mfanyakazi huyo wa shambani hakuugundua mfuko huo kwa muda wa wiki moja ukiwa eneo hilo.
Eneo ambalo kisa hicho kilitokea lipo kilomita moja kutoka mbuga ya Wanyama pori ya Mlima Kenya.
Lakini Mbijiwe anasema kwamba hakuna simba aliyeonekana katika eneo hilo katika siku za hivi karibuni licha ya wakaazi kulalamikia kutoweka kwa mifugo yao.
Chanzo: BBC