KENYA: Miss ahukumiwa kifo

KENYA: Miss ahukumiwa kifo

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Malkia wa urembo katika gereza kuu la wanawake la Lang'ata jijini Nairobi amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na kosa la kumuua mpenzi wake kwa kumchoma kisu mara 22.

Miss huyo aliyefahamika kwa jina la Ruth Wanjiku Kamande amekutwa na kosa la kumuua mpenzi wake Farid Mohammed katika mtaa wa Buruburu, Nairobi Septemba 20,2015.

Jaji Jessie Lessit amesema upande wa mashtaka umedhibitisha kesi hiyo ya mauaji bila shaka yoyote.
Jaji huyo amesema hukumu hiyo inatakiwa kuwa funzo kwa vijana wajue kwamba ‘’si vyema kumuua mpenzi wako, ni vyema ukaamua kuondoka zako."

Wakili wake Joyner Okonjo amesema mfungwa huyo alikuwa amejenga uhusiano wa karibu na Mungu tangu kuzuiliwa mwaka 2015 na kwamba alikuwa amesilimu na kuswali mara tano kwa siku.

kwa mujibu wa wakili wake ,wakati wa kukamatwa kwake, mwanamke huyo mwenye miaka 25 sasa alikuwa ndio tu amejiunga na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) kusomea masomo ya biashara.

"Mwanamume huyo aliyeuawa alikuwa na miaka 24 wakati huo alikuwa mjane na alikuwa anategemewa na ndugu wengine, haki ilitakiwa kutekelezwa," wakili wa mashtaka amesema

Akijitetea mahakamani hapo mwanamke huyo amesema kwamba mgogoro kati yake na marehemu ulizidi baada yeye kugundua kadi ya hospitali iliyoashiria kwamba Mohammed alikuwa anapokea matibabu ya Ukimwi.

Amesema baada ya kumwuliza alimgombeza huku akimwambia heri wafe wote kuliko hali yake ya Ukimwi itambulike hadharani.

Amesema alimchoma kisu mpenzi wake baada ya kisu cha kutumiwa jikoni kumwangukia wakipigana na hapo akamdunga kisu mara kadhaa.

msichana%2Bpic.jpg
 
Totally sad walahi!
Hasira hasara sana!
Ehhh Mola wangu tuepushe walahi
 
Adhabu ni kali sana kulingana na tukio lenyewe.... walitakiwa waangalie na utu bila kutumia hasira... akate rufaa.
 
Hii kesi ihamishiwe Tz ndo haki itatendeka
 
Adhabu ni kali sana kulingana na tukio lenyewe.... walitakiwa waangalie na utu bila kutumia hasira... akate rufaa.
Yani marehemu alimwambukiza mwenzake UKIMWI au mwenzie hakuwa na maambukiizi?maana dawa zinasaidia sana...sad.
 
Yani marehemu alimwambukiza mwenzake UKIMWI au mwenzie hakuwa na maambukiizi?maana dawa zinasaidia sana...sad.
Marehemu alimwambukiza mwenzake UKIMWI, baada ya kujua dada ndio hivyo akapanic na yote hayo kutokea.... ndio maana nasema wangeangalia na ubinaadam adhabu kubwa... very sad indeed.
 
Kwaio kesi imekabilika baada ya mshtakiwa kua kalibu na mungu na kuswali swala tano duuh"
 
Marehemu alimwambukiza mwenzake UKIMWI, baada ya kujua dada ndio hivyo akapanic na yote hayo kutokea.... ndio maana nasema wangeangalia na ubinaadam adhabu kubwa... very sad indeed.
Du
 
Before all,msipende kumuona binti mbaya,fuatilieni sababu za kuua na mazingira ya kuua
 
Back
Top Bottom